Tuesday, August 28, 2012

JAMAA MMOJA ASINGIZIWA KAIBA SIMU APIGWA NUSU KUFA



 RAIA WENYE ASILA KALI WAKIMPIGA
HAPA BAADA YA POLISI KUFIKA
  JAMAA AKIWA NA MDADA
JAMAA AMBAE JINA LAKE LIMEIFAZIWA ALIPELEKWA KATIKA KITUO CHA POLISI WILAYANI MAGU PAMOJA NA DADA HUYO
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MSIMAMO WANGU VURUGU,RISASI,KUJERUHI NA “KUUA” MOROGORO – JOHN MNYIKA.


Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.

Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.

States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

John John MNYIKA,
27 August, 2012.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, August 27, 2012

VURUGU ZA FFU, CHADEMA MOROGORO, ZASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA



Mkurugenzi wa Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila akionyesha alama ya V wakati akiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU)
 FFU wakiwa katika Doria.
 Mwili wa aliyekuwa muuza magazeti katika eneo la Msamvu Morogoro, Ally Nzona  ambaye alipigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia wakati wa vurugu za Polisi na Chadema Morogoro
 Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro
 Askari wa Kikosi cha kuzuia fujo FFU wakitoa onyo kwa waandamanaji kutawanyika
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege 
Sehemu ya uamati wa watu Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege, Morogoro.
Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamani wa CHADEMA mjini Morogoro.

Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi. (MrokiM blog)  
Picture
Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sunday, August 26, 2012

MWENYEKITI WA VIJANA (W) CHAMA CHA MAPINDUZI ALUDISHA KADI YA CHAMA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA WILAYANI MAGU MBELE YA MH, RENATUS PAMBA DIWANI WA SINZA


Ndg, FAUSTINE JOHN MAARUFU (KOSOVO) 
Alikuwa Mjumbe Mkuu UVCCM Wilaya Pia Alikuwa Mjumbe wa Nec na Ngazi Nyingine Nyingi Katika Chama Cha Mapiduzi Alirudisha Kadi ya Chama Hicho huku akisema Alidanganya Kwa wingi wa Madaraka Ndani ya chama Siku Zote na Hadi Leo Ajaona Mabadiliko yoyote.
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO 
HAPA AKIWASILI KATIKA MKUTANO ULIYO FANYIKA KTK VIWANJA VYA SABASABA WILAYANI MAGU
 MH, DOMINIQUE BUBESHI AKIONGEA NA WANANCHI AWALI ALIKUWA KATIBU WA CUF NGAZI YA WILAYA

 

 
 WANANCHI WALIUDHULIA KWA WINGI WAKISUBULI KUMONA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU AKIKABIZI KADI KWA MH, RENATUS PAMBA
 
MH, RENATUS PAMBA AKIONGEA NA WANANCHI AMBAYE NI DIWANI NA M/KITI WA KATA YA SINZA  PIA NI M/KITI KAMATI TENDAJI JIMBO LA UBUNGO



 MH, DOMINIQUE BUBESHI AKIWA NA KOSOVO

 MH, RENATUS PAMBA AKIWA NA KOSOVO



 NA NDIPO ALIAMUWA KUONYESHA KITAMBI CHAKE WAZI ADHARANI HUKU AKIJIANDAA KUVAA GWANDA




 BAADA YA KUIVUA T-SHET HIYO WALIKUWA WAKIIFUTIA VIATU
ALIKABIZIWA CARD YA CHADEMA NA GWAKISA B. GWAKISA 

 
 HIZI NI KADI MBALIMBALI ZA CCM ZA FAUSTINE JOHN (KOSOVO)
 HII NI T-SHET ALIYO KUWA AMEIVAA IKICHOMA MOTO BAADA YA KUIVUA
 HUYU PIA ALIKUWA KATIBU MSITAFU CUF (W) NA ALIKUWA KAMPENI MANAGER JIBO LA MAGU MJINI NA JIMBO LA BUSEGA KATIKA UCHAGUZI MKUU NAYE PIA ALILUDISHA CARD


MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, August 24, 2012

MWENYEKITI WA GYMKHANA ATIMULIWA




Wanachama wa klabu ya Gymkhana juzi walimuondoa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ali Mafuruki (pichani) na viongozi wenzake na kuundwa kamati ya muda inayokaa madarakani hadi Septemba mwaka huu.
Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya viwanja Gymkhana Dar es Salaam, walifikia uamuzi wa kumuondoa Mafuruki kwa kuiendesha klabu hiyo kibabe na kuondoa taratibu nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wanachama.

Hali iliyomfanya mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), hasiwe mbiashi kujiondoa kwani hasifanye Gymkhana kama Woorlworth ambayo ni moja ya kampuni anazomiliki Mafuruki.

Kufuatia uamuzi huo, wanachama hao wameteua kamati ya muda itayayoongozwa na Victor Kimesera na Makamu wake Erard Mutalemwa, huku manahodha wa michezo yote wanendelea na nyadhifa zao ambao ndio wanaounda kamati ya utendaji ya Ghymkhana.

Mkutano huo ulianza saa moja na nusu juzi usiku huku kukiwa na polisi waliokuwa na lengo la kulinda usalama, lakini ulitawaliwa na jazba ya kumtaka Mafuruki ajiuzuru kwa madai kuiendesha klabu hiyo kinyume na taratibu na maamuzi mengi yamekuwa yake binafsi.

Hata hivyo, Mafuruki baada ya kuingia katika mkutano huo aliwaambia wanachama hao kuwa mkutano huo haukufuata taratibu hivyo maamuzi yoyote ambayo watayachukua yatakuwa yamekiuka katiba ya klabu hiyo na kususia kikao na kuondoka.

Wakati akiondoka wanachama hao walikuwa wakizome, hali iliyofanya mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo Jaji mstaafu, Stella Longway kuchukua jukumu la kuendesha kikao kwa mujibu wa katiba yakbu hiyo na wanachama kufukia maamuzi ya kuwaondoa viongozi wote wa klabu hiyo.

Klabu hiyo mbali na Jaji Stella inawadhani wengine wawili ambao ni G. Kilindu na Ritha Akena.Wadhamini hao wana mamlaka ya kufanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo.

Kufuatia uamuzi huo, kamati hiyo ya muda inayoongozwa na Kimesera inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ni kurudisha ada ya mgeni mwalikwa ‘Guest Fees” kutoka shilingi elfu 10 hadi elfu mbili kama zamani.

Hatua nyingine ni kurudisha utaratibu wa timu za Gymkhana kualika timu za nje kucheza mechi, hali ambayo uongozi wa Mafuruki ulipiga mafuruku kucheza mechi ndani ya viwanja hivyo au timu zinazokuja kulipiwa shilingi elfu 10 kwa kila mchezaji.

Mbali na Mafuruki kama Mwenyekiti, wengingine ni Makamu Mwenyekiti, Profesa Primo Carneiro,Katibu Nicholas Siwingwa, Mweka hazina, Nada Margwe, Mkuu wa wanachama, Santosh Gajjar, Mkuu wa viwanja, David Shambwe, Mkuu wa Bar, Alfred kinshwaga na Joseph Kusaga mkuu wa kitengo cha burudani.

Wengine ni manahodha michezo yao kwenye mabano ni Joseph Tango (Gofu),Inger Njiru (Tenisi),Chukkapalli Sriram (Kriketi),Ivan Tarimo (soka),Deepak Dosh (squashi) na Firoz Yusufunali (snooka) 

Lakini wanachama hao wanakusudia kuwarudia wakuu wa vtengo vyote kasoro nafasi ya Mwenyekiti. 

Mwisho
Conct E.Mutalemwa-Makamu mwenyekiti kamati ya muda
-+255 767210332
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

POLISI YAWA ONYA WATAKAO TIBUA ZOEZI LA SENSA


 
Kamishna wa polisi anayeshughulikia operesheni na mafunzo (CP), Paul Chagonja, akitangaza msimamowa polisi jana, kuhusiana na wanaofanya mpango wa kuhamasisha watu kutohesabiwa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza Jumapili Agosti 26, 2012

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

UFAFANUZI OPARESHENI YA KUWAONDOA WAVAMIZI WA ARDHI ENEO LA MADALE NA ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR ES SALAAM WATOLEWA


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kufafanua oparesheni ya kuwaondoa wavamizi wa ardhi katika eneo la Madale na zoezi la Sensa ya watu na makazi leo jijini Dar es salaam. 

UFAFANUZI OPARESHENI YA KUWAONDOA WAVAMIZI WA ARDHI  ENEO LA MADALE NA ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR ES SALAAM WATOLEWA.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
24/8/2012, Dar es salaam.

 Serikali imesema kuwa haitayavumilia makundi ya watu wanaovunja sheria za nchi kwa kuendesha vitendo vya wizi, uvunjaji wa nyumba, uporaji na uuzaji wa ardhi kinyume cha sheria katika maeneo yanayomilikiwa kihalali jijini Dar es salaam.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kutokana na uamuzi wa serikali kuwaondoa kwa nguvu wananchi waliovamia maeneo hilo.

Amesema kuwa serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa zimezingatia kanuni na taratibu za kisheria zikiwemo baraka za kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.

“ Kufanyika kwa zoezi hili si kwamba serikali ya Kinondoni imekurupuka, hata kidogo haijafanya hivyo, zoezi hili limefuata kanuni na taratibu zote za kisheria ikiwemo uamuzi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es salaam na amri ya Mahakama”

Amefafanua kuwa matukio yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo hayo kwa baadhi ya makundi ya wananchi hasa vijana waliobeba silaha za jadi kuwashambulia, kuwajeruhi na kuharibu mali za wananchi wanaoishi katika eneo la  Madale kihalali kwa lengo la kuwaondoa kwa nguvu na kuyatwaa maeneo yao ni jambo lisilokubalika nchini.

 Amesema kuwa licha ya jambo hilo kuwa la muda mrefu na serikali kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kihalali wanafanya shughuli zao bila kusumbuliwa baadhi ya wananchi wamekuwa hawakubaliani na jambo hilo na hatimaye kuanza kuyavamia maeneo ya wazi ambayo mengine yanamilikiwa na taasisi na makampuni.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo hayo lilizingatia taratibu zote ikiwemo hatua ya serikali kuwapa taarifa wahusika wote waliovamia maeneo hayo kuondoka wenyewe jambo ambalo hawakulifanya.

“Kabla ya kutumia nguvu kuwaondoa wananchi hao serikali iliwapatia taarifa ya kuwataka kuondoka wenyewe jambo ambalo walilikaidi na kuendelea kukalia maeneo hayo kinyume cha sheria.

“ Bado naendelea kusisitiza kuwa serikali ilifuata taratibu zote, kwanza tuliwashauri wamiliki halali kwenda mahakamani kisha mahakama ikatoa amri ya wavamizi hao kuondolewa na zaidi ya hapo walipewa taarifa ya kuondoka wao wenyewe jambo ambalo hawakulifanya na hii inaashria kudharau amri ya mahakama” amesisitiza Bw. Sadiki.

Aidha Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa imebainika kuwa  baadhi ya wananchi wanaoendesha vitendo hivyo vya kihalifu sio raia wa Tanzania na kukongeza kuwa tayari vyombo vya dola vinavyohusika vinaendelea na uchunguzi wa  suala hilo na tayari vinawashikilia watu 68 kwa kuhusika na vurugu hizo.

Pia ameonyeshwa kusikitishwa na baadhi ya watendaji wachache wa serikali na viongozi wa siasa wanaoshabikia na kuhamasisha suala hilo na kuongeza kuwa serikali inaendelea na uchunguzi wa suala hilo na ikibainika hathua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amevipongeza vyombo mbalimbali vya habari vinavyoendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuongeza kuwa hivi sasa wananchi wana uelewa mkubwa juu ya zoezi hilo na wako tayari kuhesabiwa.

“Navishukuru sana vyombo vya habari kwa kazi nzuri za uhamasishaji wa watu kushiriki katika Sensa ya watu na Makazi japo vipo vichache sana vinavyoendesha mijadala ya kuipinga”

Amesema maandalizi ya zoezi hilo kwa mkoa wa Dar es salaam yamekamilika licha ya kuwepo kwa  malalamiko na madai ya baadhi ya makarani wachache kutolipwa fedha za mafunzo jambo ambalo amesema mamlaka husika zinalifanyia kazi kwa kuhakikisha kuwa ukamilishaji wa uhakiki na uthibitisho wa majina yao unakamilika leo.

“Kwa upande wa jiji la Dar es salaam wengi wameshalipwa fedha zao na kwa  wale wachache ambao madai yao yanashughulikiwa nawahakikishia kuwa watalipwa kwa kuwa fedha yao ipo” amesisitiza.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

UN YATEMBELEA VIJANA KUWAHAMASISHA KUWA WAJASIRIAMALI ILI KUPUNGUZA UMASIKINI.


Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na mtandao wa vikundi vya vijana kata ya Kibada -Kigamboni akiwaeleza jinsi Umoja wa Mataifa unavyohusika katika maendeleo ya vijana ikiwemo kuwaelimisha haki zao, kuwawezesha kujitambua na kujua umuhimu na kazi za mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Naibu Mwenyekiti wa kikundi cha vijana kata ya Kibada akizungumzia changamoto zinazowakabili kama kikundi ikiwemo ukosefu wa maktaba ambazo zingewawezesha kusoma na kujua mashirika hayo yanafanyaje. Pia tatizo lingine ni jeshi la polisi kuwafikiria na sheria zake ikiwemo kuwapangia muda wa kutembea, kukithiriri kwa rushwa mambo ambayo yanachangia kuongeza uduni wa maisha ya vijana.
Mmoja wa mwanakikundi wa vijana kata ya Kibada-Kigamboni mwenye kipaji cha kuigiza akionyesha uwezo wake wa kuigiza ikiwemo jinsi vijana wanavyokwamishwa kuanzia kwenye sekta ya elimu na kujiajiri na hata hivyo Bi. Harriet Macha wa UNIC alitoa ushauri jinsi ambavyo Shirika hilo linavyofanya kazi na serikali na mipaka yake.
Mwanakikundi wa kata ya Kibada Kigamboni akielezea kipaji chake cha ususi kilichompelekea kujiajiri na kujitegemea na kuahidi kutoa mafunzo kwa wasichana wenzake.
Pichani Juu na Chini ni Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na vijana Somangile-Kigamboni kutoka kikundi cha 'Kigamboni Peer Educator Network' (KIPENET) kuhusiana na kazi za shirika hilo na huku akipokea changamoto
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, August 21, 2012

WARAKA WA RAIS WA TAFF KWA MAHARAMIA WA FILAMU


Simon Mwakifwamba
Simon Mwakifwamba Rais wa Shirikisho la Filamu Swahiliwood.
HAKUNA mtu asiyependa maendeleo ya mtu mwingine ambayo ni halali, lakini mtu anapobaini kuwa haki yake imeibiwa na kubaini mwizi ni ndugu yake ambaye yupo karibu naye upata maumivu makali yasiyosemekana, miaka inazidi kwenda filamu zinatakaa mitaani na kuifanya jamii iamini kuwa uigizaji ni kazi inayolipa kuliko kazi nyingine japo ukweli ipo hivyo lakini si kwa Tanzania, unapokuwa Tanzania kazi ya msanii haina ulinzi jambo linalotoa fursa kwa maharamia kujinufaisha.

Simon Mwakifwamba
Simon Mwakifwamba Rais wa Shirikisho la filamu akiongelea jambo fulani.
Hivyo basi kwa umoja wetu tunaungana na kuamua kwa moyo wa dhati kupigana na maharamia hawa wananyonya jasho letu pasipo huruma, kwani wanajulikana na tunaishi nao ni rafiki zetu lakini hawana huruma na sisi wanaamua kutunyonya hadi wahakikishe damu yote inamalizika kabisa na wao kuendelea kuneemeka hilo si sawa hakuna kitu cha rahisi lazima uvune kutokana na jasho lako, wasanii wamekuwa wanyonge kimaslahi pamoja na kutoa filamu zao kila kukicha hili si jambo la kulifumbia macho hata kidogo.
Tunaambiwa Maharamia wana mtandao lakini mtandao wao umefikia ukingoni kwani tayari tumeamka na kuamua kuingia katika mapambano na maharamia hawa ambao wamekuwa wakizorotesha juhudi za wananchi kubuni ajira na kujiajiri katika tasnia ya filamu, hivi karibuni mtuhumiwa aliyekamatwa na kazi za wasanii nakala kwa nakala huku akiwa na mashine za kurudufu kazi za wasanii alikuwa huru sana kwani hakuwa na hofu hata kidogo hata aliamua kufunga mitambo yake katika nyumba yake anayoishi bila kuwa na taadhari.
Jacob Stephen, Simon Mwakifwamba, Vincent Kigosi.
Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba akiwa na JB na Ray wakiongelea suala la wizi kazi za filamu.
Hivyo basi kwa niaba ya shirikisho ningependa kuipongeza serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na bunge lake tukufu kwa ujumla kwa kubeba majukumu mazito na kufanikisha kuifikisha nchi hii mahali tulipofika ikiwa ni
pamoja na
1. Kupitisha kwa kauli moja kufanya marekebisho ya katiba ya nchi
2. Kusajili na kuwapa vitambulisho watanzania
3. Kufanikisha uwezeshaji wa sensa za watu na makazi
4. Na mengine mengi
Kama wasanii tunalitambua uwezo na ukakamavu mkuu wa serekali yetu tukufu ndio maana hatusiti kuwapa pongezi zetu za dhati na kuhimiza jamii kujitokeza na kuiunga serikali yao mkono kufanikisha malengo haya kwa haraka na
ufanisi mkubwa.
.
Jacob Steven
JB mwenyekiti wa Bongo Movie Unity ni moja kati ya wanaounda timu ya kupambana na Maharamia wa kazi za wasanii.

Tukirudi kwa upande mwingine sote tunafahamu mahali sisi wasanii tulipokuwa, mahali tulipo sasa na pengine tunapotarajia kufika. Kama mtoto mchanga tulianza kwa kuketi chini, tukaanza kutambaa, tumeanza kutembea ndiyo
tunatarajia kukimbia. Nyota yetu ndio inaanza angalao kung’aa na kuwa na ndoto na njozi nzuri kwa ajili ya urithi wa
wana wetu, lakini………………
Utamaduni wa mtanzania na utanzania wenyewe unaidhinishwa kupitia sanaa, elimu kwa jamii nzima unajumuishwa katika sanaa, maadili ya kitanzania unabebwa na kusambazwa kwa jamii kupitia sanaa, dini, uungu na utakatifu unaidhinishwa katika sanaa, wana siasa wote wanatengenezwa na kukuzwa kwa kiwango kikubwa sana na sanaa.
Wafanya kazi watiifu na wenye bidii kwa jamhuri hii wanajengwa na sanaa, wagonjwa wote wanaliwazwa na sanaa, waliofiwa wanaliwazwa na sanaa, wanandoa na harusi zote zinatimizwa na sanaa, habari na utangazaji vinabebwa na
sanaa, hivyo basi sanaa ndiyo inafanya kila kitu kiwe kama vile kilivyo, inastahili kuheshimiwa na si kudharauliwa
kama vile ilivyo sasa.
Nchi za ulaya zimejikita katika kukuza raslimali watu na kuenzi kile kitokanacho na raslimali watu hawa, mtu yeyote au kitu chochote ambacho kinaweza kuwazuia hawa raslimali watu kutimiza wajibu wao, basi inakuwa jukumu la kila mtu
kutatua tatizo hilo, huu ni mfano wa kuigwa.
Sanaa ina uwezo mkubwa sana katika kuengeza pato la nchi hii kwa zaidi ya asilimia 40%, kusaidia kuengeza ajira kwa vijana kwa zaidi ya asilimia 50% kuliko sekta nyingine yeyote, kuitambulisha nchi hii kimataifa(sasa hivi kupitia
MNET na television zingine zakimataifa)Kufanya Tanzania kuwa nchi yakitalii, kuchangia kujenga nchi hii kisaikolojia (wananchi watanzania na wageni wanapata faraja na kitulizo cha akili kupitia sanaa) huu ni mchango mkubwa sana katika taifa hili.
Mazuri haya yanatamanisha, na kila mtu anatamani na iwe hivyo, yote haya yanawezekana lakini hali kiukweli si hivyo,
wasanii wanalalamika, wazalishaji wanalalamika, wasambazaji wanalalamika, watumiaji wa kazi za sanaa walengwa wanalalamika, wanasiasa wanalalamika pia, serikali inalalamika kukosa ushuru lakini MTU MMOJA au WACHACHE wanafurahi, hawa si wasanii, wala wazalishaji au wasambazaji bali ni WEZI wa kazi za sanaa. Watu wengi wanapenda nyama sana lakini bucha za nyama ni chache kuliko library za kuuza kanda Bandia (Feki) zilizodurufiwa mtaani na hata mjini, hata upofu analiona na kulifahamu hili.
Tunabani CD na kuweka nyimbo kwenye flash, memory card haya ni maandishi tunayokutana nayo kila siku ukutani na kwenye vibao popote tuendapo Tanzania nzima hili si jambo geni, jamani huu si wizi kama wizi mwingine? Huyu msanii, mzalishaji au msambazaji atalipwa vipi? Na hili ndilo jembe lake, mbona mahindi zikiibiwa shambani mkulima analia na kulalamika vikali na hatua inachukuliwa, ngombe zikiibiwa watu wanjumuika kufuatilia pamoja na polisi wakibeba bunduki, hivi huyu msanii anaibiwa hadharani, mbele za ofisi za COSOTA wapo hapo nje, mbele za vituo vya polisi utakuta kanda feki inatembezwa hadharanibila uwoga, mbona hawa wasanii pia ni watoto wa watu kama vile watoto wengine?
Rigobert Massawe
Mtuhumiwa wa Wizi wa filamu za wasanii aliyekamatwa na filamu feki mamia kwa maalfu.
Ukiuliza mbona hivi, jibu la kwanza hatuna elimu, hatujui, hatuna ufahamu na filamu au muziki ikianza inaanza na ONYO hivi wanawezaje kuona kilicho ndani na wasione onyo, hivi hii elimu itoleweje? Mbona ilani za hamna njia hapa watu wanaona lakini inakuaje hawaoni ilani na onyo inayoanza kwenye filamu? Au muziki? Madereva wa basi wanaona vithibiti mwendo zilizoko kwa umbali barabaranilakini wanashindwa kuona ilani au onyo inayosema hairuhusiwi kuonyesha kwenye halaiki ya watu ambayo anaweka mwenyewe kuburudisha wasafiri wake, viongozi wa dini wanafundisha watu wasiibe na wao ndio wananunua kazi za wizi-feki mtaani, pengine kwa kutojua kuwa ni kazi bandia
Sisi wasanii tumebaki njia panda na tunaona na kuchukulia jambo hili kama dharau na ufanyaji mambo kimakusudi na
ukatili bila ya kujali maumivu makali anayopata mwenzio.
Hata hivyo ingawa tunaumizwa na kustahimili maumivu makali kutokana na maharamia hawa wa wizi wa kazi za sanaa tunapata faraja na moyo tukikumbuka agizo la Dr. Mohamedi Gharib Bilali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania alilotoa mnamo mwezi October 2011 akiwa katika uzinduzi wa kanuni na sheria za Filamu na michezo ya Kuigiza mjini Musoma akiagizakukamatwa kwa maharamia wote wa kazi za filamu nchini kwa mbinu yoyote ile na wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Tamko hili linanguvu sana na linaonyesha uwajibikaji wa serekali ili kuokoa sekta hii ambayo sasa inayumbayumba inashiriki kilio cha samaki anayeliwa pande zote na kubakizwa mifupa tu, ila mtaji wa maskini ni nguvu zake kama
wasemavyo wahenga, TAFF, SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA WASANII TANZANIA (SHIWATAN) likishirikiana Wadau/Wasanii wa Filamu na Muziki, Kampuni za Uzalishaji filamu, Kampuni za Usambazaji wa Filamu, Kampuni zinazo miliki bendi za Muziki na watu wote wenye uchungu na uzalendo kwa pamoja tumeamuakulivalia njuga na kulishughulikia tatizo hili ipasavyo bila kulalamikia mtu, chombo au taasisi yeyote.
Hili limedhihirika wazi mnamo jumanne tarehe 7 mnamo saa tatu asubuhi pale tulipopata taarifa za kuaminika kutoka kwa watanzania wazalendo kuhusu mtu Fulani anayedurufu kazi za wasanii mbalimbali za nyimbo na filamu, kwa kauli moja tulifahamisha polisi na kwa mpangilio madhubuti tukavamia duka lake na kufanikiwa kumkamata na kukamata
kazi nyingi sana na mitambo ya kisasa aliyokuwa anatumia kufanikisha uhalifu huo.
Kazi zilizokamatwa na polisi ziko katika mfumo wa DVD na VCD, pia kulikuwa na kava nyingi za wasanii mbalimbali makasha ya kuhifadhi DVD na VCD, Baadhi ya Filamu hizo ni Hatia 1 & 2 (Hisani Muya, almarufu kama TINO),The
Glory of Ramadhani 1& 2 (Vicenti Kigosi, almarufu kama RAY), Nakwenda kwa mwanangu 1& 2 (King Majuto na JB) Oprah 1& 2, the Twins 1 & 2 zinazomilikiwa na Game 1st quality zikiwa pamoja na Muziki mpya wa Jahazi (mpenzi Chokolate, MZEE YUSUPH).
Kazi za Injili za Kampuni ya MBC Hot Media, hizi ni baadhi tu ya kazi za wasanii zilizotajwa mtuhumiwa alikutwa na kila aina ya kazi za wasanii. Hii ni pamoja na gari lilosheheni kazi bandia (feki) alilokuwa anatumia kusambazia kazi
hizo kwa urahisi.
Mtuhumiwa alifanya uharamia huu kwa kutumia akili na ujuzi wa hali ya juu na kutumia mitambo ya hali ya juu sana kiasi kwamba huwezi kutambua iliyodurufiwa na kazi halali, pia aliweka stamp inayong’aa kuthibitisha uhalali wa kazi
hizi, hii inaonekana kuwa amefanya kazi hii kwa muda mrefu sana bila ya kugundulika na mtu yeyote kiasi kwamba alikuwa anauza hadharani bila uwoga.
Shirikisho na wadau wote wanapenda kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dr. Fenella Mukangara pamoja na Naibu waziri wa Wizarawa hiyo kwa kuwa bega kwa bega nasi katika zoezi hili la msako wa maharamia, IGP Said Mwema na Makamanda wa Mikoa pamoja na OCD wote kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu za kupambana na Maharamia.
Jambo hili linaashiria kuwa maharamia hawa ni wengi na wamekita mizizi na kufanya kazi hii bila kugundulika kwa muda mrefu sana kiasi cha kuwafanya wao kuwa matajiri wenye vitu vya thamani huku wasanii maskini kama samaki
wanabaki wakilia huku wanaliwa pande zote mbili na kubaki mifupa.
Ndugu Wanahabari Kutokana na tukio hilo, Shirikisho la Filamu Tanzania na kamati yake kwa niaba ya Wasanii wote wa filamu na Muziki, Vyama Wanachama wa Shirikisho, Wasambazaji na kampuni zinazofanya kazi za Filamu na Muziki tunatoa tamko la Kulaani vikali Uharamia uliofanywa na kampuni ya Ndugu Rigobert Massawealmaarufu kwa jina la Msukuma wa hapa Dar es Salaam, ambaye amekuwa akikamatwa kila mara na kushindwa kupata adhabu stahili.
Bwana Rigobert Massawe ni mmoja kati ya Maharamia wakubwa wa kazi za filamu hapa nchini kwa kipindi kirefu, mwenye mbinu za kimataifa za uharamia, mwenye kujiamini kupita kiasi asiye na hofu na Sheria wala Serikali.Zoezi hili la kupambana na maharamia Papa kama Rigobert Massawe ikiwa na wale maharamia wadogo ambao wanajinufaisha kwa jasho la wasanii linaendelea bila kikomo, kwani tayari tumebaini maeneo maarufu kwa wizi huo ambayo ni Yombo, Tegeta, Banana, Buguruni na Mbezi mwisho tutawakamata na kuwashughulikia ipasavyo.
Aidha pia kupitia tamko hili tunaiomba Serikali ishughulikie mambo yafuatayo;
a. kumshugulikia mtuhumiwa huyu haraka ipasavyo ili iwe fundisho na kukomesha uharamia wa kazi za sanaa nchini
b. Kushughulikia haraka sheria mpya ya hakimiliki pamoja na sheria mpya ya TRA
c. Taasisi za Serikali zinazoshughulikia masuala ya sekta ya sanaa na Wasanii nchini kuwajibika ipasavyo.
d. Kuwaonya MACHINGA wote wanaotembeza DVD/VCD ambazo si halali waaache mara moja, pia Uonyeshaji wa Filamu kwa njia ya waya (Cable operators).
e. Vibanda umiza yaani wanaonyesha mitaani bila idhini ya wamiliki waache mara moja.
f. Kuwaonya watu wanaojishughulisha na uchomaji wa kazi za filamu, muziki kwa kutumia Kompyuta.
g. Tunawaonya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kama Anga, majini na nchi kavu kama Mabasi yanayoenda Mikoani kuacha mara moja kuonyesha filamu hizo bila idhini ya wamiliki.
Niwahakikishie kwamba kuanzia leo na kuendelea yeyote ambaye atafanya hujuma katika kazi za Wasanii tutapambana
naye hata kama hujuma hiyo itafanywa kwa DVD/VCD/CD mbili za kazi yoyote ya Sanaa.
.
Mohamed Mtunis, Muhsein Awadh Msama
Mtunis akiongea na wanahabari hapo pichani kuhusu wizi wa filamu katika Hoteli ya De Mag iliyopo Mwananyamala.
Ndugu Waandishi wa habari tunatambua mpango wa serikali wa kuleta mabadiliko katika sekta ya filamu na muziki nchini lakini bila ya kufanyika jitihada za makusudi kudhibiti maharamia hawa urasimishaji unaotarajiwa kufanywa na Serikali hautakuwa na maana kwa sababu maharamia ni watu wenye mbinu katika kufanya wizi wao.
Lakini pia tunapenda kuwajulisha kwamba kutokana na kukithiri kwa matukio ya wizi wa kazi za sanaa nchini; Wasanii, Wadau wa filamu, Kampuni za Uzalishaji, Kampuni za Usambazaji wa Filamu, Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Shirikiksho la Muziki nchiniwameomba kufanyike kwa matembezi ya kulaani wizi huo ambao umeshamiri zaidi ya miaka ishirini sasa ili kuonesha hisia za wizi huo, jamii pamoja na serikali itambue kuwa TUMECHOSHWA NA WIZI UNAOJULIKANA
Mwisho nawashukuru kwa ushirikiano wenu nanyi tunaomba kushiriki kikamilifu katika kusaidia Wasanii Tanzania.

PAMOJA TUIKUZE NA KUISIMAMIA TASNIA YA FILAMU NCHINI.
AHSANTENI.
SIMON J. MWAKIFWAMBA
RAIS SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA.

VIA: http://filamucentral.co.tz
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.