Thursday, August 1, 2013

Wakazi Magu watumia maji ya madimbwi


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu, Naomi Nko
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu, Naomi Nko

Zaidi ya wakazi elfu 25 wa mji mdogo wa Magu mkoani Mwanza wanalazimika kutumia maji yaliyotuama kwenye madimbwi kufuatia uhaba mkubwa wa maji unaoukabili mji huo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu sasa.
 
Baadhi ya wakazi wa mji huo wameeleza kuwa tatizo hilo limesababisha watumie muda wao mwingi kuyatafuta maji ambayo wakati mwingine sio safi wala salama kwa afya zao badala ya kufanya kazi za kuwaingizia kipato na hivyo kuwaweka kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko.

Adha ya ukosefu wa maji safi na salama katika mji wa Magu mkoani mwanza inawalazimu wakazi wa mji huo kutembea umbali wa zaidi ya kilometa tano ili angalau waweze kuambulia ndoo moja ya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutoka katika vijiji jirani.

Wapo wananchi wa magu wanaodiriki kujitosa katika madimbwi ambayo yana kila  ishara ya kukosa hadhi ya kutumiwa na binadamu kutokana na maji yake kutuama.
Suala la upatikanaji usioridhisha wa maji katika mji wa Magu pia limeibua mjadala katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya hiyo.

Hofu ya kuibuka kwa magonjwa ya milipuko sasa ni tele miongoni mwa baadhi ya madiwani wa magu.

mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya magu NAOMI NKO amekiri kuwepo kwa tatizo hilo.

Amicus Butunga, TBC Mwanza.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment