Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika
kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya
upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe
shughuli za leo hadi jioni ilisema,
“Tanzania imegeuka chini ya
usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara
wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho,
kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.
No comments:
Post a Comment