Wednesday, January 2, 2013

STORY KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA MAISHA CLUB KWENYE SHOW YA DIAMOND



Jana Usiku ndani ya maisha club palikuwa na show kubwa ya Usiku Wa Wasafi ila haikwenda kama ilivyo pangwa na msafi Diamond.Watu waliingia club hio mapema na tayari kwa show kali kutoka kwa Diamond. Show ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza, Kundi kubwa la vijana wasiojulikana walianzan kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond. Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi Bestizo Mkononi.Bestizo ni Camera Men na Social Media Personal Wa Diamond kupitia Thisisdiamond.com. Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.


Chid Benz aliongea na watu na kusema sio kitu kizuri kufanya fujo kwenye onyesho la msanii kama Diamond.Kwani kama una chuki na Diamond mfate mtaani na sio kwenye show yake kwani unaweza kuleta matatizo kwa mashabiki wasio na hatia. Pia Chid Benz alimtuliza Diamond na kumuomba apande kwenye stage kumaliza show na kuburudisha fans waliolipa na kuja kumuona mtu wao.

Vitu vya thamani kama Cheni,Pete na Camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na Uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond Kuharibika. Skiliza Interview Yote Power Jams Ya EastAfricaRadio Leo Saa Saba Mchana.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment