Uchaguzi wa bunge nchini Djibout unafanyika leo ambapo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 upinzani unashiriki.
Uchaguzi huu unafanyika miaka miwili baada ya rais Ismail Omar Guelleh kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa tatu.
Chama chake cha PRP kimekuwa kikishinda uchaguzi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mnamo mwaka 1977 kutoka mikononi mwa Ufaransa.
Upinzani
umekuwa ukisusia uchaguzi kwa madai kuwa hakuna uwezekano wa kushinda
katika mfumo wa vyama vya wafuasi wa mirengo tofauti serikalini chini ya
rais Guelleh.
No comments:
Post a Comment