Sunday, December 23, 2012

MAELFU WAJITOKEZA KWA WINGI KUPOKEA MBUNGE WA ARUSHA GOBLESS LEMA


 
 
Na Mroki Mroki, Arusha 
MAPOKEZI ya Kihistoria katika jiji la Arusha yamefanyika leo wakati wafuasi,  Mbunge wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema walipo miminika kwa Wingi kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja vya Kilombero mjini hapa alipohutumia maelfu ya wana CHADEMA Arusha Mjini. 

Mapokezi yahoo yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa akirejea mjini Arusha akitokea jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani ya Keshi yake ya Kuvuliwa Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrejeshea Ubunge wake Desemba 21,2012.

Maelfu ya wananchi wakiwa katika msafara mrefu zaidi ya pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege KIA mara baada ya Mbunge huyo kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20 Asubuhi.

Aidha Maandamano hayo ya Mapokezi ya Mbunge huyo, hayakuwa na hata chembe ya Askari Polisi waliovalia sare wala magari yao ya diria kama ilivyozoeleka na kuyafanya yafanyike kwa amani na utulivu katika maeneo yote yaliyopita.

Huku wakiimba nyimbo za furaha hasa zile za “Oya oya Jembe letu limerudi” Wanachadema hao walijigawa na baadhi kulinda amani huku wengine wakiongoza magari.

Father Kidevu Blog ilishuhudua maelfu ya wakazi wa mji wa Arusha wakiwa katika hali ya furaha na kusimama kando ya barabara kushuhudia mapokezi ya Mbunge huyo.

“Haijawahji tokea hapa Arusha, kuwapo kwa msafara mrefu namna hii wa mapokezi ya kiongozi yeyote Yule, tena yakiwa na amani ya kiasi hiki,” alisikika akisema mmoja wa Watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Licha ya Kufanya mapokezi hayo na Kumshukuru Mungu kwa Mbunge wao kurejea madarakani, lakini Wakazi wa Arusha na Wapigakura wa Godbless Lema wamesema hivi sasa Mbunge huyo anapaswa kutulia na kutumia kipindi kilicho baki cha miaka miwili ya madaraka yake kuwatumikia wananchi katika kuhakikisha miradi ya Maendeleo inafanyika Jimboni humo na kuachana kabisa na migomo na maandamano ya kila mara.

“Sasa Lema anatakiwa kututumikia wananchi maana sisi tumesha mtumikia yeye vya kutosha kwa kuwa nae bega kwa bega katika kipindi chote cha uongozi na hata alipokumbwa na msukosuko wa kuondolewa Ubunge, hivyo sasa ni wakati muafaka wa yeye kuwaletea maendelea wana Arusha Mjini,” alisema Meshack Siriwa.

Godbless Lema  alivuliwa Ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, 2012
mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha  yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.

 Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kuanza kuanguaka.
 Furaha hiyo ilikuwa kwa kilu aliye Mwanachadema
 Skafu na vitru mbalimbali vilivyo na alama ya CHadema viliuzwa jijini Arusha kwa wingi.
 Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
 Lema Arusha anafananishwa na Barack Obama

 Watu walining'inia katika magari bila hofu

 Huyu na e'eti' alikua anachukua kumbukumbu za Video....
Lena akiwa nba Mbunge wa Arumeru Mashuari CHADEMA, Joshua Nasari.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment