T A N G A Z O | ||
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia
watu wote wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa
(QT) mwezi Novemba 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea kwamba kipindi
cha usajili kitaanza rasmi tarehe 01/01/2013 kwa ada ya shilingi
35,000/= kwa CSEE na 20,000/= kwa QT.
Kipindi cha malipo bila adhabu kinaishia tarehe 28 Februari 2013.
|
Friday, February 22, 2013
Jisajili Hapa Kwa wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea Kwa huraisi
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Upinzani nchini Djibout kushiriki uchaguzi wa bunge leo baada ya kususia kwa miaka 10.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Thursday, February 21, 2013
Jack wa Chuzi amdhalilisha Isabale Kuhusu wanaume anaotembea nao Isabela
Kauli hiyo imekuja mara baada ya mwandishi wa DarTalk, kuzungumza na Jack juu ya maneno ya chini chini yanayosambazwa na Isabela juu yake, yanayodai kuwa alisababisha kumuachananisha na bwana ake.
Jack alidai kuwa kamwe hawezi kutembea na wanaume wanatoka na msanii huyo kwani hawana ubora huku wengi ni walala hoi wasiyojiweza hata kimaisha.
Alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa kutokana na hali ya uchafu aliyonayo msanii huyo, hakuna mwanaume analiyewahi kutoka na yeye anayeweza kumtamani kwani ana mwili ambao hata mvuto hauna.
“Sijawahi kutembea na bwana wa Isabela sasa inakuwaje anazungumza mambo ya uongo tena ya chini kwa chini hana lolote nahisi anatafuta jina yeye wanaume zake wote walala hoi sasa itakuwaje watoke na mimi wakati hawana cha kunipa,” alihoji Jack.
Hata hivyo kwa mujibu wa maneno ya Isabela alidai kuwa Jack aliwahi kumfanya asielewane na mpenzi wake baada ya kumtaka kimapenzi huku akijua wazi kuwa anatokana na yeye miaka yote.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
HICHI NDO WALICHO SEMA WEMA NA AUNT EZEKIEL KUHUSU PICHA WALIZOPIGWA WAKIKATA 'MAUNO'
“Sisi tumecheza tumefurahi tu hawa waliofunga mtaa kututazama watakuwa wanataka kuona mavituzi yetu,” alisema Wema.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Acheni kutibiwa kwa Waganga wa Jadi nendeni Hospitali: Mama Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete |
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Lindi mjini kujenga mazoea ya kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara na kuachana na tabia ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi na kushikana uchawi kutokana na maradhi yanayowasumbua.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alitoa rai hiyo jana alipokuwa akiongea kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Matopeni na Wailesi zilizopo wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku saba katika wilaya ya Lindi mjini ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC.
Aliwasihi watu wenye tabia ya kutopenda kupima afya zao wakati wanaumwa na wale wenye tabia za kukimbilia kwa waganga wa jadi huku wakijua fika kuwa ni wagonjwa waache kwani wanaweza kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na kupona.
“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna Ugonjwa wa Ukimwi, muache suala la kushikana uchawi katika hili kwani ugonjwa huu haupatikani kwa kurogwa. Mtu mwenye virusi vya ukimwi anapimwa kinga za mwili za kupambana na magonjwa ( CD4) kama zipo chini atapewa dawa za kuongeza na akitumia dawa atakuwa na nguvu na kuweza kufanya kazi zake kama zamani jambo la muhimu asipitishe muda wa kuzitumia” , alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa jamii nzima inahusika katika ulezi wa watoto lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hivi sasa watu wamebadilisha mienendo ya maisha kila mtu anahangaika kulea mwanawe. Na kuwasihi wakazi wa Lindi kufuata maadili ya zamani ya kuwalea watoto kwani mtoto wa mwenzako ni wako .
“Ni jukumu la jamii nzima kuwalea watoto wao kwa kufuata mila za kitanzania , wazazi ambao wakiambiwa kuwa watoto wao wanamienondo mibaya na kuja juu badala ya kuzifanyia kazi taarifa hizo waache tabia hiyo kwani watoto wakilelewa vizuri hata shuleni watakuwa na maadili mazuri na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao”, alisema.
Kuhusu ufanyaji kazi kwa ushirikiano Mama Kikwete aliwataka wananchi hao kuachana na mambo ya siasa kwani uchaguzi umeshapita hivyo basi wafanye kazi za maendeleo kwa na kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi.
Mama Kikwete alihoji, “Hawa wazungu manaowaona wanakuja Lindi kufanya kazi wamekuja kujitolea ni jambo la muhimu kujitolea kufanya kazi za maendeleo, ukiambiwa kuna ujenzi wa shule, Zahanati wewe nenda ukajitolee usiseme ile si kazi ya Serikali sasa Serikali ni nani kama si wewe mwananchi?”.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 – 2015 Diwani wa kata ya Matopeni Suleiman Namkoma alisema kuwa idadi ya watoto wanaoanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka 45 hadi 60, kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba kutoka 20 hadi 43, kuongezeka kwa barabara zinazopitika kipindi cha masika na kiangazi na kuimarika kwa miundombinu na barabara za mifereji.
Namkoma alisema, “Tunakabiliwa na changamoto za uchache wa wataalam wa kada mbalimbali ngazi ya kata na jamii kukosa wataaluma wa huduma stahiki, ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa ngazi ya kata, ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, kuchelewa kwa ruzuku ya Serikali kuu na makusanyo madogo ya Halmashauri na upungufu wa walimu wa shule ya msingi”.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mikumbi Zahara Suleiman alisema kuwa katika kata hiyo kuna vikundi vingi vya maendeleo lakini kwa mwaka 2010/2013 hakuna vikundi vilivyokopeshwa na Seambavyo ni Ayayoli na Mafundi Seremali.
Suleiman alisema, “Tunawashukuru wafadhili waliovikopeshwa baadhi ya vikundi vyetu vya maendeleo kwani kikundi cha Mwambao Fishing Group kilipewa na Mama Salma Kikwete boti na vifaa vya kuvulia vyenye thamani ya shilini milioni 57 na kikundi cha Uganda kilipewa pesa kutoka MACEP shilingi milioni 15”.
Katika mkutano wa kata ya Mikumbi Mjumbe huyo wa NEC aliwapokea vijana 18 waliokuwa wanachama wa CUF na kujiunga na CCM. Akiwa katika kata za Matopeni, Wailesi na Mikumbi alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM 43 , Umoja wa vijana 60, Umoja wa Wanawake 22 na Jumuia ya Wazazi 59.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Kampuni ya Deloitte yafanya Utafiti wa Teknolojia na Mawasiliano kwa Miezi 18-24 Ijayo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
RAIS WA KENYA AZINDUA BARABARA YA MWAI KIBAKI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
PICHA ZA NGONO ZA RAYUU ZA SAMBAA MTANDAONI
MTANDAO wetu, umezinasa picha kadhaa za msanii Rayuu zinazomuonesha akiwa kwenye tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajajulikana mara moja, ambazo kati ya hizo nyingine hazifai kuonekana machoni mwa watu kutokana na uvunjaji wa maadili.
Picha hizo zimeonekana kwenye mtandao mmoja maarufu wa nje zikiwa kwenye utata mkubwa huku mwanaume anayeonekana akiwa ni raia wa Tanzania, kutokana na utata wa wa mtandao huo ambao unahusika zaidi na picha za ngono. Mtandao huu baada ya kuzipata picha hizo, ulifanya uchunguzi kwa kumtafuta muhusika ili kuzungumza naye, ambapo hata hivyo mwenyewe alionekana kushutuka kwa madai kuwa hajui picha hizo zimetoka wapi.
Rayuu alidai kuwepo kwa picha hizo kwenye mitandao ya ngono anahisi wasi kuna baadhi ya watu wanataka kumchafua kwani hajawahi kushiriki kwenye picha yoyote ya ngono kama picha hizo zinavyomuonesha.
“Jamani mbona naonewa sana hizo picha mimi sijui zimetoka wapi, kwanza kama nimefanya mapenzi mimi watu kiwanawahusu nini acha wazitazame sina muda nao napenda kufanya mambo yangu siku zote,” aliongeza.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Wednesday, February 20, 2013
Hiki ndio alichosema Dr.Cheni Kuhusu Kurudi kwa Lulu Shule Rasmi
Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake
Alisema kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo
Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele
"Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuidumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa akifanya mambo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia" alisema
Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ananafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake
Akizungumzia kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Tuesday, February 19, 2013
HALI ILIVYO KUWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JANA KATIKA KESI YA SHEKH PONDA
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.