Friday, October 11, 2013

WATANZANIA WAMEASWA KUTOJIINGIZA KATIKA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA MCHAKATO WA KUTAFUTA KATIBA MPYA


Watanzania wameaswa kutojiingiza katika itikadi za vyama wala kufungamana na kundi lolote katika mchakato wa kutafuta katiba mpya ili kuwezesha kupatikana kwa Katiba bora yenye manufaa kwa wananchi wote bila kujali hali zao, dini wala dhehebu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere JOSEPH BUTIKU amesema wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba za Mwalimu Nyerere kwa njia ya simu kuwa suala la katiba ni muhimu na kuonya kutoingizwa kwa siasa katika mchakato wake jambo ambalo linaweza kusababisha kutopatikana Katiba yenye matakwa ya wananchi.
BUTIKU amesema kupitia mitandao ya simu kwa kushirikiana na Taasisi ya simu ya PUSH MOBILE wananchi wataweza kupata hotuba za Mwalimu NYERERE zitakazowaelimisha kuhusu masuala mbalimbali.
Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Mwalimu NYERERE amesema Baba wa Taifa aliiachia Tanzania urithi mkubwa wa ujumbe tofauti kupitia hotuba zake na machapisho mbalimbali ingawa imekuwa ni vigumu kwa watanzania kufuata maneno yake kwa vitendo.
Oktoba 14 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE ambapo kwa mwaka huu maadhimisho yatafanyika siku nne zijazo.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment