Sunday, October 13, 2013

MWANDISHI UFOO SARO WA ITV AJERUHIWA VIBAYA KWA RISAASI MAMAYAKE MZAZI AFARIKI


Mwandishi wa habari wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, katika moja ya matukio ya kikazi hapa nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amedaiwa kupigwa risasi ya tumbo na kupelekea kumjeruhi vibaya,  huku mama yake mzazi naye akifariki baada ya kupigwa risasi katika tukio hilo.
 
Habari za awali zinasema kuwa mwandishi huyo pamoja na mama yake wamefanyiwa kitendo hicho na kijana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Ufoo Saro, ambaye inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo eneo la Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia risasi na kisha nayeye kujiua kwa risasi. 

Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilofanyiwa mwanadada huyo anayefanya kazi katika kituo cha ITV na Radio One, kinachomilikiwa na Kampuni ya IPP, chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi.
 
CHANZO: FATHER KIDEVU BLOG
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment