Mashauriano
kuhusu kuundwa kwa serikali mpya nchini Tunisia yanakusudiwa kuanza
tena. Waziri mkuu Hamadi Jebali anataka kubuni utawala wa kiteknokrasia.
Mfumo huu wa kiteknokrasia hujumuisha utawala unaongozwa na wahandisi,
wanasayansi na wataalam wengine. Lakini hatua hiyo inapingwa na kiongozi
wa chama chake cha Ennahda, Rached Ghannouchi. Bwana Jebali ametishia
kujiuzulu iwapo uamuzi wake, anaotarajia kuwa suluhisho la kisiasa
nchini humo, utaendelea kupingwa na Ennahda.
Mzozo wa
kisiasa ulizuka baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa upinzani
nchini humo, Chokri Belaid. Familia ya Bwana Belaid ilikilaumu chama
hicho kwa kupanga mauaji yake. Chama hicho cha Kiislamu cha Ennahda
kimegawanyika kati ya walio na msimamo wa kadri, wakiongozwa na waziri
mkuu, na wale wenye itikadi kali, wanaoongozwa na Bwana Ganouchi.
No comments:
Post a Comment