Baada ya kifo cha Goldie Harvey
msanii ambae pia alikua mwakilishi wa Nigeria Big Brother Africa 2012,
mwanaume aitwae Andrew Harvey amejitokeza na kusema Goldie alikua mke
wake baada ya kufunga ndoa ya siri mwaka 2005 na walikua wanatarajia
kupata mtoto wao wa kwanza 2013.
Pamoja na kwamba Goldie
inajulikana alikua mpenzi wa CMB Prezzo wa Kenya baada ya kutoka Big
Brother na hata Prezzo kuthibitisha mpango wa kumuoa, mume huyo amesema
hakua na wasiwasi wowote kuhusu ishu zozote zilizoendelea kati ya Prezzo
na Goldie manake alikua anafahamu kwamba Prezzo alikua sehemu ya
mchezo, ni kama movie… na kusingetokea chochote kwa sababu Prezzo alikua
anapenda tu kusema chochote ili apate attention, hata Goldie alimwambia
walikua wanafanya kazi tu.
Andrew ambae ni raia wa England
alikua kwenye mipango ya kuchukua uraia wa Nigeria kabla ya kuhamishiwa
Malaysia ambako ndipo anapofanya kazi na kuishi kwa sasa lakini Goldie
tayari alikua ana uraia wa U.K hata kabla hawajakutana na Andrew manake
aliwahi kuishi na kusoma U.K
Andrew ambae yuko Malaysia kwa sasa amesema wiki hii ndio atawasili Nigeria kwa ajili ya mazishi.
No comments:
Post a Comment