Baada ya kutangazwa kuwa
mshindi wa Urais nchini Kenya jumamosi iliyopita, jana jumapili march 10
2013 Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu.
Standard Media wameripoti
kwamba Rais huyu wa awamu ya nne aliwasili Kanisani huko Kiambu akiwa na
ulinzi mkali ambao unalingana na levo yake ya Urais.
Vilevile William Ruto ambae anatarajiwa
kuapishwa kama Makamu wa Rais alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu
kanisani jijini Nairobi.
Ruto alimwaga machozi
wakati aliposimama mbele ya umati kutoa ushuhuda wa ushindi wao pamoja
na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania.
No comments:
Post a Comment