Niliwahi
kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali
imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza
kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama
chama cha mauaji.
Raia
watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya
yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa
CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa
mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo
vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha
toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara
ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.
States
captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many
years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot.
Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya
wengi.
John John MNYIKA,
27 August, 2012.
No comments:
Post a Comment