Friday, July 6, 2012

FACEBOOK MTANDAO WA KIJAMII KUFUNGWA TAREHE 15/7/2012


Najua kwamba taarifa hii inaweza kumshtua kila mtu ambaye amekuwa memba wa mtandao huu kwa kipindi kirefu ila kwa hapa hakuna budi kukubaliana na huyu mtu ambaye aliuleta mtandao huu kwenye internet na sisi kujoin.

Nilikuwa naipitia habari hii huku picha ya Mark Zurkerberg ikiwa pembeni akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari nje ya ofisi yake na kusema "Mtandao huu umekuwa ukinisumbua sana maishani mwangu kwa kuwa kuna wengi wamekuwa wakilalamika kila siku. Tuliweka kikao kizito na kuamua kwamba ni lazima tuufunge mtandao huu wa Facebook kwa sasa. Kilikuwa ni kikao kigumu na kizito na hata kuufikia uamuzi huo lilikuwa ni jambo zito, ila kwa sasa hatuna jinsi. Ni lazima tuuzime ifikapo tarehe 15/7/2012" Mark alisema na kuendelea. 

Najua wengi wanaweza wasiwe na furaha, ila ningependa kuwaambia watu kwamba kwa sasa inawapasa kuchukua kila picha ambazo wanazo kwenye facebook kwa sababu baada ya tarehe hiyo hawataweza kuziona tena. Ni wakati sasa wa watu kuwasiliana, kukutana na kutengeneza urafiki wa kweli" Mark alisema mbele ya waandishi wa habari.
Najua kama haujawahi kuisikia habari hii utakuwa umeshtuka kama ambavyo mimi nimeshtuka. Kipindi cha nyuma nilikuwa nikipuuzia kwa sababu tarehe ambazo zilikuwa zikitangazwa kwa mtandao kufungwa wala haukufungwa. Nafikiri kwa sasa inaweza kuwa kweli na si porojo kama ambavyo ilivyokuwa mwanzo kwa sasabu ni Mark Zuckerberg mwenyewe ndiye ameongea hayo pamoja na msaidizi wake Bwana Avrat Humarthi.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment