Tuesday, May 8, 2012

"SEND OFF PARTY YA DADA REHEMA MATAMBO ILIYO FANYIKA 02/05/2012 MAGU AKISINDIKIZWA NA KAKA YAKE ARAPHAT"

UKUMBINI

Saturday, May 5, 2012

UCHAGUZI WA KUWACHAGUA VIONGOZI WATAKAO WAKILISHA VIJANA WILIYANI MAGU MWENYEKITI, KATIBU, MWASIBU NA WAJUMBE WAFANYIKA KWA AMANI NA MATOKEO KUTANGAZWA LEO

KABULA YA KUTANGAZWA MATOKEO
HAPA BAADA YA KUTANGAZWA MATOKEO

Tuesday, May 1, 2012

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI WILAYANI MAGU YA FANA SANA

MH. MAGEMBE

Bob Junior - Ni Chum

Sunday, April 29, 2012

Fanuel Sedekia - Ni Neema

Friday, April 27, 2012

MVUA ZINAZOENDEREA KUNYESHA WILAYANI MAGU

ENEO LA UWANJA SABA SABA IMESITAWI MAJANI.

Thursday, April 12, 2012

RAY THE GREATEST: POLE MAMA STEVEN KANUMBA

RAY THE GREATEST: POLE MAMA STEVEN KANUMBA:   Muda ulifika wa Mama Kanumba kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere maana wakati mauti yanamfika mwanae alikuwa safarini ...

Monday, April 9, 2012

Fahamu Historia ya Marehemu Steven Charles Meshak Kanumba

KAMATI YA MAZISHI YA MSANII STEVEN CHARLES KANUMBA YATOA RATIBA YA MAZISHI YA KANUMBA THE GREAT


IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 ASUBIHI SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P THE GREAT

RATIBA
Mwili wa marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.

Saa 3:30 asubuhi, mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali.

Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.

Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.
Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.

K.N.Y GABRIEL MTITU
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI

HABARI HII KUTOKA http://djchoka.blogspot.com

Saturday, April 7, 2012

BREAKING NEEWZZZZZZZZZZ!!!!!!!!!! STEVEN KANUMBA AMEFARIKI DUNIA!!

Msanii Steven kanumba enzi za uhai wake

msanii maarufu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili.

TULIKUPENDA SANA LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI. Tutamkumbuka Daima Milele.

Mwenyezi mungu aiweke Roho Yake Mahali pema peponi "AMEN"

Friday, April 6, 2012

Professor Jay ft Marco Chali - Kamili Gado ( Official Video HD)

Friday, March 9, 2012

MAPEI & SUPHI IN NEW WITOGWA STUDIO



BRO, JORAM AND BRO, SELE IN JOYCE M-PESA SHOP.



DOGO JORAM

BRO SELE

Sunday, February 26, 2012

GOSPER SONG

 
Posted by Picasa

Wednesday, February 8, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 HAYA HAPA