Saturday, July 7, 2012
TANZANIA NA MSIMAMO WAKE JUU YA NDOA ZA JINSI MOJA
Tanzania stands firm on aid-gay rights spat with UK
By Fumbuka Ng'wanakilala | Reuters – Fri, Nov 4, 2011
DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzania has become the latest African government to say it will not legalise homosexuality even if that means it loses substantial financial aid from Britain.
Government officials reacted strongly to Prime Minister David Cameron's threat to cut aid to countries that deny gay rights.
"Tanzania will never accept Cameron's proposal because we have our own moral values. Homosexuality is not part of our culture and we will never legalise it," foreign affairs minister Bernard Membe was quoted as saying by Tanzania's Guardian newspaper.
"We are not ready to allow any rich nation to give us aid based on unacceptable conditions simply because we are poor. If we are denied aid by one country, it will not affect the economic status of this nation and we can do without UK aid."
Tanzania, a former British colony and one of Africa's biggest per capita aid recipients, received $453 million (282 million pounds) of aid for its 2011/12 budget, with Britain the largest provider of general budget support.
Ghana's President John Atta Mills said Wednesday his government would never legalise homosexuality. Uganda has also reacted strongly to Cameron's comments.
The Department for International Development (DFID) gave Tanzania 144 million pounds in aid in 2009/10 and has pledged to spend an average of 161 million pounds per year in Tanzania until 2015.
Homosexuality is a serious criminal offence in Tanzania, punishable by imprisonment, but no one has been prosecuted.
"We cannot be directed by the United Kingdom to do things that are against our set laws, culture and regulations," Membe was quoted as saying.
Zanzibar President Ali Mohamed Shein also rejected the British demands for gay rights to be respected in Tanzania.
"We have strong Islamic and Zanzibari culture that abhors gay and lesbian activities, and to anyone who tells us that development support is linked to accepting this we are saying no," Shein told journalists Thursday.
Zanzibar, Tanzania's semi-autonomous archipelago, enacted a law in 2004 banning homosexual relations. Male offenders face more jail time, up to 25 years, than convicted women.
Homosexuality is illegal in 37 African countries, and rights groups say gays are often the targets of violent hate campaigns.

SASA UNAWEZA KUTOA MAONI YAKO KUHUSU KATIBA KUPITIA UKURASA WA FACEBOOK WA TUME.
Sasa tunaweza kuwasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya, kupitia Facebook
(bofya hapa), kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa akaunti ya
iliyoanzishwa kwa jina Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania https://www.facebook.com/pages/Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Tanzania/323414977745643
Watu wenye silaha wemeishambulia helikopta iliyokuwa ikibeba vifaa vya uchaguzi vitakavyotumika kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa Jumamosi nchini Libya, maafisa wa nchi hiyo wamesema.
wapiganaji wa nchini Libya
Helikopta hiyo ililazimishwa kutua nje ya mji wa mashariki wa Benghazi. Taarifa ambazo hazijathitishwa zinasema mtu mmoja amefariki.
Utambulisho wa washambuliaji bado haujajulikana, lakini eneo la mashariki mwa Libya limekosa utulivu kutokana na makundi yanayotafuta uhuru wa kanda hiyo.
Uchaguzi wa wabunge ni za kwanza nchini humo baada Marehemu Muammar Gaddafi kupinduliwa mwaka jana.
Habari hizi zinakuja wakati watu wenye silaha wamefunga vituo vitatu vya kuuza nje mafuta kupinga uchaguzi huo.
Watu hao wamekasirishwa kwamba eneo la magharibi ya nchi limepewa viti 200 zaidi katika Bunge jipya ikilingalishwa na eneo la mashariki lenye utajiri wa mafuta.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, nusu ya vituo vya Libya vya kuuza nje mafuta vimefungwa kutokana na hali hiyo.
"Helikopta iliyobeba masanduku ya kura iliruka juu eneo la Hawari Kusini mwa Benghazi ambapo alipigwa kwa kuwa kutumia silaha ndogo," AFP limenukuu shirika la habari Kanali Ali al-Sheikhi likisema.
Alisema mtu mmoja aliuawa, lakini shirika la habari la Reuters linamnukuu rasmi akisema kuwa mtu mmoja aliyekuwa ndani ya helkopta alijeruhiwa wakati helikopta alipopigwa kombora la kutungulia ndege.
RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA MAHAKAMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Ignus Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama (Chief Registrar) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012. Kabla ya kuteuliwa kushika wadhfa huo mpya, Bwana Kitusi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
Katika uteuzi huo, vilevile Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi, Bwana Panterine Muliisa Kente kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani (Registrar of the Court of Appeal) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.
Aidha, Mhe. Rais amemteua Bwana Benedict Bartholomew Mwingwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu (Registrar of the High Court) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mwingwa alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Julai, 2012
Friday, July 6, 2012
FACEBOOK MTANDAO WA KIJAMII KUFUNGWA TAREHE 15/7/2012
Najua
kwamba taarifa hii inaweza kumshtua kila mtu ambaye amekuwa memba wa
mtandao huu kwa kipindi kirefu ila kwa hapa hakuna budi kukubaliana na
huyu mtu ambaye aliuleta mtandao huu kwenye internet na sisi kujoin.
Nilikuwa naipitia habari hii huku picha ya Mark Zurkerberg ikiwa
pembeni akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari nje ya ofisi yake
na kusema "Mtandao huu umekuwa ukinisumbua sana maishani mwangu kwa
kuwa kuna wengi wamekuwa wakilalamika kila siku. Tuliweka kikao kizito
na kuamua kwamba ni lazima tuufunge mtandao huu wa Facebook kwa sasa.
Kilikuwa ni kikao kigumu na kizito na hata kuufikia uamuzi huo lilikuwa
ni jambo zito, ila kwa sasa hatuna jinsi. Ni lazima tuuzime ifikapo
tarehe 15/7/2012" Mark alisema na kuendelea.
Najua wengi wanaweza
wasiwe na furaha, ila ningependa kuwaambia watu kwamba kwa sasa
inawapasa kuchukua kila picha ambazo wanazo kwenye facebook kwa sababu
baada ya tarehe hiyo hawataweza kuziona tena. Ni wakati sasa wa watu
kuwasiliana, kukutana na kutengeneza urafiki wa kweli" Mark alisema
mbele ya waandishi wa habari.
MTAKATIFU THOM AELEZEA MIKAKATI YANGA, AANZA KAZI MARA MOJA
hom Saintfiet akiongoza mazoezi ya Yanga, Uwanja wa Kaunda jioni hii.
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA mpya wa Yanga, Thom Saintfiet amesema kwamba sera yake
ni ushindi na mataji na hahofii mpinzani yeyote katika soka ya Tanzania, ikiwemo
watani wao wa jadi, Simba SC.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari jioni ya leo,
makao makuu ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam,
Saintfiet alisema kwamba yeye ni muumini wa ushindi na mataji, hivyo anachotaka
ni ushindi tu.
“Nikishinda 5-0 ni vizuri, lakini hata nikishinda 1-0 si mbaya,
mimi ni mshindi na ndio maana nimekuja hapa kushinda,”alisema.
Thom alisema kwamba akili yake hapo kwa Simba tu, bali wapinzani
wote katika Ligi Kuu na akasema anataka kurejesha ubingwa wa Ligi Kuu, ambao
msimu uliopita klabu hiyo ilipokonywa na watani wao hao wa jadi.
“Upinzani ni mkubwa, nasikitika mwaka jana timu imepoteza
ubingwa wa Ligi Kuu, lakini si mbaya, si lazima timu bora kila mwaka iwe na
taji. Hata Barcelona ni timu nzuri, lakini haikuchukua ubingwa wa Ligi ya
Mabingwa wala La Liga.
Timu (Yanga) ilibeba nafasi ya tatu msimu uliopita, siyo
nzuri sana. Nataka nishirikiane na wenzangu kurejesha heshima,”alisema.
Saintfiet alisema kwamba ameona wachezaji ni wazuri na
anamuamini kocha anayemkuta Freddy Felix Minziro ni mzuri na amefanya kazi
nzuri. “Timu ilicheza mechi na Express wiki iliyopita, nimeambiwa ilicheza soka
nzuri na kushinda, naamini naikuta timu ikiwa vizuri,”alisema.
Mbelgiji huyo alisema kwamba ana wiki moja kabla ya kuanza
kwa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na hana wasiwasi atafanya
vizuri kwa sababu timu ina wachezaji wazuri na Minziro alianza kuwaandaa mapema.
Saintfiet alikataa kuzungumzia falsafa yake akisema hataki
wapinzani wake wajue siri zake, ila akasistiza sera yake ni ushindi na kubeba mataji.
Tom Saintfiet alizaliwa Machi 29, mwaka 1973 mjini Mol, Ubelgiji
na kabla ya kuwa kocha alicheza soka katika nafasi ya kiungo kuanzia mwaka 1983
hadi 1997 alipostaafu na kuwa kocha akiwa ana umri wa miaka 24, akiweka rekodi
ya kocha kijana zaidi kuwahi kutokea katika soka ya Ubelgiji.
Saintfiet amefundisha nchi kadhaa kuanzia kwao Ubelgiji,
Qatar, Ujerumani, Visiwa vya Faroe, Finland na Uholanzi.
Pia ana uzoefu wa kutosha wa kufundisha soka Afrika akiwa
amefundisha Namibia na Zimbabwe kama kocha Mkuu wa timu za taifa za nchi hizo.
Anasema kabla hajakwenda Namibia, Saintfiet alikuwa kocha wa
klabu ya Ligi Kuu Finland, iitwayo RoPS Rovaniemi na mwaka 2002, alikwenda
kuifundisha B71 Visiwa vya Faroe ambayo aliiwezesha kushika nafasi ya pili
katika Ligi Daraja la kwanza. Anasema kutoka hapo, akaenda kuwa kocha wa Al-Ittihad
Sports Club ya Qatar (sasa inaitwa Al-Gharafa SC) ambako alidumu hadi mwaka 2004
alipochukuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17
ya Qatar.
Saintfiet ana leseni Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) ya
kufundisha soka ya kulipwa popote barani humo, ambayo aliipata mwaka 2000.
Kati ya mwaka 2006 na 2007 alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa FC
Emmen ya Daraja la Kwanza Uholanzi na pia amewahi kufanya kazi kama Mshauri wa
Ufundi wa Shirikisho la Soka la Kazakhstan.
Amewahi kuwa
Mchambuzi wa soka katika Televisheni katika nchi za Ubelgiji, Afrika Kusini na
Namibia na alifanya kazi kama mkalimani DFB. Amesomea Saikolojia ya Michezo na
Uchumi.
Anazungumza lugha kibao na kwa ufasaha zaidi ni Kiholanzi, Kiingereza,
Kifaransa, Kijerumani, Kifaroe na ‘ana jua jua’ Kiarabu, Kiafrikana na Kispanyola
na sasa tayari ameanza kujifunza Kiswahili.
Baada ya kumaliza kusaini mkataba majira ya 9:47 jioni,
Saintfiet aliyewasili jana mchana nchini, aliteremka Uwanja wa Kaunda kuanza kufundisha
timu. Kwanza alianza kuzungumza na wachezaji kuwaelezea falsafa zake na kisha akaanza
kazi.
Picha zote na Mahmoud Zubeiry
TFF LEO.16 BORA COPA COCA COLA YAANZA KESHO
HATUA ya 16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inaanza
kesho (Julai 7 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazokutanisha timu nane kati ya 16
zilizofuzu hatua hiyo. Mechi hizo za 16 bora zitachezwa kwenye viwanja vya
Kumbukumbu ya Karume na Tanganyika Packers vya Dar es Salaam.
Ruvuma iliyoongoza kundi A itacheza na Temeke iliyoshika
nafasi ya tatu kundi C. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Karume.
Mechi nyingine ya asubuhi itakayochezwa Tanganyika Packers itawakutanisha
washindi wa pili kundi A Kigoma dhidi ya Mara walioshika nafasi ya nne kundi C.
Mechi za jioni kwa kesho zitakazoanza saa 10 kamili jioni
zitakuwa kati ya Mjini Magharibi na Kagera kwenye Uwanja wa Karume wakati
Morogoro na Pwani zitaumana kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe,
Dar es Salaam.
Hatua ya 16 bora itakamilika keshokutwa (Julai 8 mwaka huu)
kwa mechi za asubuhi kati ya Kinondoni na Rukwa kwenye Uwanja wa Karume, na
Dodoma dhidi ya Arusha kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers. Mechi za jioni siku
hiyo ni kati ya Kilimanjaro na Mwanza (Uwanja wa Karume) na Tabora na Tanga
(Tanganyika Packers).
Timu zitakazoshinda zitaingia hatua ya robo fainali
itakayochezwa Julai 10 na 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Nusu fainali itachezwa Julai 13 mwaka huu, na kufuatiwa na mechi ya mshindi wa
watatu na fainali ambazo zote zitachezwa Julai 15 mwaka huu.
Kifaa cha kupima ukimwi sokoni
Kifaa hicho kwa jina OraQuick kitawezesha watu kutumia mate kuchunguza kama wana virusi vya ukimwi.
Itachukua muda wa kati ya dakika 20 na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi huo.
Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu kuchunguza hali yake mwenyewe nyumbani au kokote anakotaka kitaanza kuuzwa nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka huu.
Serikali ya Marekani inatarajia kuwa kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia miongoni mwa watu wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya Wamarekani wako katika kitengo hicho.
Utafiti wa kimatibabu unaoyesha kuwa majaribio ya matokeo ya uchunguzi wa kifaa hicho cha Oraquick yananaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na mbili, miongoni mwa watu wanoishi na virusi vya ukimwi.
Wednesday, June 27, 2012
Tuesday, June 26, 2012
WAHAMIAJI 42 RAIA WA EPHIOPIA WAFARIKI DODOMA
Kamanda Zelothe Stephen
WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu. Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi. Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana. Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wake wapo katika hali mbaya. Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku wahamaji watano wanaendelea kupata matibabu katika Zahanati ya kijiji cha Chitego ambapo wengine waliobaki wamehifadhiwa katika kanisa la Anglikan wakipatiwa huduma mbalimbali. Huduma hizo mbalimbali ni pamoja na kupewa maji , uji na matibabu. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuhaidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Tuesday, June 12, 2012
MAHAKAMA YASOGEZA KESI YA LULU HADI TAREHE 25 JUNI, 2012.
Lulu’ akishuka katika basi la magereza.
‘Lulu’ akiwa ndani ya mahakama.
‘Lulu akiteta jambo na wakili wake muda mfupi baada ya kufika mahakamani.
Akitoka mahakamani baada ya kesi yake kusogezwa hadi tarehe 25 mwezi huu, ambapo watetezi wa ‘Lulu’ wametakiwa kuwasilisha vielelezo vyenye uthibitisho wa umri wake ifikapo tarehe 13 mwezi huu, wakati upande wa serikali wameomba kuwasilisha vielelezo vyao tarehe 22 mwezi huu ili kumaliza tatizo la utata kuhusu umri wa mtuhumiwa huyo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika eneo lote nda na nje ya mahakama kuu wakati wa kesi hiyo.
HABARI TOKA http://dewjiblog.com
Monday, June 11, 2012
KENYA WATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO YA SAITOTI
Kenya imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi.
Mabaki ya ajali hiyo.
Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio hilo.
Idara ya polisi imesema uchunguzi utafanywa kujua sababu ya ajali hiyo, na balozi wa Marekani mjini Nairobi, amesema Marekani iko tayari kusaidia kwenye uchunguzi huo, ikiwa itatakiwa kufanya hivyo.
Msemaji wa polisi alieleza kwamba inavoelekea kuanguka kwa helikopta hiyo lilikuwa tukio la ajali.
Raia wa Kenya walikuwa na masikitiko Jumapili, baada ya taarifa ya ajali hiyo kujulikana, na watu wamekuwa wakizuru nyumba ya kuhifadhi maiti mjini Nairobi kutoa heshima zao.
Makamo wa rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea:"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi"
Rambi-rambi zimekuwa zikimiminika nchini Kenya, pamoja na za Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alipatanisha baada ya ghasia za uchaguzi uliopita nchini kenya.
Profesa Saitoti alikuwa akizungumza kwa ukali dhidi ya al-Shabaab na inaaminiwa alihusika na uamuzi wa jeshi la Kenya kuingia Somalia mwaka jana.
Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Alikuwa na umri wa mika 67.

Friday, June 8, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI FURSA YA WASANII WA TANZANIA KUSHINDA EURO 5,000 KATIKA SHINDANO LA KUTUNGA WIMBO RASMI WA KUNDI LA MATAIFA YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP GROUP OF STATES)
Monday, June 4, 2012
Habari kwa Kiswahili: FBI Kuzima Kompyuta 350,000 Zilizoambukizwa na Virusi.
Mmoja kati ya watengeneza virusi aliyewekwa chini ya ulinzi na watu wa usalama FBI kutokana uhalifu wake.
Hivi sasa FBI iko katika maandalizi ya kuzima kompyuta 350,000 duniani kote kutokana kuambukizwa na kirusi aina ya Trojan aliyetengenezwa na kundi la Kiestoni ambalo ni la wahalifu.
Pia FBI wamefanikiwa kukamata kifaa aina DNS changer ambacho hutumika kutengenezea Vurusi hao.
Walinzi wa kimarekani ambao wanashughulika na uhalifu huo wanafahamu kompyuta na Macs zote zilizoambukizwa na hicho kirusi aina ya Trojan , hivyo basi hitimisho la wamiliki endapo watachukua hatua ya kutatua tatizo, njia ni moja ya kuviondoa vifaa hivyo katika mtandao (Internet).
Kifaa hicho cha kutengeneza virusi DNS changer, kilitengeneza na kuachia virusi hao kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2007. Kiliweza kuhasiri watumiaji, kwani kompyuta ilitenda kazi kinyume na inavyoweza. Na tatizo kubwa kwa watumiaji ilikuwa kompyuta kufanya kazi kwa taratibu sana katika mtandao. Pia virusi hivyo viliweza kulemaza antivirus programu na maelekezo ya kompyuta kuwa ya udanganyifu.
Virusi hivyo viliachiwa na kundi la wahalifu wa Kiestoni na kuaminika kuwa, idadi ya virusi vilivyoachiwa katika mtandao ni dola milioni 16.
Baada ya kashfa hiyo kugundulika, FBI walizima kifaa hicho kilichotumiwa na wahalifu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (server) na mmoja wao kuchua nafasi hiyo, lakini Bureau alitaka kifaa hicho (server) kizimwe kabisa kwa sababu kinagharamia makumi ya maelfu ya dola kukiendesha.
Bureau iliweka kifaa maalumu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (Server) kwa maombi ya DNS kutoka kwa kompyuta zilizoambukizwa, kwani bila kifaa hicho (server) kompyuta hizo zilizoambukizwa zisingeweza kuunganishwa na mtandao.
Jinsi ya kuunganishwa na mtandao
Amri ya mahakama iliruhusu kifaa cha kotoa mawasiliano ya mtandao (Sever) cha FBI kupitisha anwani ya IP ya wale walioambukizwa na muda wake kumalizika Julai 9, wakati kompyuta hizo zitakapokuwa zimeondolewa katika mtandao (offline). hatua hiyo, kompyuta zote zilizoambukizwa na virusi aina ta Trojan hazitaweza kuunganishwa katika mtandao.
Kuepukana na kompyuta yako kuzimwa na mtandao wa kuhakiki kompyuta zilizoambukiza "DNS ya FBI. ambao unaruhusu kwa sasa watumiaji kuangalia kama wana virusi na kuviondoa mapema.
Kwani inasemekana kuwa tayari kuna baadhi ya kompyuta 150,000 zimesafishwa virusi hao. Lakini baadhi ya wakosoaji wanaonya hii, kuwa haitoshi hivyo ni bora kutangaza na uhamasishaji unahitajika.
Ni lazima kuelewa kwamba kirusi aina ya Trojan kimeambatana na kirusi aina ya root kit ambacho ni kigumu kukiondoa katika kompyuta, hivyo kusababisha mtumiaji kufuta mpangilio na kuhifadhi upya.
Hata hivyo makampuni ya usalama wa mipangilio ya kompyuta ambayo ni Norton, Kaspersky, Trend Micro, Microsoft, McAfee na wengine, husaidia kukiondoa kirusi aina rootkit bila kufuta mipangilio ya kompyuta yako.
Kifaa hicho cha kutengeza virusi DNS Changer kimekuwa katika habari tangu Novemba 8, 2011, wakati botnet kubwa ya kusambaza virusi chini ya jina la kampuni ya Rove Digital, iliwekwa chini ya ulinzi na muungano wa msako ambao ni FBI pamoja na kundi la Kiestoni wahalifu. Na kutokea kukamatwa kwa wanaume sita.
HABARI TOKA http://cheraboy.blogspot.com

Sunday, June 3, 2012
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU (DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA) ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA BANK WILAYANI MAGU KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU
DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA
KUZALIWA
Marehemu alizaliwa mnamo mwaka 1960 akiwa ni Mtoto wa Saba katika familia ya Mzee Lufega Masalu, Alizaliwa katika Kitongoji cha Benki eneo ambalo kwa sasa Cadirac Hotel. Katika Wilaya ya magu na Ndani ya Mkoa wa Mwanza.
ELIMU
Daud Kilungumika Lufega alipata Elimu yake ya msingi Katika Shule ya Msingi Nyalikungu mwaka 1972 na kuhitimu darasa la saba mwaka 1978.
1980 Alijiunga na Chuo cha Kilimo na Mifugo Ukiligulu Mwanza na kutunukiwa cheti cha Afisa Usimamizi Kilimo na Mifugo.
UBATIZO:
Daudi Kilungumika Lufega alikuwa ni Muumini wa Kanisa katoliki.
Mwaka 1993 alibatizwa katika Parokia ya Magu.
Mwaka 1993 alipata kipaimara katika Parokia ya Magu.
NDOA
Mwaka 1985 alimwoa Bi. Fausta Mayengela.
KAZI/SHUGHULI
Mwaka 1981 -1984 Afisa Mazao wa Mamlaka ya Pamba –Tanzania Kanda ya Manawa Ginnery.
1984-1994- Afisa Ukusanyaji mapato(Revenue Collector) HALMASHAURI YA Wilaya ya Magu.
UONGOZI NA UZOEFU:
Mwaka 1999-2009 Balozi wa nyumba kumi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Benki. Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mwaka 2009-2012 Mwenyekiti wa Mtaa wa Benki katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Magu Mjini Kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi –CUF.
Mwaka 2010-2012 Kada wa Chama na Mjumbe wa kamati ya Utendaji Wilaya –CUF.
UGONJWA na MAUTI
Daudi Kilungumika Lufega alianza kuugua Mwezi Marchi 2012 akisumbuliwa na matatizo ya Inni na Figo, Alibahatika kupata Matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Magu pia alifakiwa kupata matibabu ya Tiba mbadala
1. Lakini kwa vile Andiko linasema “Kila nafsi itaonja mauti”
2. Na Kwa kuwa Mauti ni kitanda ambacho kila Mwanadamu atakilalia.
3. Mauti ni Mlango ambao kila Mwanadamu atauingia.
4. Mauti ni vazi ambalo kila Mwanadamu atalivaa.
Na Tarehe 31-05-2012 Majira ya saa 12:30 asubuhi Daudi Kilungumika Lufega alifariki Dunia.
Marehemu ameacha
1. Mjane
2. Watoto 9 wakiume 4 na Wakike (5)Watano, na
3. Wajukuu 4
SHUKRANI:
Familia ya Marehemu inatoa Shukrani zake za dhati kwa Waganga na Wauguzi wote wa Hospital ya Wilaya ya Magu kwa juhudi zao kumhudumia Marehemu kipindi alipokuwa amelazwa Hospitalini hapo. Wataalam wa Tiba mbadala kwa Jitihada zao zote za Kutaka kuokoa Maisha yake japo haikuwezekana.
Shukrani kwa Majirani, Ndugu, Jamaa, Marafiki, Vyama vya Siasa, Mamlaka ya Mji Mdogo Magu Mjini na wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika hali na Mali kufanikisha Mazishi na Maziko ya marehemu Mpendwa wetu.
Marehemu alikuwa Mtu wa Watu, Mcheshi, Mtu huru na mtu mwenye maamuzi ya kweli.
BWANA AMETOA,
BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE,
AMINA.
Subscribe to:
Posts (Atom)

Tanzanian Shilling Converter