Wanachama
wa klabu ya Gymkhana juzi walimuondoa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ali
Mafuruki (pichani) na viongozi wenzake na kuundwa kamati ya muda
inayokaa madarakani hadi Septemba mwaka huu.
Katika
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya
viwanja Gymkhana Dar es Salaam, walifikia uamuzi wa kumuondoa Mafuruki
kwa kuiendesha klabu hiyo kibabe na kuondoa taratibu nyingi ambazo
zimekuwa kero kwa wanachama.
Hali
iliyomfanya mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, ambae ni Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), hasiwe mbiashi kujiondoa kwani
hasifanye Gymkhana kama Woorlworth ambayo ni moja ya kampuni anazomiliki
Mafuruki.
Kufuatia uamuzi huo, wanachama hao wameteua kamati ya muda itayayoongozwa na Victor Kimesera na Makamu wake Erard Mutalemwa, huku manahodha wa michezo yote wanendelea na nyadhifa zao ambao ndio wanaounda kamati ya utendaji ya Ghymkhana.
Mkutano
huo ulianza saa moja na nusu juzi usiku huku kukiwa na polisi waliokuwa
na lengo la kulinda usalama, lakini ulitawaliwa na jazba ya kumtaka
Mafuruki ajiuzuru kwa madai kuiendesha klabu hiyo kinyume na taratibu na
maamuzi mengi yamekuwa yake binafsi.
Hata
hivyo, Mafuruki baada ya kuingia katika mkutano huo aliwaambia
wanachama hao kuwa mkutano huo haukufuata taratibu hivyo maamuzi yoyote
ambayo watayachukua yatakuwa yamekiuka katiba ya klabu hiyo na kususia
kikao na kuondoka.
Wakati
akiondoka wanachama hao walikuwa wakizome, hali iliyofanya mmoja wa
wadhamini wa klabu hiyo Jaji mstaafu, Stella Longway kuchukua jukumu la
kuendesha kikao kwa mujibu wa katiba yakbu hiyo na wanachama kufukia
maamuzi ya kuwaondoa viongozi wote wa klabu hiyo.
Klabu
hiyo mbali na Jaji Stella inawadhani wengine wawili ambao ni G. Kilindu
na Ritha Akena.Wadhamini hao wana mamlaka ya kufanya kazi hiyo kwa
niaba ya wanachama wa klabu hiyo.
Kufuatia
uamuzi huo, kamati hiyo ya muda inayoongozwa na Kimesera inatarajia
kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ni kurudisha ada ya mgeni
mwalikwa ‘Guest Fees” kutoka shilingi elfu 10 hadi elfu mbili kama
zamani.
Hatua
nyingine ni kurudisha utaratibu wa timu za Gymkhana kualika timu za nje
kucheza mechi, hali ambayo uongozi wa Mafuruki ulipiga mafuruku kucheza
mechi ndani ya viwanja hivyo au timu zinazokuja kulipiwa shilingi elfu
10 kwa kila mchezaji.
Mbali
na Mafuruki kama Mwenyekiti, wengingine ni Makamu Mwenyekiti, Profesa
Primo Carneiro,Katibu Nicholas Siwingwa, Mweka hazina, Nada Margwe, Mkuu
wa wanachama, Santosh Gajjar, Mkuu wa viwanja, David Shambwe, Mkuu wa
Bar, Alfred kinshwaga na Joseph Kusaga mkuu wa kitengo cha burudani.
Wengine
ni manahodha michezo yao kwenye mabano ni Joseph Tango (Gofu),Inger
Njiru (Tenisi),Chukkapalli Sriram (Kriketi),Ivan Tarimo (soka),Deepak
Dosh (squashi) na Firoz Yusufunali (snooka)
Lakini wanachama hao wanakusudia kuwarudia wakuu wa vtengo vyote kasoro nafasi ya Mwenyekiti.
Mwisho
Conct E.Mutalemwa-Makamu mwenyekiti kamati ya muda
-+255 767210332
No comments:
Post a Comment