Sunday, November 2, 2014

!KAMA HAUKUPATA NAFASI YA KUTAZAMA PICHA ZOTE ZA HARUSI YA MH JOSHUA NASARI ILIVYOFANA..HIZI HAPA


Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30 ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi zilikuwa zikipambwa mdogo mdogo zikapanda Kilima zikiwa na maharusi Joshua Nassari na Anande Nnko safari ilikuwa ni kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru tayari kwa ajili ya Ndoa.
Hatimaye Bw Harusi Joshua Nassari anateremka katika usafiri wake aina ya Range Rover muda mfupi baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kama kwa Mchungaji Babu.

waheshimiwa kibao walikwepo.


Photo: And more

HAWA WALIKWEPO ILI KUNOGESHA WA KWANZA KULIA NI JESSICA PAUL NA MARAFIKI ZAKE

Wageni mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ya ndoa mmoja wapo ni huyu ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai(katikati)
Bibi Harusi Anande Nnko alikuwa ni mwenye furaha kila wakati ,"Full Tabasamu."
Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu walikuwa wamevalia mavazi nadhifu aina ya suti wakingojea ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga.
Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko.
Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX.
Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko.
Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari
Kisha Maharusi wakapongezana.
Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi.
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani)
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana.
Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao.
Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza)
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.
Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka.
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani

Hivi ndivyo mwili wa aliyekuwa rais wa Zambia,Michael Sata ulivyopokelewa..

Sata8
Mwili wa Rais wa Zambia, Michael Sata umewasili Zambia tayari kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika November 11.

Mwili wa rais huyo umewasili uwanja wa ndege wa Kenneth Kaunda International Airport na kupelekwa Mulungushi International Conference Centre kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine zilizopangwa na Serikali ya nchi hiyo kufanyika kabla ya mazishi.

Hizi ni picha 10 zikionyesha namna mapokezi yalivyokuwa katika jiji la Lusaka siku ya jana Novemba 1.
Sata4
Sata5
Sata6
Sata9
Sata11
Sata10
Sata8
Sata7
Sata Kuwasili
Sata3

Thursday, October 30, 2014

LADY JAYDEE AANZA KUMUIMBA MTALAKA WAKE.

Mdau mmoja Huko Jamii Forums Amefunguka Hivi kuhusu Tangazo la Mgahawa Mpya wa MOG ambalo amelifanya Lady Jady linalorushwa Radio Mbali Mbali: “Naamini wengi wamesikia tangazo jipya la mgahawa wa Jaydee unaokwenda kwa jina jipya la MOG na kikolombwezo cha LIFE IS TOUGH na mwishowe anamalizia na YAHAYA UNAISHI WAPIII Wenye kujua mafumbo wanajua anamaanisha nini!!! Jaydee ni mtu wa nongwa sana na anapenda visasi kapitiliza, ukigombana naye hakuachi mpaka akutungie wimbo wa vijembe kafanya hivyo kwa wengi tu wakiwemo Ruge, Mwana FA, na sasa vijembe vyote ni kwa mtalaka wake,

Friday, October 3, 2014

MLAPA NG’OSHA: KALALE PEMA (OFFICIAL VIDEO)

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Gabriel Samalu Ng’osha ‘Mlapa Ng’osha' ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Kalale Pema' aliyoelezea maisha ya mateso anayopata mama mjamzitoVideo hiyo imetengenezwa chini ya prodyuza Melkiadi Oreje 'OJ' wakati audio ikifanywa na Lebo ya Audio Visual ya nchini Kenya chini ya maprodyuza Haptune & Douncher.

Saturday, September 6, 2014

MAALIM SEIF APATA AJALI MBAYA MKOANI MWANZA: ALIKUWA ANAELEKEA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA MARA JANA

Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya Na Karoli Vinsent
Habari zilizotufikia mda huu Zinasema MSAFARA wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad umepata Ajali mbaya  Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.       
Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu,
Mkurugenzi wa habari wilaya'na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
    Akithitisha kutokea kwa Ajali hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu, mda huu kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad  ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,
Rehema Mwendaalikuwa kwenye msafara huo aiugulia maumivu
“Ni kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF  Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido  ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.

Kambaya alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga  Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo  lilikuwa la nne kutoka gari  lililombeba Maalim Seif  kwenye msafara huo,

Tazama Picha za Ajali Mbaya Ambayo Haijawai Kutokea Musoma,Na Kusababisha Fiesta Kuahirishwa Mkoani Hapa






Ni ajali mbaya kuwahi kutokea katika mkoa wa Mara...Ni ajali iliyotokea leo asubui mida ya saa nne asubuhi ambapo basi la J4 lilokuwa likitoka Mwanza kwenda tarime limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach ambalo lilikuwa likitoka Musoma likienda Mwanza.

Chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo aina ya Land Cruiser ambayo ilikuwa ikiovatek bas la J4 ndipo baada ya kupoteza uelekeo kwenye kona ilioko maeneo ya sabasaba %ziro ziro% na kuacha mwanya wa basi hizo mbili kupoteza uelekeo na kugongana uso kwa uso.

Mpaka kufikia sasa watu waliofariki katika ajali hiyo ni 70 ambapo bas la J4 limeuwa abiria wote na majeruhi wa mwanza coach ni wengi pia.

Mungu zilaze mahali pema roho hizo