Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na mtandao wa vikundi vya
vijana kata ya Kibada -Kigamboni akiwaeleza jinsi Umoja wa Mataifa
unavyohusika katika maendeleo ya vijana ikiwemo kuwaelimisha haki zao,
kuwawezesha kujitambua na kujua umuhimu na kazi za mashirika ya Umoja wa
Mataifa hapa nchini.
Naibu Mwenyekiti wa kikundi cha vijana
kata ya Kibada akizungumzia changamoto zinazowakabili kama kikundi
ikiwemo ukosefu wa maktaba ambazo zingewawezesha kusoma na kujua
mashirika hayo yanafanyaje. Pia tatizo lingine ni jeshi la polisi
kuwafikiria na sheria zake ikiwemo kuwapangia muda wa kutembea,
kukithiriri kwa rushwa mambo ambayo yanachangia kuongeza uduni wa maisha
ya vijana.
Mmoja wa mwanakikundi wa vijana kata ya
Kibada-Kigamboni mwenye kipaji cha kuigiza akionyesha uwezo wake wa
kuigiza ikiwemo jinsi vijana wanavyokwamishwa kuanzia kwenye sekta ya
elimu na kujiajiri na hata hivyo Bi. Harriet Macha wa UNIC alitoa
ushauri jinsi ambavyo Shirika hilo linavyofanya kazi na serikali na
mipaka yake.
Mwanakikundi wa kata ya Kibada
Kigamboni akielezea kipaji chake cha ususi kilichompelekea kujiajiri na
kujitegemea na kuahidi kutoa mafunzo kwa wasichana wenzake.
Pichani Juu na Chini ni Bi. Harriet
Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza
na vijana Somangile-Kigamboni kutoka kikundi cha 'Kigamboni Peer
Educator Network' (KIPENET) kuhusiana na kazi za shirika hilo na huku
akipokea changamoto
No comments:
Post a Comment