Monday, January 14, 2013

WANAFUNZI 1,400 WASHINDWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA KWA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA


Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za wilaya hiyo zilizopo Buswelu ilemela jijini Mwanza.

  Wiki moja baada ya kuanza kwa muhula wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2013 zaidi ya wanafunzi 1,400 kati ya 6,000 waliofaulu kujiunga kuingia kidato cha kwanza wameshindwa kuanza masomo kutokana na uhaba wa zaidi ya vyumba 24 vya madarasa.

Hilo limebainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela  Bi. Amina Masenza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya wilaya yake kwa msimu wa 2005 hadi 2012 mbele ya waandishi wa habari.

Baada ya kuwepo kwa uhaba huo wa vyumba vya madarasa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela imeanza mikakati ya ujenzi wa vyumba hivyo 24 vya madarasa unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu kwa lengo la kuweza kuchukuwa wanafunzi wote walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari katika kata tisa za Halmashauri hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa Mkurugenzi wa wilaya yake na Wataalamu wa Idara ya Elimu kwa kushirikiana na Idara ya Uhandisi tayari wapo katika shule husika kuendelea kusimamia ujenzi wa vyumba hivyo ili uweze kukamilika katika wakati uliopangwa.



MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment