Thursday, October 10, 2013

TFDA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA AINA 273 YA DAWA MBALIMBALI ZISIZOFAA KWA MANUFAA YA BINADAMU


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamefanikiwa kukamata aina 273 ya Dawa mbalimbali zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 49 kutoka katika Mikoa tisa nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishina wa Polisi (DCI), ROBERT MANUMBA wakati akitolea ufafanuzi kuhusiana na Operesheni ya kukamata Wananchi wote wanaojihusisha na Bishara ya Dawa bandia, Dawa zisizosajiliwa, Dawa duni pamoja na zile zilizoisha muda wa matumizi.
Kamishina huyo wa Polisi amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa kutokana na matokeo ya Operesheni hiyo ambapo hadi sasa jumla ya Majalada 42 ya kesi tayari yamefunguliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi dhidi ya Watuhumiwa kutoka katika Mikoa hiyo 9 ambayo imehusishwa katika Operesheni.
Operesheni hiyo ambayo imefanyika kati ya Oktoba 01 hadi 03 mwaka huu katika maeneo 138 ilihusisha Mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Dodoma,Kilimanjaro, Mara Geita pamoja na shinyanga.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment