Tuesday, November 27, 2012

MSIKILIZE KAMANDA WA POLISI WA TANGA AKIONGEA KUHUSU KIFO CHA MSANII SHARO MILIONEA


Kuhusu kifo cha msanii /mwigizaji Sharo
Milionea , namkariri Kamanda wa Polisi
Tanga akisema “ leo majira ya saa mbili
usiku kwenye barabara ya Segera Muheza
mtu mmoja alietambulika kwa jina la
Hussein Ramadhani au Sharo Milionea
akiwa anaendesha gari namba T 478 BVR
Toyota Harrier akitokea Dar es salaam
kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari
lake liliacha njia na kupinduka mara
kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili
wa marehemu umehifadhiwa kwenye
hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana
wala ubovu wa barabara kwenye sehemu
aliyopata ajali Sharo Milionea , katikati ya
Segera na Muheza ambapo gari
imehifadhiwa mahali salama kwa sababu
haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.

by G5 NEWS


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment