Wednesday, January 2, 2013

Zaidi ya 60 wafa wakikaribisha mwaka mpya, Ivory Coast


 
 

Maafisa wa serikali nchini Ivory Coast wanasema  takriban  watu 60 wamefariki wakati wa mkanyagano wa sherehe za mwaka mpya mjini Abidjan. 

Wengine 50  walijeruhiwa katika  mkasa huo ambao ulitokea mapema  Jumanne katika wilaya ya Plateau kwenye uwanja wa mpira ambapo watu walikusanyika kujionea fataki zikirushwa kuukaribisha mwaka mpya. 

Televisheni ya AIP nchini Ivory Coast inaripoti kwamba wengi wa waathirika walikuwa vijana. Wazazi wakiwa na huzuni walikwenda kwenye uwanja wa mpira wakiwatafuta watoto wao.
Walioshuhudia wamesema polisi walijaribu kuwadhibiti watu waliohudhuria sherehe za mwaka  mpya lakini vurumai zilizuka na kusababisha watu kukanyagana. Haikufahamika mara moja ni nini kilikuwa chanzo cha mkanyagano huo

Rais Alassane Outtara wa Ivory Coast ameeleza kuwa vifo vya watu hao ni msiba wa kitaifa na amesema  uchunguzi utafanyika.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment