Tuesday, July 24, 2012

Baba amfumania Mama akizini na mwanaye; Awaua wote


Mkazi wa Kijiji cha Ng’hoboko, Stephano Mihulu (60) anadaiwa kumfumania mkewe na akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa na kuwaua kwa kuwakata mapanga.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita (40) ambaye ni mke wa mtuhumiwa na Boyayi Stephano (27) ambaye ni mtoto wake.

Akizungumza jana, kamanda alisema Mihulu alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake ndipo alipoghadhabika na kuwashambulia kwa kuwakata mapanga na kisha kuwachinja shingoni.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda, tukio hilo ni la saa 7 usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Ng’hoboko wilaya ya Meatu mkoani hapa.

Baada ya kufanya mauaji hayo, inadaiwa Mihulu alitembea kwa miguu umbali wa kilometa 18 kutoka kijiji cha Ng’hoboko hadi makao makuu ya wilaya ya Meatu mjini Mwanhuzi, kwenda kujisalimisha kwenye kituo cha polisi cha wilaya hiyo.

Kamanda alisema mtuhumiwa alikabidhi silaha ambazo ni panga na fimbo alivyotumia kufanya mauaji hayo.

Alisema Mihulu alitembea kwa miguu kuanzia saa 7 usiku hadi asubuhi kwenda kituo cha polisi kwa madai kuwa hakutaka kuwasumbua polisi na kwamba yeye ndiye mhusika wa mauaji hayo.

Katika tukio lingine la kifo, kijijini Ipililo tarafa ya Mwagala wilayani Maswa, mkazi wa kijiji hicho Lugate Lazaro (45) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake Yohana Lazaro (9) mwanafunzi wa shule ya msingi ya Ipililo B na kusababisha kifo chake.

Inadaiwa kuwa mtoto Yohana alipigwa na baba yake kwa kuchelewa kurejea nyumbani baada ya kutoka shule kutokana na michezo njiani na wanafunzi wenzake. Kutokana na kipigo hicho, hali ya mtoto huyo ilikuwa mbaya mpaka saa 10 alfajiri ya kuamkia jana alipofariki.

Polisi inaendelea na uchunguzi wa matukio hayo na mara baada ya uchunguzi kukamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayowakabili.

via HabariLeo
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment