Wednesday, June 27, 2012
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Tuesday, June 26, 2012
WAHAMIAJI 42 RAIA WA EPHIOPIA WAFARIKI DODOMA
Kamanda Zelothe Stephen
WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu. Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi. Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana. Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wake wapo katika hali mbaya. Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku wahamaji watano wanaendelea kupata matibabu katika Zahanati ya kijiji cha Chitego ambapo wengine waliobaki wamehifadhiwa katika kanisa la Anglikan wakipatiwa huduma mbalimbali. Huduma hizo mbalimbali ni pamoja na kupewa maji , uji na matibabu. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuhaidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Tuesday, June 12, 2012
MAHAKAMA YASOGEZA KESI YA LULU HADI TAREHE 25 JUNI, 2012.
Lulu’ akishuka katika basi la magereza.
‘Lulu’ akiwa ndani ya mahakama.
‘Lulu akiteta jambo na wakili wake muda mfupi baada ya kufika mahakamani.
Akitoka mahakamani baada ya kesi yake kusogezwa hadi tarehe 25 mwezi huu, ambapo watetezi wa ‘Lulu’ wametakiwa kuwasilisha vielelezo vyenye uthibitisho wa umri wake ifikapo tarehe 13 mwezi huu, wakati upande wa serikali wameomba kuwasilisha vielelezo vyao tarehe 22 mwezi huu ili kumaliza tatizo la utata kuhusu umri wa mtuhumiwa huyo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika eneo lote nda na nje ya mahakama kuu wakati wa kesi hiyo.
HABARI TOKA http://dewjiblog.com
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Monday, June 11, 2012
KENYA WATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO YA SAITOTI
Mabaki ya ajali hiyo.
Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio hilo.
Idara ya polisi imesema uchunguzi utafanywa kujua sababu ya ajali hiyo, na balozi wa Marekani mjini Nairobi, amesema Marekani iko tayari kusaidia kwenye uchunguzi huo, ikiwa itatakiwa kufanya hivyo.
Msemaji wa polisi alieleza kwamba inavoelekea kuanguka kwa helikopta hiyo lilikuwa tukio la ajali.
Raia wa Kenya walikuwa na masikitiko Jumapili, baada ya taarifa ya ajali hiyo kujulikana, na watu wamekuwa wakizuru nyumba ya kuhifadhi maiti mjini Nairobi kutoa heshima zao.
Makamo wa rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea:"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi"
Rambi-rambi zimekuwa zikimiminika nchini Kenya, pamoja na za Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alipatanisha baada ya ghasia za uchaguzi uliopita nchini kenya.
Profesa Saitoti alikuwa akizungumza kwa ukali dhidi ya al-Shabaab na inaaminiwa alihusika na uamuzi wa jeshi la Kenya kuingia Somalia mwaka jana.
Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Alikuwa na umri wa mika 67.
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Friday, June 8, 2012
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI FURSA YA WASANII WA TANZANIA KUSHINDA EURO 5,000 KATIKA SHINDANO LA KUTUNGA WIMBO RASMI WA KUNDI LA MATAIFA YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP GROUP OF STATES)
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Monday, June 4, 2012
Habari kwa Kiswahili: FBI Kuzima Kompyuta 350,000 Zilizoambukizwa na Virusi.
Hivi sasa FBI iko katika maandalizi ya kuzima kompyuta 350,000 duniani kote kutokana kuambukizwa na kirusi aina ya Trojan aliyetengenezwa na kundi la Kiestoni ambalo ni la wahalifu.
Pia FBI wamefanikiwa kukamata kifaa aina DNS changer ambacho hutumika kutengenezea Vurusi hao.
Walinzi wa kimarekani ambao wanashughulika na uhalifu huo wanafahamu kompyuta na Macs zote zilizoambukizwa na hicho kirusi aina ya Trojan , hivyo basi hitimisho la wamiliki endapo watachukua hatua ya kutatua tatizo, njia ni moja ya kuviondoa vifaa hivyo katika mtandao (Internet).
Kifaa hicho cha kutengeneza virusi DNS changer, kilitengeneza na kuachia virusi hao kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2007. Kiliweza kuhasiri watumiaji, kwani kompyuta ilitenda kazi kinyume na inavyoweza. Na tatizo kubwa kwa watumiaji ilikuwa kompyuta kufanya kazi kwa taratibu sana katika mtandao. Pia virusi hivyo viliweza kulemaza antivirus programu na maelekezo ya kompyuta kuwa ya udanganyifu.
Virusi hivyo viliachiwa na kundi la wahalifu wa Kiestoni na kuaminika kuwa, idadi ya virusi vilivyoachiwa katika mtandao ni dola milioni 16.
Baada ya kashfa hiyo kugundulika, FBI walizima kifaa hicho kilichotumiwa na wahalifu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (server) na mmoja wao kuchua nafasi hiyo, lakini Bureau alitaka kifaa hicho (server) kizimwe kabisa kwa sababu kinagharamia makumi ya maelfu ya dola kukiendesha.
Bureau iliweka kifaa maalumu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (Server) kwa maombi ya DNS kutoka kwa kompyuta zilizoambukizwa, kwani bila kifaa hicho (server) kompyuta hizo zilizoambukizwa zisingeweza kuunganishwa na mtandao.
Jinsi ya kuunganishwa na mtandao
Amri ya mahakama iliruhusu kifaa cha kotoa mawasiliano ya mtandao (Sever) cha FBI kupitisha anwani ya IP ya wale walioambukizwa na muda wake kumalizika Julai 9, wakati kompyuta hizo zitakapokuwa zimeondolewa katika mtandao (offline). hatua hiyo, kompyuta zote zilizoambukizwa na virusi aina ta Trojan hazitaweza kuunganishwa katika mtandao.
Kuepukana na kompyuta yako kuzimwa na mtandao wa kuhakiki kompyuta zilizoambukiza "DNS ya FBI. ambao unaruhusu kwa sasa watumiaji kuangalia kama wana virusi na kuviondoa mapema.
Kwani inasemekana kuwa tayari kuna baadhi ya kompyuta 150,000 zimesafishwa virusi hao. Lakini baadhi ya wakosoaji wanaonya hii, kuwa haitoshi hivyo ni bora kutangaza na uhamasishaji unahitajika.
Ni lazima kuelewa kwamba kirusi aina ya Trojan kimeambatana na kirusi aina ya root kit ambacho ni kigumu kukiondoa katika kompyuta, hivyo kusababisha mtumiaji kufuta mpangilio na kuhifadhi upya.
Hata hivyo makampuni ya usalama wa mipangilio ya kompyuta ambayo ni Norton, Kaspersky, Trend Micro, Microsoft, McAfee na wengine, husaidia kukiondoa kirusi aina rootkit bila kufuta mipangilio ya kompyuta yako.
Kifaa hicho cha kutengeza virusi DNS Changer kimekuwa katika habari tangu Novemba 8, 2011, wakati botnet kubwa ya kusambaza virusi chini ya jina la kampuni ya Rove Digital, iliwekwa chini ya ulinzi na muungano wa msako ambao ni FBI pamoja na kundi la Kiestoni wahalifu. Na kutokea kukamatwa kwa wanaume sita.
HABARI TOKA http://cheraboy.blogspot.com
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Sunday, June 3, 2012
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU (DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA) ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA BANK WILAYANI MAGU KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.


Tanzanian Shilling Converter


