Tuesday, August 7, 2012

MGOGORO WA ZIWA NYASA KATI YA TANZANIA NA MALAWI




Mgogoro TZ & Malawi ktk Ziwa Nyasa.
Hii ni ramani rasmi inayoonyesha eneo ambalo Malawi imeingia mkataba na Surestream Pretroleum ya England kufanya utafiti wa mafuta(eneo la kijani).

TZ iliiomba Malawi isitishe zoezi hilo mpaka mgogoro wa mpaka upite, lakini Malawi walipuuza ombi hilo na kusema hawatasimamisha utafiti huo hata TZ iseme nini sababu ziwa lote ni lao! Tanzania imejibu mapigo kwa kuionya Malawi kwamba ni mafuruku kwa utafiti huo kuvuka katikati ya ziwa sababu nusu ya ziwa ni ya TZ, na itachukua hatua zote kulinda eneo la TZ.

Kuna habari zisizothibitishwa zinazosema kwamba majeshi ya TZ pamoja na equipment yamekua yakipelekwa eneo la Mbeya kutoka sehemu mbalimbali za nchi kuanzia mwishoni wa mwezi uliopita


MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment