Tuesday, August 7, 2012

HII NDIO VIDEO YA KWANZA YA DOGO JANJA TOKA AONDOKE TIPTOP, SOMA PIA ALICHOSEMA KUHUSU KUKUTANA NA MADEE.Dogo Janja.

Dogo Janja amedrop single yake ya kwanza ‘Yamoyoni’ toka aondoke kwenye kundi la Tiptop Connection akiwa chini ya usimamizi wa Madee June 13 2012.

Hii single ya Dogo Janja amezungumzia maisha yake na anasisitiza kwamba “mimi sina hila na wala sina kisasi, ni single ya kutoa tu yale ya moyoni na ni ukweli nimewazungumzia TipTop lakini sijawazungumzia vibaya”

Janja amesema “toka nimetoka Tip Top kuna mtu mmoja tu ambae naongea nae vizuri hata nikimpigia simu yangu hana makuu ambae ni Tunda Man, Madee hajawahi kunipigia simu lakini nitaendelea kumuheshimu kama baba yangu kwenye music kwa sababu ndio amenifanya mpaka leo nafanya hii interview, thanx sana bro umenipa uwezo mkubwa sana kwenye muziki umenifungua upeo, najua kuandika vizuri nyimbo mwenyewe”

Pamoja na kwamba Janja wakati anaondoka TIP TOP  aliwahi kusema hatotaka tena kumuona Madee, leo amesema mpaka sasa hajawahi kuonana na Madee uso kwa uso ila anatamani sana kuonana nae.

Kuhusu kauli yake ya kutotaka kuonana na Madee tena amesema “zile zilikua hasira mwanzoni na pia nilikua nafikiria vitu vingi sana, nilikua napakwa matope Watanzania walikua hawajanielewa, walikua wanajua kweli mimi nimekataa shule lakini yale matope ambayo nilikua napakwa Ostaz Juma kanimwagia maji ya kitanashati nikawa msafi, sio kwamba nina shida ya kuonana na Madee ila nikionana nae nitamsalimia wala mimi sina tatizo nae, tutapiga story tu hata za kimaisha kushauriana hapa na pale”


VIA: http://millardayo.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment