Tuesday, May 14, 2013

KILICHOJILI JANA MAHAKAMANI WAKATI JIDE ALIPOENDA KUSIKILIZA MASHTAKA YAKE HIKI HAPA                                         Jide na Mumewe wakiwasili mahakamani leo.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee(Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
 
Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment