Monday, May 20, 2013

NISHA WA BONGO MOVIE AWATOSA WATOTO YATIMA....


MSANII wa maigizo, Salma Jabu ‘Nisha,’ amedaiwa kuwatosa watoto yatima waliokuwa wakimsubiri baada ya kuweka ahadi kuwa angekwenda kuwatembelea na kuwapa msaada. 


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Nisha aliahidi kwenda kuwapa msaada watoto yatima wa kituo cha Hisan Orphan Center kilichopo maeneo ya Mbagala Charambe, jijini Dar lakini ulipofika muda, hakutokea.
 


Rafiki wa karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alipoulizwa kulikoni alikiri kutotoa taarifa kwa uongozi wa kituo hicho cha watoto yatima na kudai walikuwa na dharura siku hiyo.

“Kuna tatizo lilitokea ikabidi tughairi. Tunaomba radhi kwa kuwafanya wasubiri sana ila niwaambie kuwa mpango wa Nisha kuwatembelea watoto yatima bado upo palepale,” alisema

Waraka wa John Mnyika kuhusu muswada wa Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2013


Waraka wa John Mnyika kuhusu muswada wa Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2013
Vijana wenzangu na wote wenye dhamira ya kuwezesha maendeleo ya vijana nchini, salaam!

Mtakumbuka kwamba mwezi Januari 2013 nilitoa taarifa kwa umma ya kueleza kuwa niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge Muswada Binafsi wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa na kuomba hatua za ziada toka ofisi ya Bunge kwa kuzingatia Kanuni ya 21 na Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge.


Toka wakati huo muswada huo mpaka sasa Mei 2013 haujachapwa katika gazeti la Serikali na nimepokea barua toka kwa ofisi ya Bunge kwamba wamepokea ushauri toka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa muswada huo hauwezi kuchapishwa katika gazeti la Serikali kwa kuwa umekiuka masharti ya ibara ya 99 ya Katiba ya Nchi.
 
Sababu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa ushauri huo ni kuwa muswada unalenga pamoja na mambo mengine kupitia kifungu cha 31 kipengele cha kwanza kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa madhumuni ya kugharamia shughuli za baraza la vijana la taifa, mipango ya baraza na kutekeleza miradi ya vijana kwa ajili ya maendeleo ya vijana.
 
Kwa maoni yangu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa ushauri huo bila kuzingatia kwamba kifungu cha 31 kipengele cha pili kinataja vyanzo mbalimbali vya fedha za mfuko ikiwemo kutaja kuwa fedha za mfuko zitatokana na fedha zilizotengwa na Serikali na Bunge kwa ajili ya Baraza kwa mujibu wa Ibara ya 135 kifungu cha pili cha katiba ya Nchi.

Ibara ya 135 (2) ya Katiba ya Nchi inatamka kuwa “fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na sheria ya kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe kwenye mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum”.
 
Hivyo, ni maoni yangu kuwa ibara hiyo ya Katiba ya Nchi inaweza kutumika kuwezesha kuanzishwa kwa Baraza la Vijana na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana bila kufungwa na Ibara ya 99 ya Katiba kifungu cha kwanza ambacho kimeweka masharti kuwa “Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Rais.”
 
Kifungu cha pili kinataja mambo yanayohusika na ibara hiyo ya 99 ni pamoja na muswada wa sheria kwa ajili ya “kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko mwingine wowote au kubadilisha kiwango hicho kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza”.
 
Toka Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 itamke kwamba Serikali itawezesha kuanzishwa kwa Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007; miaka takribani 17 imepita marais wote wa awamu husika na mawaziri wenye dhamana hawajawasilisha bungeni muswada huo hali ambayo imenifanya niandae muswada binafsi kuwezesha baraza kuundwa.
 
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa 2013 niliouwasilisha kwa maoni yangu hauna lengo la kuagiza malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko mkuu wa Hazina ya Serikali au Mfuko mwingine wowote kwa mujibu wa ibara ya 99 bali unalenga kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 135.
 
Hata hivyo, kwa kuwa muswada huu unahusu mustakabali wa vijana na ni suala la kitaifa kupitia waraka huu naomba kupata maoni yenu kuhusu suala hili, mapendekezo ya marekebisho yanayohitajika kufanyika na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
 
Maoni, mapendekezo na hatua hizo zitumwe kupitia mbungeubungo@gmail.com au kwa Afisa wa Ofisi ya Mbunge Ubungo Gaston Garubimbi (0715825025) kabla ya tarehe 24 Mei 2013. 
Nakala ya rasimu ya muswada wa Baraza la Vijana la Taifa wa mwaka 2013 inapatikana katika mtandao wa http://mnyika.blogspot.com kwa ajili ya rejea. 
 
Aidha, nawaalika kushiriki mikutano ya kupokea maoni kupitia mtandao huo tarehe 20 mpaka 23 Mei 2013 saa 9 alasiri mpaka 10 Jioni ambayo nitashiriki na kutoa maelezo ya zaidi kwa kadiri itakavyohitajika.
 
Natarajia kupokea maoni ya vijana na wananchi wengine bila kujali tofauti mbalimbali kwa kuwa madai ya kutaka kuundwe Baraza la Vijana la Taifa yamekuwa yakitolewa na vijana, asasi na taasisi kwa muda mrefu.
 
Vyama vya siasa kwa kuzingatia matakwa hayo viliahidi kutekeleza azma hiyo kwa mfano Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010-2015 kipengele 6.4.1 (viii) ilitamka “Kwa kuwa vijana ndio kundi kubwa hapa nchini, na kwa kuwa uhai wa muda mrefu wa taifa letu upo mikononi mwa vijana, Serikali ya CHADEMA itawezesha vijana kuunda Baraza la Vijana (BAVITA) ambalo limekwamishwa na Serikali ya CCM kwa muda mrefu”.
 
Kwa upande mwingine, Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 iliahidi katika kipengele 80 (k) “Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi ikiwa ni pamoja na kukamilisha uanzishaji wa Baraza la Vijana”.
 
Mwaka 2011 niliihoji Serikali bungeni ni lini itakamilisha uanzishwaji wa baraza hilo na ikaahidi kwamba kazi hiyo itakamilishwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 hata hivyo sasa ni Mei 2013 Serikali haijakamilisha.
 
Hivyo vijana, wabunge na wananchi kwa ujumla ni muhimu kuboresha muswada huo na uwasilishwe bungeni kuwezesha baraza la vijana na mfuko wa maendeleo vijana kuanzishwa; maslahi ya umma kwanza.
 
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb) 
19 Mei 2013 
Dodoma

Muswada wa Baraza la Vijana 2013-Rasimu ya Kwanza; pakua hapa (download here): 
https://docs.google.com/file/d/0B8xvLNf5FlohSHJPX2trR3p6YzQ/edit?usp=sharing


Profesa jay afunguka kuhusu sakata la JayDee na Clouds FM

 
WIKI hii kwenye Funguka na Risasi tunaye mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Haule, ‘Profesa Jay’ ambaye anafunguka juu ya bifu kati ya Judith Wambura ‘Jide’ na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.
Profesa Jay naye ametajwa katika sakata hilo kutokana na kushirikishwa katika wimbo wa Joto Hasira ambao wengi wameutafsiri kuwa na vijembe kwa Ruge.
Funguka: Mambo vipi Profesa, nimekutafuta ili nipate msimamo wako kwenye bifu kati ya msanii mwenzako (Jide) na Ruge.
Profesa Jay: Kwanza nianze kusema kuwa mimi sina upande wowote ambao ninaweza kuusimamia, sipo kwa Ruge wala kwa Jide.
Funguka: Kumekuwa na minong’ono mitaani kuwa upo upande wa Jide kwani mmekuwa mkifanya kazi pamoja vilevile ni marafiki kwa muda mrefu na ndiyo maana amekushirikisha kwenye wimbo wake wa Joto Hasira. Unalizungumziaje hili?
Profesa Jay: Ishu siyo mimi kuwa upande wa Jide au wa Ruge, kitu ambacho ninaweza kukizungumzia ni kwamba Jide alinishirikisha kwenye wimbo huo hata kabla ya hilo bifu lao sijalifahamu. Mimi niliimba kutokana na maudhui ya wimbo ulivyokuwa ukitaka. Kwa hiyo bado nasisitiza kuwa sifungamani na upande wowote katika jambo hili.
Funguka: Kama ni hivyo, unachukuliaje suala la Jide na Ruge kufikia hatua ya kuburuzana mahakamani?
Profesa Jay: Kuhusu hilo, sitakuwa msemaji sana ila kwa jinsi ninavyofahamu, Jide ni msanii mkongwe. Kama unakumbuka nilishawahi kufanya naye traki kadhaa kama Bongo Dar-es-salaam na Niamini. Kikubwa ni kwamba Jide anajiheshimu sana na nadhani kila anachokifanya anakijua vizuri.
Funguka: Unamuongeleaje Ruge na uongozi mzima wa Clouds kuhusu sakata hili?
Profesa Jay: Binafsi siwezi kuwaongelea Clouds au Ruge kwa jambo lolote, kwa sababu ninaamini na wao ni watu wazima na wanafahamu nini wanachokifanya.
Funguka: Hivi karibuni tumesikia wasanii kadhaa wamejitoa kwenye orodha ya wasanii watakaomsapoti Jide kwenye shoo yake ya Mei 31, vipi wewe utakamua kama kawaida?
Profesa Jay: Nikutoe wasiwasi, mimi binafsi nitakuwepo kwenye shoo ya Jide na nitapiga mzigo wa kufa mtu kumsapoti kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na moyo wangu wote.
Funguka: Poa, nashukuru kwa ushirikiano wako, kazi njema.
Profesa Jay: Haina kwere.

Breaking News:Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Anna Makinda,amelazimika kuliahirisha bunge kwa dharura

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Anna Makinda,amelazimika kuliahirisha bunge kwa dharura ili kutoa nafasi kwa Kamati ya kudumu ya maadili ya bunge kupitia hotuba ya makadirio ya wizara ya Habari,Vijana utamaduni na michezo,iliyokuwa inawasiliashwa na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani kwa wizara hiyo kwa maelezo kuwa hotuba hiyo ilikuwa imejaa uchochezi.

KWA MARA YA KWANZA LULU AMPAISHA BABA YAKE KWA NJIA HII, CHEKI HAPA

BABA LULU
As anavyojiita Hotlulumichael, kuna pande mbili zilishirikiana kumpata yeye na huo u-hottness wake..Nazungumzia upande F na upande M. So, kama wewe ni shabiki wa Hotlulumichael, basi utakuwa ushamuona mara nyingi aki-post picha kibao akiwa na mamaa(F) yake . Hatujahi kuskia ishu ya baba yake, labda mara moja tu kupitia gazeti la udaku. Lakini recently Hotlulumichael amerusha baba yake akiandika na caption kama inavyosomeka hapo juu. I hope ur glad to see the man na je?, Lulu is hot sawa…but she got it from her mama au papa??

Polisi Wakamatwa na Bangi Gunia 18 Wakisafirisha na Gari ya Mkuu wa Polisi

Siku chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.

Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.


Akithibitisha kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema askari hao walikuwa wakipeleka bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa mfanyabiashra mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake.


Kamanda Boaz aliwataja askari waliokamatwa na wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi katika mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734 Koplo Edward (dereva) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Arusha na G.2434 Konstebo George wa kituo cha polisi Ngarenanyuki Wilaya ya Arumeru.


Alibainisha kuwa kukamatwa kwa askari hao kunatokana na operesheni ya kukabiliana na dawa za kulevya inayofanywa na polisi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.


Alisema operesheni hiyo imefanyika kikamilifu katika Mkoa wa Arusha uliokuwa ukitumika kupitishia bidhaa hiyo, na sasa wahusika wameamua kuutumia Mkoa wa Kilimanjaro.


“Baada ya kuwahoji askari wale, walidai kuwa walikodishwa na mfanyabiashara huyo kuipeleka bangi hiyo wilayani Rombo tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini Kenya ambako inaaminika kuna soko kubwa,” alisema.


Kamanda Boaz alisema hivi sasa polisi wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha wanafanya uchunguzi kubaini mtandao wa askari hao unaojihusisha na vitendo haramu.
Aliongeza kuwa hatua inayofuata kwa askari hao ni kufunguliwa mashtaka ya kijeshi na iwapo watakutwa na hatia watafukuzwa kazi kisha watafikishwa katika mahakama za kiraia.


Kamanda Boaz alibainisha kuwa kwa kawaida askari wanapotoka mkoa mmoja kwenda mwingine hupatiwa kibali maalumu cha kusafiria (Movement Order).


Alisema kibali hicho husaini kila mkoa ambao askari husika hupita, lakini waliokamatwa na bangi hawakuwa nacho.
Kamanda Boaz alibanisha kuwa kwa hali ilivyo askari hao waliondoka na gari la mkuu wa FFU bila kumpa taarifa wala kupata kibali chake.


Tanzania Daima limedokezwa kuwa askari hao wamekuwa wakisafirisha bangi hiyo mara kwa mara kupitia mji huo wa Himo bila kukamatwa kutokana na gari lao kuwa na namba za kijeshi, hivyo kuwa vigumu kwa askari wenzao kuwatilia shaka.
Taarifa zaidi zimedai kuwa kukamatwa kwa askari hao kulitokana na gari lao kupata hitilafu katika eneo hilo la Kilemapofu, na ndipo askari wa doria walipofika kwa lengo la kutoa msaada kwa wenzao, lakini ghafla walisikia harufu ya bangi.


Mtoa taarifa aliyezungumza kwa sharti la kutotaka jina lake litajwe, alisema baada ya askari hao kusikia harufu ya bangi waliwaarifu viongozi wao waliowaamrisha walifanyie upekuzi gari hilo sambamba na kuwaweka chini ya ulinzi askari wote waliokuwamo.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa katika upekuzi huo walibaini uwepo wa magunia 18 ya bangi yaliyolengwa kupelekwa nchini Kenya.
Kilibainisha kuwa baada askari hao kukamatwa, mmoja wao alisikika akiongea na mtu aliyemuita bosi kumuarifu kukamatwa kwao.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa bosi aliyearifiwa tukio hilo alihoji imekuwaje wakakamatwa kizembe namna hiyo.
Kilidokeza kuwa bosi huyo alimhoji aliyempigia simu kuwa wamebaki na shilingi ngapi ili wawape rushwa polisi waliowakamata.
“Bosi aliambiwa kuna laki tano, naye akawaambia wawape fedha hizo zote, lakini kwa bahati mbaya hawakufanikiwa,” kilisema chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, hakukiri wala kukanusha kuwapo kwa taarifa za kukamatwa kwa askari wake.
Tanzania Daima lilitaka kujua Jeshi la Polisi mkoani Arusha limechukua hatua gani dhidi ya askari hao ambapo kamanda Sabas alisema hayupo katika nafasi nzuri ya kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa yupo hospitalini.

Sunday, May 19, 2013

HAYA NDIO MAJIBU YA HALIMA MDEE KUHUSU STORY ZA YEYE AKUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Kupitia season mpya ya Clouds Fm, ndani ya so 
so fresh na fetty, Mh Halima Mdee jana 
amefunguka juu ya swali aliloulizwa kuhusu
 story zilizosambaa kuwa 
anashiriki mapenzi ya 
jinsia moja.

aah unajua huwezi kuzuia watu kusema, 
na mimi huwa sihangaiki na watu wanasema nini,
 lakini ukitaka kumjua Halima unaweza
 ukamchunguza kirahisi sana, kwa
 kumuangalia alipotoka, 
historia yake na mahusiano yake,
 ambayo mengine ni wazi sana watu 
walikuwa wanayajua, 
watu wanapenda ku speculate pale 
ambapo wanaona kitu ambacho hawati kuona, 
sasa hilo swala lilishaandikwa sana, 
nadhani walioandika baadae wakaja 
kuomba radhi kwasababu waligundua 
wameandika kitu kisicho sahihi, 
probably kutokana na sauti yangu you know, 
probably kutokana na tembea yangu, 
kwasababu mimi nimekulia kwenye 
familia ya wanaume watupu umeona eeh,
 mimi nimekuwa ni mpambanaji tokea utotoni, 
kwasababu nimezungukwa na jeshi la kibabe,
 thats who iam, lakini mtu anaetaka kumjua
 Halima na ana uhuru tu, hata akitaka niwatajie
 list ya watu wangu i can do that, 
 lakini sidhani kama is their damn business, 
cause ma life is personal, 
na wakitaka kuchunguza wachunguze 
kwa mpango wao na watapata taarifa, 
 kwa uhuru tu, na wanaweza wakatoa tangazo kwamba
 jamani watu waliowahi kuwa na 
uhusiano na huyu if any wajitokeze, watajitokeza
 kama wapo upande huo, watajitokeza
 kwasababu sasa hivi si dunia huru bana

Yule Kijana Aliyesema kuwa Diamond ni Kaka yake Akanusha na Kusema Si Kweli Nimechezewa mchezo tu Simjui Diamond


Katika Hali isiyo ya kawaida yule kijana ambae video yake ilienea mtandaoni akiongea kuwa Diamond ni kaka yake wa damu walio changia baba...na kusema kuwa Diamond Amemtelekeza na kuwa hataki kumsaidia kwa vyovyote....Jana katika Kipindi cha XXL segment ya U-heard Amesema kuwa Hamjui Diamond na wala si kaka yake ....Alipoulizwa kuhusu Video aliyorekodi Akimtuhumu Diamond alisema kuwa alichezewa mchezo na rafiki ake ambae alimwambia Afanye kama ana Act kuongea hivyo coz anafanana na Diamond kwa Sura,,,Baada ya Ku act hivyo alishangaa Kesho yake video imewekwa You Tube na Blogs Kuanza kuandika....So Amesema Si kweli na Amemuomba Diamond Msamaha, Midomo ilimponza

WEMA NA RAHEEM WAFUNGUKA JUU YA PICHA YAO YA KIBALOVIDAVE


Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, huku akifurukuta kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ametokelezea na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
GUMZO MITANDAONI
Picha hiyo ambayo pozi lake ni ‘very romantic’ imezua gumzo katika mitandao mbalimbali ilipotundikwa na wadau wengi walionekana kuamini kuwa Wema alikuwa akimnadi mpenzi wake mpya.
Mtoa maoni mmoja aliandika: “Naona Wema ameamua kutuonesha shem wetu mpya, sasa hapo kazi kwa wenye vijicho.”
Mwingine aliandika: “Mmh! Mbona (Raheem) haonekani uso? Kama lengo lake lilikuwa kumwanika angemuacha tu aonekane ila dah! Ana kifua kizuri sana. Huyu jamaa anaonekana anafanya sana mazoezi.”
DIAMOND ATAJWA
Katika gumzo hilo, wengine walikwenda mbali zaidi, wakisema kwamba inawezekana Wema alikuwa na Raheem kwa siri muda mrefu lakini sasa ameamua kuvunja ukimya ili kumringishia x – boyfriend wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Siku zote alikuwa wapi? Atakuwa anamwoneshea Diamond tu huyu,” mtoa maoni mwingine aliandika.
INTERVIEW NA RAHEEM
Ni jadi ya magazeti ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi Mchanganyiko kutafuta mzani wa habari kabla ya kwenda hewani hivyo lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye kwenye vyombo vya habari.

Alisema: “Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu, haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu. Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.
“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si mtu wangu kabisa…she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Risasi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?
Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?
Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.
Risasi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?
Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.

Wema alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kupiga picha na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina uhusiano wowote na suala la mapenzi.
“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki) wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali popote…sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Risasi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Risasi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi…lile pozi lipo romantic sana, hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante

Saturday, May 18, 2013

HAYA NDO MAJINA YA WANAFUNZI WA CBE NA UDSM WALIONASWA WAKIJIUZA ( MAKAHABA)

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.

Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.

“Msako huo ulifanyika Maisha   Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema

Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.

Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia

Friday, May 17, 2013

JAH RULE AMETOKA JELA NA MVUTO WA HATARI

 
Rapper Jah rule ametupia picha yake kupitia mtandao wa instagram ikimuanyesha akiwa na mwili wa mazeoze tofauti na alivyoingia jela. inaonekana alikua akipiga chuma wakati akitumikia miaka yake miwili aliyokuwa amefungwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria na tax evasion

BREAKING NEWZZ! LINAH SANGA NA BARNABA KUTUPIWA VIRAGO THT!!

KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’  huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.
 
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.
 
Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.
 
“Juzi Lina,haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushahuri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.
 
Hata hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata ilizisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT  na watu wa karibu wanaoiunga THT.
 
“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa,  sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.
 
Aidha, katika ‘ku-balance’ huondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.
 
Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.
 
Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee  na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.
 
Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.
 
Mtandao huo wa kijamii  blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13.

HUU NDIO WARAKA WA MASHITAKA YANAYO MKABILI MSANII LADY JAYDEE MASHTAKA YALIYOFUNGULIWA NA JOSEHP KUSAGA NA RUGE MTAHABA, UCHEKI HAPA

 
HUU NDIO WARAKA WA MASHITAKA YANAYO MKABILI MSANII LADY JAYDEE MASHTAKA YALIYOFUNGULIWA NA JOSEHP KUSAGA NA RUGE MTAHABA... JE' HII NI WAZI JIDE NI KOMANDO MPAKA JAMBO LILE LINAFIKIA HATUA HII???

NEWS: T.I.D AJITOA KWENYE SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAY DEE...


 
MNYAMA...U CAN CALL HIM T.I.D a.k.a TOP IN DAR,LEO KUPITIA FANPAGE YAKE YA FACEBOOK AMEFUNGUKA MENGI KUPITIA YEYE KUJITOA KWENYE SHOW INAYOFUATA YA LADY JAY DEE AMBAYO ITAFANYIKA TAREHE 31 MWEZI HUU.



''
three reason why i cant do lady JIDE SHOW .............No.1 i have better contract pays me better than.No.2 i really dont want to be between anybodys conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari...No.3 nataka kuoa muda wangu ndo huu ...............kama nimekukosea captein na madame kazeni but i have been thru same shit.........''ALIANDIKA T.I.D.


Movie aliyoigiza mama Kanumba kutoka leo

mama-steven-kanumba-without-a-daddy-movie-poster-pichaFilamu inayoitwa “Without Daddy” ambayo imekua ikipikwa kwa muda mrefu sasa, inatoka leo. Filamu hiyo ina upekee fulani sababu itakua ni filamu ya kwanza ambayo Mama yake marehemu Steven kanumba ameigiza.

Watu wengi wana hamu kuangalia movie hii kwa sababu mbalimbali. Wengine wanataka wapime kipaji chake, wengine ku-show support kwa mama wa msanii kipenzi chao wanayem-miss… Steven Kanumba.

Utabiri wangu ni kwamba mama atakuwa mkali kwenye kuigiza. Sababu? Kwanza yuko comfortable mbele ya kamera kwa interview mbalimbali nilizomuona. Pili asilimia kubwa ya kina mama wana uwezo wa kuigiza sababu sehemu kubwa ya maisha yao ni kuigiza mbele ya watoto, kama vile wanapotumia ucheshi kuficha ugumu au ukubwa wa tatizo ili watoto wasi-panic. Tatu yeye ndiye aliyezaa kipaji, Steven Kanumba, hivyo kuna uwezekano mkubwa personality na ucheshi aliokua nao hayati Kanumba kwa kiasi fulani aliridhi kutoka kwa mama yake

Producer Master Jay Aziponda Tuzo za Kilimanjaro Music




MTAYARISHAJI nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joachim Kimario 'Master Jay' amesema amekosa imani na Tuzo za Kilimanjaro Music, kwa kuwa zinalengo la kuwadhalilisha baadhi ya wasanii.
 
Master jay amekosa imani kumetokana na Kamati ya Kilimanjaro Academia ambayo imepewajukumu la kuchagua wasanii kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kukosa sifa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Master Jay alisema tatizo linaanzia kwenye kamati hiyo kuchagua wasanii waliokosa sifa na vigezo, huku ikiwa haiko wazi kwa wadau pamoja na wasanii ambao ni washiriki wa tuzo hizo.
 
Alisema watu waliochaguliwa kwenye kamati hiyo, wamekosa uelewa wa muziki na ndiyo maana wanachagua baadhi ya wasanii waliokosa ubora na kusababisha kupoteza imani ya tuzo hizo kwa jamii nzima.
 
Mtayarishaji huyo alisema ndiyo maana baadhi ya wasanii wanajitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kuogopa kujidhalilika.
 
"Sijui ni akina nani wanaounda kamati hiyo kwani imepoteza sifa na ndipo tatizo linapoanzia hapo kila mwaka, kukosa uelewa kwenye kamati hiyo na kutokuwa na uwazi kunachangia malalamiko ya kila siku kwa baadhi ya wadau wa muziki.
 
"Baadhi ya wasanii wanalalamika sana kuhusu tuzo hizi na ndiyo maana wengi wanajitoa, si kwamba wanajitoa kwa kuogopa kushindana hapana bali kudhailika kwani hizi tuzo sasa zinadhalilisha baadhi ya wasanii," alisema Master Jay
Hata hivyo aliwapongeza kwa kuongeza vipengele vingine kwenye tuzo hizo, ambapo mwaka jana kulikuwa na vipengere 29 na sasa vimeongezwa na kuwa 32.
 
"Kila mwaka wanapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua 30 nyuma, hali ambayo inaonesha hakuna maendeleo yoyote kwenye upande wa tuzo hizo, hivyo wanahitaji marekebisho ili kuwe na usawa na kurudisha imani ya tuzo hizo kwa wasanii," alisema Master Jay.
 
Kwa upande wake Mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala alisema tatizo lipo kwa waandaaji ambao ni Kampuni Bia Tanzania (TBL) kushindwa kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wote wa muziki nchini.
 
Alisema TBL inatakiwa kuelimisha umma kujua kazi ya Kilimanjaro Academia, inavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa tuzo hizo zinavyokwenda, ili kuepuka ulalamikaji unaojitokeza kwa baadhi ya wadau wa muziki.
 
"Elimu ikitolewa kwa washiriki pamoja na wadau wa muziki, imani itarudi kwenye tuzo hizo na watajua mchakato mzima unavyofanyika hivyo uwazi wa jambo hilii ndiyo utapunguza malalamiko katika tuzo hizo," alisma Luhala.

PICHA ZA NUSU UCHI ZA KUNDI LA "ZE KOMEDI' ZAVUJA'.....HII NI ZAIDI YA AIBU

Picha za aibu  zinazowaonesha wasanii wa kundi la Ze Komedi wakiwa kwenye fukwe moja ya huko Kigamboni zimezua balaa kubwa ......
 Happy  kabla  hajavua  nguo.... 
==

Mtandao  huu  umefanikiwa  kuzipata  picha  hizi  kutoka  kwa  msomaji  wetu  mpendwa  ambaye  kwa  uzalendo  wake  ametutumia  kwa  njia  ya  email  huku  akielezea  kwa  kifupi  kuhusu  sakata  hilo  la  aibu.....

 
Happy akichezewa matiti na master Face huku akichekelea
Huyu  ni  Happy na Master  Face  wakifanya  Uchafu wao....Hapa  wanatomasana  kabla ya uzalendo kuwashinda  na  kuamua  kuvunja  amri  ya  sita...
Vipi  baby....umezidiwa.....!!!! Aibu tupu 
==
Mdau  huyo  anaripoti  kwamba, kundi  hilo  liliingia  ndani  ya  ufukwe  wa  Chadibwa  na  kuanza  kufanya  mambo  ya  aibu  mbele  ya  watu..... 
Wasanii  walioongoza  kwa  mambo  ya  aibu  ni  mdada  mmoja  aliyejulikana  kwa  jina  la HAPPY  ambaye  ni  mrembo  aliyejigeuza  mbwa  na  kukubali  kushikwashikwa  ovyo  matiti  yake  na  viungo  vingine  "sensitive"  bila  kujali  watu.....

 Matiti  bado  yanaendelea  kuteswa
Kiwewe  naye  alikuwa  kivyake  na  wakwake.....
  Mbali  na  Happy, kulikuwa  na Msanii KIWEWE ambaye  yeye  alikuwa  akijimilikisha  VIUNO  vya mabinti  hao  bila  aibu..... 
 Achilia  mbali Kiwewe, alikuwepo  pia  MANAIKI SANGA  ambaye  naye  alikuwa  akikumbatia  watatu  watatu....Cha  ajabu  ni  kwamba, yeye  alikuwa  kavaaa, akina  dada  walikuwa  uchi.....
 Aliyetia  aibu  ya  mwaka  ni MASTER FACE ambaye  kwa  mujibu  wa  mdau  alitutumia  picha  hizi  ni  kwamba  yeye  na HAPPY  walifikia  hadi  hatua  ya kuvunja  amri  ya  sita  nyuma  ya  gari.....!!!!
Uzalendo uliwashinda wakaamua  wamalizane....
 Asante  sana  mdau  kwa  picha  na  maelezo.....

Thursday, May 16, 2013

CPwaa ateuliwa kuwa msimamizi mkuu na MC wa michuano ya Foosball.


 Cpwaa, msanii maarufu na wa kimataifa wa Bongoflava akisaini mkataba wa kuteuliwa kuwa  msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) nchini Tanzania, pamoja naye ni Caroline Kakwezi meneja masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe Mkurugenzi wa Heineken Tanzania.

 

Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe – Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, kulia Cpwaa na Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.


Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe – Mkurugenzi Mkuu na Cpwaa msanii maarufu wakishikana mikono na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania baada ya kusaini mkataba wa kuteuliwa kuwa msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) kulia ni Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.

Msanii maarufu wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya CPwaa ateuliwa na kampuni ya bia Heineken Tanzania kusimamia michuano ya mpira wa mezani (Foosball) pamoja na kutangaza na kuhamasisha mchezo huo wakati wa mashindano ambayo ni endelevu.Mpango huo ulikamilishwa kati ya kampuni ya Brainstormmusic & Media Co. Ltd na Heineken Tanzania Limited

Wednesday, May 15, 2013

RIPOTI KUHUSU RAISI KIKWETE KUONGEZEWA MUDA WA KUKAA MADARAKANI HADI 2017

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani.
 Rais Jakaya Kikwete
Profesa Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF, Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017.

Hata hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba yamepingwa vikali na Serikali na viongozi wake watatu waandamizi ambapo walijibu walipoulizwa kwa maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma wanakohudhuria kikao cha Bunge.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alijibu: “Mchakato wa Katiba upo ‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna sababu ya kufanya hivyo.”

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini kwangu nitasema ni kitu gani.”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alijibu kwa utani bila ya kufafanua: “Njooni niwajuze, unajua kamba haitoki Ukambani kama ilivyo kamba.”

Profesa Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali wazo hilo akisema wananchi hawatakubali na taifa linaweza kuingia katika mtafaruku.

“Nitapenda kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo kwani litachafua taswira ya nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala bora,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa sababu ya Katiba kwani bado uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru unawezekana kwa utaratibu mwingine.

“Mchakato wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatuambia kwamba mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa CUF tunasema kwamba hata kama Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi hicho kuwe na Tume huru ya Uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.

Jukwaa la Katiba kutinga mahakamani

Siku nne baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya mwongozo kuhusu uundwaji wa Mabaraza ya Katiba, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema litafungua kesi mahakamani kutaka kusitishwa kwa mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa madai kuwa uendeshwaji wake umejaa mizengwe, itikadi za vyama na rushwa. Limetaja sababu tano ambazo zimekiukwa.

Limesema kesi hiyo itasimamiwa na timu ya mawakili 10 watakaoongozwa na Mwanasheria wa masuala ya Haki za Binadamu, Dk Rugemeleza Nshala na itawasilishwa mahakamani siku saba zijazo kuanzia jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alitaja sababu hizo kuwa ni kutokufanyiwa marekebisho katika sehemu tatu za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoahidiwa na Rais Kikwete, kuvurugwa kwa Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba, mchakato wa Katiba kukosa uongozi, kuminywa kwa demokrasia wakati wa mchakato huo pamoja na Jukwaa hilo kuzuiwa kuonana na Rais ili kueleza upungufu uliopo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

WANAFUNZI WA SHULE YA MANZESE WAKUMBWA NA "POPO BAWA"....30 WAMEANGUSHWA CHINI MUDA HUU



Wanafunzi wa shule ya secondary manzese zaidi ya 30 muda huu wanaanguka hovyo na kusema a maneno yasiyoeleweka kutokana na kinachohisiwa kuna nguvu za Giza zimetanda shuleni hapo huku wakijibamiza kwenye miti:
 
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese aliyeanguka na kuweweseka.
Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha wanafunzi wa shule hiyo kukimbia ovyo,kuanguka na kuweweseka. Wadau wa mambo ya giza wanadai ni NGUVU ZA KICHAWI

Blackberry BBM Service is Coming to iPhone’s & Androids.




The only thing that may have held so many iPhone and Android lovers from tossing their Blackberry’s was the infamous BBM service that the phone provided. But according to the company’s vice president it looks as if the BBM service will be accessible to iPhone and Android owners in the near future.

Announcing the move at the company’s developer conference, software vice president Andrew Bocking said: “the time is definitely right for BBM to become a multi-platform mobile service. BBM has always been one of the most engaging services for BlackBerry customers, enabling them to easily connect while maintaining a valued level of personal privacy. We’re excited to offer iOS and Android users the possibility to join the BBM community.”

Chief executive Thorsten Heins called the move “a statement of confidence”. BlackBerry says that BBM has more than 60 million monthly active users, with more than 51 million using BBM for an average of 90 minutes per day. Its customers collectively send and receive more than 10bn messages daily, with almost half read within 20 second of being received, it said.

The free app will be available once approved for Apple’s iOS 6 software released last year and devices running Android 4.0 or higher, released in late 2011.

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Mabalozi wa Tanzania nchini Marekani na Umoja wa Falme za Kiarabu.



Tuesday, May 14, 2013

Lady Jay Dee Ataka Kuihama Tanzania-Achoshwa na Wanaomfitini

Ni masaa machache tu yaliyopita mwanamuziki LADY JAYDEE ameandika kutaka kuihama nchi yake  na kuelekea nchi jirani ya  KENYA ...

Lady Jaydee anafikiria kwenda kuomba uraia KENYA ama MALAWI kwa kile kinachoonekana kuwa ni kutaka  kujinasua  katika  migogoro  inayomkabili ambayo  tayari  iko mahakamani....

Mwanamuziki huyo ame-tweet kupitia mtanadao wa kijamii wa twitter na kuandika 

KILICHOJILI JANA MAHAKAMANI WAKATI JIDE ALIPOENDA KUSIKILIZA MASHTAKA YAKE HIKI HAPA


                                         Jide na Mumewe wakiwasili mahakamani leo.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee(Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
 
Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo

Monday, May 13, 2013

ANGALIA PICHA ZA WANAFUNZI KUMI NA MZUNGU MMOJA WALIVYOKAMATWA KATIKA NYUMBA MOJA WAKIFANYA MAPENZI NA MBWA HUKO MOMBASA KENYA,KAMA UNAMWANAO SOMA MAJINA YAO HAPO

 

Kenya ilikua kimya kidogo baada ya uchaguzi mkuu kuisha lakini kwa sasa inamake headline sana katika vyombo vya habari hasa katika nchi za afrika mashariki. Tukio lililoifanya kuandikwa sana katika mitandao ni kutokana na wanawake 12 pamoja na raia mmoja kutoka anayetokea nchini Uswiss kunaswa na polisi wakifanya mapenzi na mbwa huku wakichukuliwa video.


vyanzo mbalimbali ni kua mzungu huyo alikua akiwalipa wakina dada hao kiasi cha sh 3000 za kenya ili kufanya mapenzi na mbwa huyo huku wakichukuliwa video.

hii ni picha ya mtuhumiwa akiwa nchini kwao
Inadaiwa kwamba siku za hivi karibuni kumekua na utitiri wa raia wa kigeni kuingia nchini kenya na kutafuta wadada hasa wanafunzi wa kufanya na ngono na hat kuwafanyisha ngono na mbwa kama ilivyotokea katika tukio hili. Baada ya polisi kuwafatilia kwa mda mrefu hatimaye siku ya siku ikafika na hatimaye kuwakamata wadada 10 na mwanaume huyo wakiwa katika nyumba moja huko kenya katika lilitokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali, jijini Mombasa kenya


Na  haya  ndo  majina  11  ya  watuhumiwa  wa  kashfa  hiyo  chafu.....
  1. Christopher Clement Weisssenrieder, 
  2. Janet Akoth Omollo, 
  3. Mercy Waithera Karanja, 
  4. Mary Nyambura Kimani, 
  5. Magdaline Wairimu Chege, 
  6. Celestine Nekesa Sitati 
  7. Dorcus Melishah Indakwa
  8. Lydia Nyaboke Momanyi, 
  9. Philidelia Mawia Solomon, 
  10. Anne Wanjiku Gichuki 
  11. Celilia Nzambi Katuku

Thursday, May 2, 2013

R.I.P Chris Kelly wa "Kriss Kross"

R.I.P Chris Kelly wa "Kriss Kross"

Rapa Chris Kelly a.k.a Mac Daddy wa kundi la zamani la Kriss Kross amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34. Imeripotiwa kwamba rapa huyo alikutwa nyumbani kwake huko Atlanta akiwa hana fahamu na kutangazwa kuwa amekwisha kufa baada ya kupelekwa huko Atlanta Medical Center.

Chanzo cha kifo chake hakijajulikana bado.

Hii ni moja ya nyimbo kali zilizo-hit 'miaka ya tisini' kutoka kwa Kriss Kross - Jump

http://youtu.be/010KyIQjkTk
R.I.P Chris Kelly wa "Kriss Kross"

Rapa Chris Kelly a.k.a Mac Daddy wa kundi la zamani la Kriss Kross amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34. Imeripotiwa kwamba rapa huyo alikutwa nyumbani kwake huko Atlanta akiwa hana fahamu na kutangazwa kuwa amekwisha kufa baada ya kupelekwa huko Atlanta Medical Center.

Chanzo cha kifo chake hakijajulikana bado.

Waziri Mkuu Pinda ahudhuria sherehe za kusimikwa kwa Askofu msaidizi wa Dar Mhashamu Titus Mdoe.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es slaam, Mhashamu Titus Mdoe katika ibada ya kumsimika askofu huyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Msimabazi Centre jijini Dar es salaam, Mei 1, 2013 . kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwadhama Polycarp Kadianali Pengo (kushoto) wakishuhudia wakati Mhashamu Titus Mdoe, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam akikata Keki katika Ibada ya kumsimikwa kwa Askofu huyo zilizofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre jijini Dar es salaam Me 1, 2013. (Picha na  Ofisiya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es slaam, Mhashamu Titus Mdoe katika ibada ya kumsimika askofu huyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Msimabazi Centre jijini Dar es salaam, Mei 1, 2013 . kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wednesday, May 1, 2013

DIAMOND PLATNUMZ, AKIWA NYUMBANI KWA MTOTO WA KAMANDA KOVA UINGEREZA.