Picha ya pamoja mara baada ya Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) leo kuzindua  huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi  ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
 Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimpokea Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe mara baada ya kuwasili KIA tayari kwa uzinduzi 
Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe akishuka kwenye ndege ya Qatar kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa ameambatana na Mkewe pamoja na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 Ndege ya Qatar ikiwasili kabla ya kuzinduliwa rasmi KIA.
 Ikifanyiwa shower kwa mbwembwe zote.
 Wageni waalikwa mbali mbali wakisubiri kushuhudia uzinduzi huo.
Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Novatus Makunga akizungumza jambo  na Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima,Bw.Absalom Kibanda.
Baadhi ya Wanahabari Waandamizi wakiwa kwenye uzinduzi huo mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).