Mkurugenzi
wa Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila akionyesha alama ya V wakati
akiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU)
FFU wakiwa katika Doria.
Mwili wa aliyekuwa muuza magazeti katika eneo la Msamvu Morogoro, Ally Nzona ambaye alipigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia wakati wa vurugu za Polisi na Chadema Morogoro
Ndugu
wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake
katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa
risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro
Askari wa Kikosi cha kuzuia fujo FFU wakitoa onyo kwa waandamanaji kutawanyika
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod
Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji
vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege
Sehemu ya uamati wa watu Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege, Morogoro.
Mtu
mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa
wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia
Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamani wa CHADEMA mjini
Morogoro.
Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi. (MrokiM blog)

Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui
No comments:
Post a Comment