Thursday, November 6, 2014

VYAMA VYA SIASA VYAUNGANA KUPAMBANA NA UKAWA, CCM


Vyama vya siasa ambavyo havina uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimetangaza kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi ujao.Wakati vyama vya upinzani vikiwa na umoja wao maarufu kama UKAWA na kutangaza kuungana, vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimetangaza kuungana na kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lengo likiwa kupambana na UKAWA na Chama Cha Mapinduzi.

Akitangaza jijini Dar es Salaam uamuzi wa kuungana katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakilishi wa vyama Sita visivyokuwa na uwakilishi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha UPDP Bw. Fahmi Dovutwa amesema kuwa wameamua kuungana ili kupambana na UKAWA na CCM ambapo vyama vinavyounda umoja huo ni UMD, SAU, UPDP, AFP, Jahazi Asilia na Demokrasia Makini.

Mmoja wa viongozi wa wanaounda vyama Sita vinavyounda vyama hivyo ambaye ni wenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Bw. Rashid Rai amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa maendeleo hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment