Thursday, May 30, 2013

NECTA yatangaza upya Matokeo ya Kidato cha Nne 2012


 ANGALIA KWA KUBOYEZA  HAPA CHINI

BONYEZA HAPA
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HIVI NDIVYO MWAKILISHI WETU KATIKA BBA ALIVYOJIACHIA BAFUNI NA DILISH. WACHEKI HAPA




Dillish na Nando wakioga
Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time).
 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.

Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uruzi wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania.
Dillish
Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger. Lakini second kadhaa baadae akafuta kauli yake na kumwambia kuwa alikuwa anatania. Really?!

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi kukumbwa na Eviction.

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Wednesday, May 29, 2013

NESI ANASWA KATIKA JARIBIO LA KUMTOA MIMBA MWANAFUNZI!


 
Mwanafunzi akiwa kitandani tayari kwa kutolewa mimba
MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam.
 Nesi akidhibitiwa na polisi…
Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitutumia ujumbe  wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
Nesi akiwa chini ya ulinzi….

Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.
Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na  pesa mkononi.
Timu ya waandishi wetu wa habari  pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe , walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.
Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.
Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo.
Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.
Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.
Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
 
Vifaa vilivyotumika….
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.
Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.
“Tumekuwa tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika eneo lake.
Safari ya kwenda polisi kwa mahojiano ilianza hapo huku muuguzi huyo akiwa na ‘ushahidi’ wake mkononi. Muda mwingi alionekana asiyeamini macho yake kwa kile kilichomtokea.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MSANII WA KIZAZI KIPYA MAREHEMU ALBERT MANGWEA KUZIKWA MOROGORO ALIKOZIKWA BABA YAKE.


 
KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na baba yake mdogo kupitia East Africa Radio leo asubuhi, mazishi ya rapper Albert Mangwea aliyefariki jana katika hospitali ya St. Helen jijini Johannes
burg, Afrika Kusini yanaweza kufanyika mjini Morogoro.

“Tumekubaliana kwamba tumelazimika kuzika Morogoro kwasababu huyu kaka yetu ambaye ni baba wa marehemu tumemzika pale Morogoro na familia yote ya marehemu ipo pale Morogoro. 

Lakini hapa Dar es Salaam tutafanya mapokezi na msiba utakuwa hapo kwa kaka yangu ni sehemu za Mbezi hapo, kwahiyo tutakuwa kwa kaka yangu anaitwa David Mangwea,” amesema.

Ameongeza kuwa taarifa hizo za msiba nao walizipata jana jioni lakini bado hawajawa na uhakika ni vipi mwili wa marehemu utaletwa nchini kutokea Afrika Kusini.

“Kitu tunachokifanya na tumewaagiza tu hao vijana wetu waliopo hapo Dar es Salaam wajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini kuona namna gani ambavyo tunaweza kupata more information na kiasi kwamba tukaweza kujua namna gani msiba utakuja hapa.”

Mpaka sasa bado haijajulikana mwili wa marehemu Mangwea utakuja lini nchini.

CHANZO JUMA MTANDA BLOG
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEHA.....



Jina lake halisi ni Albert Keneth Mangweha, ana asili ya Ruvuma
 (Mngoni) lakini alizaliwa Mbeya 16 Novemba 1982 akiwa mtoto 
wa mwisho. Kwa baba yake alikuwa mtoto wa 10 na kwa mama
 ni mtoto wa 6 kuzaliwa.

Akiwa na miaka 5 alihama Mbeya na kuhamia Morogoro na kusoma
 Shule ya Msingi Bungo hadi darasa la 5 na kisha kuhamia Dodoma
 akiwa na Baba yake na kumalizia Shule ya Msingi Mlimwa.
Alisoma Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

KAKA YAKE NGWAIR ANATARAJIWA KUSAFIRI LEO HADI SOUTH AFRIKA KUUFATA MWILI WA MAREHEMU, PIA HAPA NDO MSIBA ULIPO KWA WAKAZI WA DAR



Habari zilizopatikana muda huu zinasema kuwa familia ya Mangwea inajipanga kutuma ndugu kwenda Africa Kusini leo (May 29) kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili wa Marehemu Albert Mangwea.
1
 

Akiongea na Bongo5 muda mfupi uliopita dada wa marehemu aitwaye Evelyn, amesema kuwa anahitajika ndugu wa marehemu asafiri kwenda Africa Kusini kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili, sababu kule hawawezi kumtoa na kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kwenda.
Kwa Mujibu wa Evelyn familia iko katika mipango ya mwisho ya safari hiyo ambayo kaka yao mkubwa na Mangwea ndiye anayetarajia kusafiri leo hii (May 29) kwenda South Africa kuufuata mwili.

“Habari mpya ni kwamba mtu atoke hapa Tanzania aende akachukue mwili kule hawawezi kuconfirm yaani kumtoa kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kutoka huku, kwahiyo ndio process zinafanywa, kaka yake mkubwa ambaye ni kaka yetu atoke hapa aende South, ndio nadhani atarudi na huo mwili. Ataondoka leo hii hii muda wowote na wakati wowote, “Alisema dada wa marehemu Albert Mangwea.

Msiba wa rapper kipenzi cha wengi Ngwea uko Mbezi Beach Goigi kwa baba yake mdogo , ukishuka goigi ukiulizia kwa mzee Mangwea kwenye msiba utaelekezwa. R.I.P
 
CHANZO : BONGO5
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Imezibitishwa Mangwear Kafariki kwa Kujioverdose Cocaine na Crack:Soma Report ya Doctor Hapa


The Medical report from Helen Joseph hospital,Dr Shirley Radcliffe  confirming that albert Mangwairdied from “alcohol toxicity” after drinking toomuch,Over-exhaustion and drugs overdose....The inquest heard that Albert 28, collapsed in the his friends home had been more thanfive-times the legal S.A drink-drive limit with 416mgof alcohol per 100 millilitres of blood in hissystem....
Radcliffe described thereasons for ICU admission included hypoxemia and one of his friend found “two empty vodka bottles[found] on the Car” and he hadbeen suffering from the eating disorder Bulimiafor several months before his death and endless partying session with little or no resting...sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he overdosed Heroin,Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in his blood...and his death was caused by massive heart attack and respiratory failure followed by sudden Heart stop...and end up dead within seconds! R.I.P Mangwear!

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, May 28, 2013

HILI NI ENEO LA HOSPITALI AMBALO MWILI WA MSANII MANGWAIR ULIPOPELEKWA


 
Aliyewekewa kivuli ndo aliyempeleka Msanii Albert Mangwair hospitalini na chini inaonekana tweet yake iliyoandikwa tarehe 26/5/2013. Endelea kutembelea http://www-kingsele.blogspot.com/ kwa habari zaidi...
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sababu Inayotajwa Kusababisha Kifo cha Msanii wa Music Ngwear


Ripoti kamili
Taarifa Nilizo Pata Kutoka South
Africa Kutoka Kwa Hussein
Original Ambaye Yupo Pretoria
Amesema Ngwear Amefariki Leo
Asubuhi. Alikuwa Ghetto Moja Na
Msanii M To The P.

Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa
Watu Wa Karibu Wa Ngwear
Huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, May 27, 2013

Diamond & Nay wa mitego – Muziki Gani (Official Music Video)


MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka


Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako


*******
Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
 
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
 
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
 
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
 
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
 
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
 
Matokeo ya awali
 
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
 
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
 
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
 
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
 
Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.
 
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.
Ratiba ya Bunge
 
Wakati hayo yakiendelea, ratiba ya vikao vya Bunge la bajeti imefanyiwa marekebisho na kusogeza mbele zamu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo awali, ilikuwa imepangwa kusoma hotuba yake ya makadirio ya matumizi leo, badala yake nafasi hiyo imepewa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 
Wizara ya Elimu sasa imepangiwa kuwasilisha hotuba yake Juni 4 mwaka huu, hatua ambayo inatajwa kwamba lengo ni kusubiri kutangazwa kwa matokeo hayo ya kidato cha nne na kidato cha sita.
 
Wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma, walisema hawako tayari kujadili hotuba ya wizara hiyo hadi matokeo ya kidato cha nne na sita yatakapotangazwa.


MWANANCHI
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Saturday, May 25, 2013

MWANAFUNZI WA CHUA APIGA PICHA YA "UTUPU" ILI AFANANE NA RIHANNA...JE HII NI SAHIHI....?


 
Huyu ni mwanafunzi wa chuo(jina kapuni) aliyehamua kupiga picha ya utupu ili afanane na Rihanna Katika pozi...
Mwanafunzi Huyu ambaye yeye Binafsi anapenda kujifananisha na mwanamuziki asiyeishiwa na skendo Rihanna alifikia uhamuzi wa kujimulika na kamera na hatimaye kuficha....Ila ckuzote maovu ayajifichi.....
Picha hii ilisambaa mitandaoni hasa ya kijamii na hatimaye mdau wetu alitutonya na tukaipata...

Sio mbaya kama umefanana na mwanamuziki fulani ......ILA pia sio sahihi kuiga kila kitu ambacho mwanamuziki huyo anafanya...Kwa mtazamo tuu


TUNAJIFUNZA NINI...

Je ni sahii Kujimulika na katika picha za utupu ili tuuuu ujione umekamika na kufanana na mwanamuziki fulani........?
ANGALIZO.
TUMEFICHA SURA KWA KIUSALAMA WA MWANAFUNZI HUSIKA.....ILA TUJIFUNZE
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, May 24, 2013

BATULI AFUNGUKA KUHUSU BABA WA MTOTO WAKE KUDAIWA KUWA NI RAY.


Siku za hivi karibuni kumeibuka madai kuwa actress Yobnesh Yusuph(Batuli) amezaa na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi(Ray) kwa mtoto wa Batuli anayeitwa Jaheim kudaiwa kufanana sana na Ray na hata baada ya Batuli kuweka picha za mtoto huyo facebook baadhi ya watu walitoa maoni na kuuliza mbona mtoto amefanana sana na Ray na Batuli kutotaka maswali hayo akionyesha kuchukizwa na kauli kuwa amezaa na Ray. Wiki takribani mbili wasomaji wa Swahiliworldplanet walituma ujumbe kutaka jibu kama Batuli amezaa na Ray au la!.

Swahiliworldplanet kama kawaida yake ilimtafuta Batuli na kumueleza kila kitu ukiwemo ujumbe wa mashabiki wake na muigizaji huyo kusema kuwa ni kweli mwanae amefanana sana na Ray na suala hilo pia linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzake lakini amesema kuwa hayuko tayari kuliweka wazi suala hilo kwa sasa ila atalizungumzia kwa kina siku zijazo ili watu na mashabiki wake waelewe kila kitu. "Ni kweli mwanangu amefanana sana na Ray hili linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzangu. Ipo siku nitalijibu swali hili kwa ufasaha zaidi ila kwa sasa sipo tayari kuongea chochote" alisema muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto wa aina yake. Mtoto huyo pia anadaiwa kuwa na kipaji cha uigizaji na anatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza hivi karibuni katika filamu inayoandaliwa na Batuli mwenyewe. Angalia picha ya Batuli na mtoto wake hapo chini......................

                                           Batuli katika pozi
Batuli akiwa na mwanae Jaheim anayedaiwa kufanana sana na Ray
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MUME WA MTU ANASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI





INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.

Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.


Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.


Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.

Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.

Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.

Taarifa iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya kumuondoa denti huyo.


Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.

Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.

Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.

Waandishi wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa darasani.


Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.

“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki aliniambia nije kwake.

“Naombeni mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.



Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha.

Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.

UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).

“Ndugu zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma (utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”

Utetezi wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 – KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

GPL
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MWANDISHI MAARUFU WA VITABU NCHINI NIGERIA,CHINUA ACHEBE AZIKWA JANA,PICHA ZA MAZISHI YAKE HIZI HAPA


Jeneza lilibeba mwili wa marehemu Chinua Achebe
Raisi wa Nigeria Goddlucky Jonathan
Mmoja wa waombelezaji ambaye ni muuzaji wa vitabu hapo Nigeria
 
Raisi wa Nigeria na Raisi wa Ghana wakiwapungia waombolezaji
 Mke wa Marehemu Christie Achebe
RIP Chinua Achebe..nakikumbuka kitabu cha 'Things Fall Apart'
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, May 23, 2013

Kikwete: Hata kama Mtu anaechochea Wananchi Ana Pembe Tutayakata




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mh Jakaya Kikwete leo akihutubia ktk Mkutano wa CCM mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha ktk vyombo vya Sheria.

Akiongea kwa hasira alisema kua Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe.

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, May 21, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


IMG_1585 
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara  akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Gasper Mwembezi  wa wizara hiyo. IMG_1596 
Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee (CHADEMA ),pamoja na Mhe. Ester Bulaya (Viti Maalumu-CCM)) wakiingia bungeni leo. 
IMG_1604 
Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Manaibu Waziri kutoka Wizara mbalimbali wakisikiliza michango ya wabunge wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo IMG_1625 
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Mhe. Adam Malima akijibu  maswali ya wabunge bungeni leo. IMG_1656 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Mhe. wasira akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo. IMG_3844 
Mhe. Michael Leizer (Longido),Mhe.Rita Kabati (Viti maalumu CCM) na Mhe. Deogratius Ntumazina(Ngara) wakiingia bungeni leo. 
 IMG_3920 
Wabunge wakitoka katika ukumbi wa bunge baada ya kipindi cha asubuhi kumalizika
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA


Msanii maarufu wa bongo flava Joseph Haule aka Proffesor Jay, leo hii amejiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kukabidhiwa kadi yake ya uanachama mjini Dodoma.

Click image for larger version. 

Name: Prof Jay Ajiunga Na Chadema.jpg 
Views: 0 
Size: 47.5 KB 
ID: 94612
 

Click image for larger version. 

Name: Prof Jay Na Sugu Na Mnyika.jpg 
Views: 0 
Size: 40.8 KB 
ID: 94613 
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HII NDIO KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA AJARI YA MELI YA MV BUKOBA ILIYOZAMA TAREHE 21 MAY



Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uhokoaji
  MV Bukoba ikiwa inazama ilikuwa ni tarehe 21 mei 1996
 
 Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa.

RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.
 
Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.   
 
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.  
 
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.  
 
Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi.
 
Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.   
 
Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.  
 
Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.
 
Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.

Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.