Saturday, April 7, 2012

BREAKING NEEWZZZZZZZZZZ!!!!!!!!!! STEVEN KANUMBA AMEFARIKI DUNIA!!


Msanii Steven kanumba enzi za uhai wake

msanii maarufu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili.

TULIKUPENDA SANA LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI. Tutamkumbuka Daima Milele.

Mwenyezi mungu aiweke Roho Yake Mahali pema peponi "AMEN"
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment