Monday, April 27, 2015

HABARI MPYA! AJIRA MPYA ZA WALIMU MWAKA 2015. ANGALIA HAPA


OFISI YA WAZIRI MKUU 
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA WALIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15

A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya       

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
i.                 walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi  11,366; 
 
i.                 walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari 
ii.              mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa  masomo ya  sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari

B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara            

Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i.                 walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii.              kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi; 
i.                 kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
ii.              hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
iii.            fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
                                                                        Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA. 
kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo:
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment