Friday, February 15, 2013

Picha ya mrembo aliyeuawa na mpenzi wake Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius


Hii ni picha ya mchumba wa mshindi wa medali ya dhahabu wa riadha ya walemavu wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, aliyeuliwa kwa risasi leo asubuhi na mpenzi wake huyo.
Gazeti la Beeld limeripoti kuwa mwanariadha huyo Pistorius alidhania mpenzi wake huyo,Reeva Steenkamp waliyedumu naye kwa mwaka mmoja kuwa ni jambazi aliyevamia nyumbani kwake Pretoria. Reeva alikuwa mwanamitindo wa nchini Afrika Kusini aliyekuwa ameanza kupata mafanikio.


Oscar na Reeva
Oscar na Reeva
Amefariki kutokana na majeruhi mkononi mwake na kichwani na tayari Pistorius amekamatwa na anakabiliwa na tuhuma za mauaji.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment