Thursday, July 26, 2012

MTOTO WA AJABU MWENYE VICHWA VIWILI AZALIWA TANZANIAMwanamke mmoja amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili katika hospitali teule ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Mganga Mkuu wa hospitali ya DDH Bunda, Dk. Willam Krekamoo, amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Sarah Abenenego (16), mkazi wa mtaa wa Chiringe, mjini Bunda.


Dk. Krekamoo alisema mwanamke huyo alipokelewa hosptilini hapo usiku wa kuamkia jana akiwa anaumwa uchungu, na kwamba muda mfupi alijifungua mtoto wa kike akiwa na vichwa viwili, midomo miwili, macho manne na masikio manne.

Alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa pia na mikono miwili na miguu miwili na kwamba baada ya muda mfupi alipoteza maisha.

Alisema uchunguzi unaonyesha kuwa ujauzito ulikuwa wa miezi saba na huo ulikuwa ni uzazi wake wa kwanza na kuongeza kuwa hali ya mwanamke huyo inaendelea vizuri.
 
 
via: NIPASHE
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment