Wednesday, February 6, 2013

BAADA YA VURUGU BUNGENI FEB 4, HII NDIO KAULI YA SPIKA SIKILIZA


 

Spika wa bunge Anne Makinda amesema taasisi ya bunge inalaani vurugu zilizojitokeza bungeni february 4 2013 na kusababisha kuahirishwa kwa kikao cha bunge wakati wa mjadala wa mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) kuhusu upatikanaji maji katika jiji la Dar es salaam.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu february 5 2013 Spika Makinda kasema katika kikao cha dharura cha kamati ya uongozi kilichofanyika feb 4, kimelaani hizo vurugu na kuamua kupeleka hiyo ishu kwenye kamati ya haki, kinga na madaraka ya bunge ili kufanya uchunguzi na kuwasilisha bungeni matokeo ya uchunguzi huo.

Jingine lililojadiliwa na kufanyiwa maamuzi ni kamati kusitisha uwasilishwaji wa hoja zote binafsi za wabunge zilizotakiwa kuwasilishwa katika mkutano huu wa bunge ili kuepuka vurugu zinazoweza kutokea tena.

Baada ya hayo maelezo wabunge kadhaa walisimama na kuomba muongozo wa spika akiwemo mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliyehoji kuenguliwa kwa hoja yake, pia mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyetaka kujua hatua zilizofikiwa katika rufaa za wabunge zilizokatwa kupinga maamuzi mbalimbali ya spika.

Namkariri mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisema “sasa kama fujo zinatokea bungeni na kupelekea hoja yangu kuondolewa, kamati iliyopaswa kukaa kuzungumza ni kamati ya maadili sio kamati ya uongozi, kamati ya uongozi kimsingi haina mamlaka ya kuondoa hoja yangu kwenye ratiba ya shughuli za leo, mh Spika naomba muongozo wako”

Mbunge Tundu Lissu alisema “kwa taratibu za kanuni za bunge, mbunge ambae haridhiki na uamuzi wa spika anatakiwa akate rufaa na naomba muongozo wako, rufaa zaidi ya 10 ambazo zimekatwa dhidi ya maamuzi ya kwako spika na muheshimiwa naibu spika… za tangu mwaka 1011, za mwaka jana, zitaamuliwa lini… ni lini utaitisha kikao cha kamati ya kanuni ili kisikilize hizo rufaa ambazo mmekatiwa”

BOFYA HAPA KUSIKILIZA
https://soundcloud.com/ayo2013/www-millardayo-com-nassari
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment