Sunday, November 2, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA:-BOMU LALIPUKA NA KUUA MTU UKO SHINYANGA

KUNA TUKIO LA MLIPUKO WA KITU KINACHODHAWINA NI BOMU NDANI YA GARI NA KUSABABISHA KIFO/MAJERUHI. Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45hrs katika center ya Muhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu. 


 Gari no T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) msukuma wa Muhunze.


Wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mwangaza wa Ngara ambaye ni familia ya mwenye gari.(Pichani) 

Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.


Pia mfanyabiashara Donard s/o Nzugala Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Wengine ni Maganga s/o Piusi (14 ), msukuma,mkulima wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto,mgongoni na mkono wa kushoto
 Seni s/o Edward (25 ), msukuma mkulima wa Lubaga Kishapu amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment