Dogo Janja amedrop single yake
ya kwanza ‘Yamoyoni’ toka aondoke kwenye kundi la Tiptop Connection
akiwa chini ya usimamizi wa Madee June 13 2012.
Hii single ya Dogo Janja
amezungumzia maisha yake na anasisitiza kwamba “mimi sina hila na wala
sina kisasi, ni single ya kutoa tu yale ya moyoni na ni ukweli
nimewazungumzia TipTop lakini sijawazungumzia vibaya”
Janja amesema “toka nimetoka
Tip Top kuna mtu mmoja tu ambae naongea nae vizuri hata nikimpigia simu
yangu hana makuu ambae ni Tunda Man, Madee hajawahi kunipigia simu
lakini nitaendelea kumuheshimu kama baba yangu kwenye music kwa sababu
ndio amenifanya mpaka leo nafanya hii interview, thanx sana bro umenipa
uwezo mkubwa sana kwenye muziki umenifungua upeo, najua kuandika vizuri
nyimbo mwenyewe”
Pamoja na kwamba Janja wakati
anaondoka TIP TOP aliwahi kusema hatotaka tena kumuona Madee, leo
amesema mpaka sasa hajawahi kuonana na Madee uso kwa uso ila anatamani
sana kuonana nae.
Kuhusu kauli yake ya kutotaka
kuonana na Madee tena amesema “zile zilikua hasira mwanzoni na pia
nilikua nafikiria vitu vingi sana, nilikua napakwa matope Watanzania
walikua hawajanielewa, walikua wanajua kweli mimi nimekataa shule lakini
yale matope ambayo nilikua napakwa Ostaz Juma kanimwagia maji ya
kitanashati nikawa msafi, sio kwamba nina shida ya kuonana na Madee ila
nikionana nae nitamsalimia wala mimi sina tatizo nae, tutapiga story tu hata za kimaisha kushauriana hapa na pale”
VIA: http://millardayo.com
No comments:
Post a Comment