Tuesday, July 17, 2012

CHAMA CHA ADC CHA DHAMINIA NA WANACHAMA ZAIDI YA 250 MARA


Mkoa wa Mara umevuka lengo la wanachama waliojitokeza kukidhamini chama cha (ADC) ambapo jumla ya wanachama waanzilishi 250 kutoka wilaya za Mkoa wa Mara walijitokeza kukidhamini na kuizidi mikoa ya Mwanza,Tanga na Pemba ambapo tayari chama hicho kimeshakwenda kutafuta wadhamini.
Mara baada ya kutangazwa kuvuka lengo la wanachama walijitokeza kukidhamini chama kipya cha siasa hapa Nchini cha Alliance Democratic Change (ADC) shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Musoma club Kaimu Katibu mkuu wa chama cha ADC Kadawi Lucas Limbu aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha ni namna gani walivyo tayari kwa ajili kutaka mabadiliko.

Ujio wa chama hicho unatajwa kuja mara baada ya vyama vingi vya siasa vilivyoanzishwa hapa nchini kuonekana kuwa na ubinafsi na kushindwa kuwashirikisha viongozi wengine katika ngazi za chini hasa kwenye masuala ya ruzuku na uwezeshaji pamoja na vyama hivyo kushindwa kufikia malengo ya kuanzishwa kwake na kutokukidhi yale ambayo wananchi wanayatarajia kutoka katika vyama hivyo.
 
Kwa mujibu wa viongozi wa ADC, Chama hicho kinatarajia kuwa mfano wa kuigwa katika kuwashirikisha wananchama wake na viongozi katika kada zote na iwapo chama cha hicho kitakamilisha masharti waliyopewa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa hapa nchini, kitakuwa chama cha 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment