Thursday, August 2, 2012

MSANII NA MTOTO WA MITAANI BALAJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA



Leo hii, maeneo ya manyanya, mtoto wa mitaani ambae pia alishawahi kurekodi wimbo (maumivu) pamoja na video yake, chini ya msaada wa fish crab producer Lamar, amepigwa nusu ya kufa na wananchi baada ya kutuhumiwa kumuibia mtu asiyejulikana aliekuwa kituo cha basi, "watu wamempiga sana, alikua keshaanza kutoka damu mdomoni, mi nimefika pale ndio wakaacha kumpiga" amesema lamar ambae alikua eneo la tukio
Balaja anatokea kahama mkoani shinyanga, mara nyingi amekuwa akiomba nauli ya kurudi kwao ambapo anadai kuishi na bibi yake, lakini kila akidakiswa nauli, kesho unamkuta tena mitaani.

VIA:  http://djfetty.blogspot.com
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment