Tuesday, April 23, 2013
HIVI NDIVYO WALINZI WA CHADEMA WANAVYO MLINDA MWENYEKITI WAO MH. MBOWE

Walinzi
wa Chadema wakiwa wameninginia kwenye gari la Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe wakati wakielekea kwenye mkutano wa hadhara wa
chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Wajenzi, mjini Dodoma, Jumamosi
iliyopita.
ALICHOKISEMA DIAMOND, KUHUSU KUMREKODI WEMA NA KUSAMBAZA CLIP HIYO MTANDAONI, HIKI HAPA
Skendo iliyokuwa ikiendelea mtaani kuhusu msanii Diamond na tuhuma za kumrekodi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanadada Wema Sepetu, msanii huyo amekir kuwa ni kweli alifanya tuhuma hizo kwaajili ya kulinda penzi lake.
“Hivi karibuni Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu Penny akiwa na leno la kutaka kuni haribia juu ya mimi na mpenzi wangu, nilichukia sana kwahiyo siku alivyoamua kunipigia simu ndipo niliamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamoni kabisa” Alifunguka Diamond.
Sauti hiyo ambayo ilitoka kwa Wema Sepetu ikiwa inambembeleza Diamond waweze kurudiana pamoja kwakuwa bado anampenda, Diamond amekiri kuirekodi hiyo sauti lakini amekana kuisambaza mitaani na hajui nani kafanya hivyo.
“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi” aliongeza Diamond.
Baada ya kukiri kujutia, Diamond aliambiwa aombe msamaha Live ili Wema asikie ila alikataa na kusema hawezi kumuomba msamaha maana haoni kosa lake.
Monday, April 22, 2013
ROSE NDAUKA ANASWA KIMAHABA HADHARANI
Staa
anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa
akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke,
Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio
hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika
Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na
sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea
kwa ‘maji’, Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku
wakifanyiana vitendo vya kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea
ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana
mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo
alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni
waalikwa.
“Makubwa
haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi yaani leo ndiyo mara
ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na wanapendeza sema tu
hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika dada mmoja
akijadili na mwenzake. Pamoja
na hayo, sherehe hiyo ya mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada
ya wageni waalikwa kukolea ‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku
wasichana wakiwa wamevalia vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za
maungo nyeti hasa wakati wakiserebuka hivyo kuwatoa udenda wanaume
wakware.
Kwa hisani ya GLP
BREAKING NEWS:MAHAKAMA YA RUFAA YATUPILIA MBALI RUFAA YA KUPINGA USHINDI WA MBUNGE WA ARUSHA.

Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema. Godbless Lema
--
Ombi la kwanza la waleta rufani la
kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi ya
Mh.Lema na kutaka isikilizwe na jopo la majaji 7 limetupiliwa mbali leo
katika mahakama ya rufaa na sasa ni majaji walewale waliotoa hukumu
wamepitia ,Mahakama imetupilia mbali madai ya kwanza kwa kuwa hayapo
based on merits Kesi hii ilifunguliwa tena baada ya
Mh.Lema kushinda rufaa tarehe 21 desemba 2012,Warufani safari hii
walitaka mahakama ipitie upya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu
na wametaka kuwe na majaji saba.
Mahakama imetupilia mbali mashtaka yao na mahakama imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.
CHANZO JUMA MTANDA
WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND
Kwa Kumdhalilisha
Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !
Kitendo cha
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi
mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo
yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote
wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kuielekeza jamii kuishi
kwa kufuata na
kuheshimu maadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi
wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza
mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na
mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha
wanawake wa kitanzania"Tunaowaomba akinamama
na kinadada na
wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria
onyesho lolote lile litakalofanywa na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka
Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote
pale walipo.
Wanawake wote
wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za
mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji
wa Mwanamke"
Wanawake wote ambao
wamempa like au ad katika mitandao kama facebook kujiondoa mara moja na kogemea
kununua jarida au gazeti lolote litakalo mpamba mwanamuziki huyo.
HACKERS WAINGILIA TOVUTI YA MAKAMU WA RAIS WAANDIKA MATUSI NA KUWEKA NYIMBO ZA MATUSI
Katika
hali isiyo kuwa ya kawaida hacker waendele
kusumbua sasa ni zamu ya tovuti ya serikali ya makamu wa rais kilicho
andikwa nimatusi kwa maandishi na kuna muziki wa hiphop wa
mitusi.. Kuna mtu anajiita Govt Attacker. Mr. Spam ..! Eti ni Mmoroco.
Home -
uone. Je hii inamaanisha nini kwa systems zetu za mawasiliano kuwa
rahisi
kufanyiwa uhuni kama hivyi mpaka lini.
Hata hivyo wahusika wa tovuti hiyo wamefanikiwa kuondoa tatizo hilo kwa sasa
Hata hivyo wahusika wa tovuti hiyo wamefanikiwa kuondoa tatizo hilo kwa sasa
SOURCE BONGOCLANTZ
Mkuu wa wilaya ya Singida adai wanafunzi 118 wameacha shule mwaka jana kutokana na utoro.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, akitoa taarifa yake ya
utekelezaji wa ilani cha uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa mkoa wa Singida
(aliyeketi) Dk.Parseko Kone.Dk.Kone alifanya ziara ya kiazi katika
manispaa ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Jumla
ya wanafunzi 139 wa shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya
Singida waliacha shule mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
ya utoro.
Akitoa
taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa
mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone aliyefanya ziara ya kikazi ya siku
moja katika manispaa ya Singida, Mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi
amesema jumla ya wanafunzi 118 kati yao wavulana 76 na wasichana
42,waliacha shule kutokana na utoro.
Amesema
wengine 11 waliacha shule kutokana na kukosa mahitaji muhimu na wawili
walifariki dunia katika kipindi hicho cha mwaka jana.
Akifafanua
zaidi, amesema kuwa utoro wa wanafunzi katika baadhi ya shule,
umeendelea kuwa tatizo kubwa hali inasababishwa na wanafunzi kujihusisha
na biashara ndogo ndogo, kuajiriwa na pia wazazi kutowapatia mahitaji
muhimu.
Aidha,
Mlozi aitaja baadhi ya mikakati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi kuwa ni
pamoja na kuhamasisha na kuhimiza shule na jamii kuongeza vivutio
shuleni ikiwemo kuimarisha bendi za shule, michezo, kwaya na ngoma.
Mkuu
huyo wa wilaya, ametaja mikakati mingine kuwa ni kuhamasisha jamii
kuwapa watoto chakula cha mchana wawapo shuleni na orodha za watoro
kupelekwa kwa maafisa watendaji wa kata ili sheria zichukuliwe.
Wakati
huo huo, Mlozi amesema manispaa ya Singida inakabiliwa na upungufu wa
vyumba vya madarasa 274, nyumba za walimu 793, matundu ya vyoo 870 na
maktaba 43.
AVRIL KUZINDUA SINGLE YAKE NA OMMY DIMPOZ TAREHE 30 APRIL

Siku ya mkesha wa kuamkia sikukuu ya wafanyakazi "mei mosi", Msanii
kutoka Kenya Avril anatarajia kuzindua single yake aliyomshirikisha Ommy
Dimpoz huku perfomace za wasanii kutoka Kenya na Bongo zikitawala

LULU AINGIA LOCATION TENA KUANZA KUFANYA VITU VYAKE.

JACKLINE WOLPER: MIMI NA RAMMY GALIS SIYO WAPENZI BALI TUNAFANYA FILAMU YA KIISLAMU PAMOJA.
Rammy Galis


HII NDIO AC FAKE YA LULU INAYOTUMIWA NA WATU WASIOJULIKANA ONA HAPA.
Kwa upande wa Elizabeth Lulu ambaye bado anakabilliwa na kesi mahakamani, watu wanachulia advantage na kufungua account mpya ya twitter ambako ndipo Lulu ana-spend sana time zaidi ya facebook siku hizi. Kupitia Instagram Lulu aliandika “Haya lulu mwngne huyo on twitter…..!am tired jaman…nyie ma lulu nioneeni huruma basi…..!!!nimechoka kusikia case’z zenu!!!!NIMECHOKA JAMANI“. Accouunt hiyo fake inatumia jina la @Lulu_actress wakati account halisi ya lulu ni @Hotlulumichael. Kitu pekee ambacho kinaweza kuwatofautisha lulu fake na wengine ni alama ya Verified ambayo twitter hutoa kwa watu maarufu.
Sunday, April 21, 2013
Wakati Maduro akiapishwa kuwa rais mpya wa Venezuela avamiwa na kunyang’anywa kipaza sauti na mtu asiejulikana.
Mwanasiasa Nicolas Maduro ameapishwa rasmi kuwa rais wa Venezuela na kuchukua nafasi ya Hugo Chavez.
Akizungumza baada ya kuapishwa Maduro ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na upinzani ili kuijenga nchi yao iwe bora zaidi.
Maduro
mwenye umri wa miaka 50 amesema anataka kuanza kipindi chake cha urais
kwa kuwataka watu wa Venezuela kuijenga nchi hiyo iwe ya amani.
Hata
hivyo, wakati akihutubia mbele ya marais, mawaziri wakuu na viongozi
wengine, hotuba hiyo ilivurugwa baada ya mtu mmoja kuvamia jukwaa na
kumpokonya kipaza sauti.
Akizungumza
baada ya tukio hilo lililoleta mkanganyiko, Maduro ameisema vikosi vya
usalama vimeshindwa kazi, kwani angeweza kuuawa.
Maduro
ameapishwa saa chache baada ya tume ya uchaguzi ya Venezuela kusema
itahesabu tena kura zilizosalia za uchaguzi wa Jumapili iliyopita
kufuatia mpinzani wake Henrique Capriles, kudai kura zihesabiwe upya.
JUMBA LA LWAKATALE LAZIDI LETA UTATA BUNGENI

WABUNGE wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya kwamba kuna zuio la Mahakama.
Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.
Sambamba na hilo wametaka watendaji wa Serikali waliohusika kutoa vibali kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe hatua.
Mbunge wa kwanza kuanza kuzungumzia hilo ni wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) aliyetaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwemo cha mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani waliojenga nyumba zivunjwe licha ya kuwepo zuio la Mahakama.
“Mwaka jana Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka alivunja nyumba za kawaida licha ya zuio la Mahakama, lakini nyumba zilizo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 hazikuvunjwa kwa sababu ya zuio la Mahakama hii ni double standard (ndumilakuwili) hatuwezi kuvumilia.
“Wengine wenye nyumba ni viongozi tupo nao humu tena wa kiimani, lakini kwa nini viongozi tunafanya hivi wakati tunatakiwa tuwe wa mfano na tunawafanya viongozi wenzetu washindwe kufanya kazi zao?… hakuna haja ya kuogopa Waziri Huvisa (Mazingira) vunja nyumba, haiwezekani kuwa na nguvu ya fedha.
“Wabunge wenzangu tuazimie Manispaa ya Kinondoni na NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), wakavunje nyumba hizo ndani ya wiki moja , naomba kutoa hoja,” alisema.
Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimweleza; “Haiwezekani kutoa hoja kwa kuingilia vyombo vingine”.
Mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani mwenye nyumba katika eneo hilo la Mbezi Beach aliyejenga katika fukwe ya bahari kwa kuondoa mikoko na kuweka kifusi na kujenga nyumba ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dk Getrude Lwakatare (CCM). Hata hivyo wakati wa michango hiyo mbunge huyo hakuwa ndani ya Bunge.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) akichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alisema Kamati yake ya Ardhi na Mazingira ilitembelea eneo hilo la Mbezi Beach na kukuta aliyejenga katika kiwanja 2019 hakuwa na ofa wala hati.
“Ametumia pesa kuwarubuni watendaji akaondoa mikoko, akaweka kifusi na akajenga nyumba naomba Wizara ya Ardhi na ya Mazingira wawachukulie hatua watendaji hao,” alisema.
Akijibu hoja ya Bulaya, kuwa kwanini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuvunjwa wakati nyingine zilivunjwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema: “Sisi ni wajibu wetu twende mahakamani kusema watu hao wamevunja sheria kujenga hapo.
Wao wanaruhusiwa na Katiba na Mahakama itafuata sheria. “Nashauri Bulaya usitoe Shilingi kuzuia Bajeti ya Waziri, uje tuone huyo kigogo itakuwaje.” Hata hivyo, Huvisa alisema: “Nyumba tulizovunja hazikuwa na kesi na hii tuliyoiacha ilikuwa na kesi.”
Jumba la kifahari linalodaiwa kuwa la Mchungaji Lwakatare ambalo lilizinduliwa mwaka jana, limekuwa likitajwa kuwa lina thamani ya takribani Sh bilioni 1.5.
MAKAHABA WAWAVALIA NJUGA POLISI

Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, limelalamikiwa kwa vitendo vya baadhi ya askari wake kuvamia vyumba vinavyodaiwa kupangwa na watu wanaodaiwa kuwa makahaba (madanguro) na kuwapora fedha, simu na vitu vingine vya thamani nyakati za usiku.
Aidha, askari hao wamedaiwa kuwageuza wanawake hao mashine za kutolea fedha (Atm) ambapo hufika katika vyumba vyao kila baada ya wiki moja na kuwadai fedha kati ya Sh.30,000 na 50,000 kila mmoja kama hongo ili wasiwafikishe polisi.
Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya akina mama wanaoishi eneo la Mwananyamala walipozungumza na NIPASHE baada ya askari hao kukamata wanawake zaidi ya 87.
Kiongozi wa wanawake hao, Judith Rugamwa alidai kuwa, askari hao kutoka vituo vya Oysterbay na Mabatini wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga, jambo ambalo ni kinyume cha haki zao binadamu.
"Wakitukamata huwa wanasema kosa letu ni kufanya ukahaba, lakini tukifikishwa kortini kosa linabadilika na kuwa uzembe na uzururaji, wakati wametukamata vyumbani kwetu ," alisema Judith.
Alisema wamechoka kunyanyaswa kama wakimbizi na kuonya kuwa sasa wanajiandaa kupambana na kila askari atakayefika hasa nyakati za usiku na kuwavunjia milango ya vyumba vyao ili kuwamata na kuwalazimisha wawape fedha huku wakimtaja afande Swai na Emma kuwa ndiyo wanaoongoza uovu huo.
Akizungumzia tuhuma hizo, afande Swai alijitetea kuwa yeye binafsi hajawahi kushiriki katika kuomba fedha wala kupora simu za wanawake hao licha ya kukiri kuwa ndiye anayeongoza misako yote Kinondoni.
"Kuhusu madai ya kuomba fedha, siwezi kukataa kwa sababu mimi huwa siingii vyumbani kukamata wanawake hao, badala yake askari wangu ndiyo wanaohusika moja kwa moja kabla ya kuwaleta katika gari ambayo huwa nawasubiri, lakini kama wanafanyiwa hivyo naomba wawataje kwa majina askari hao," alisema.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela, alisema amri ya kuwasaka na kuwakamata makahaba hao huwa inatolewa na ofisi yake na kwamba madai ya polisi wake kuchukua fedha na simu za watuhumiwa ni uongo mkubwa.
"Kama kuna mtu amewahi kufanyiwa hivyo aje ofisi kwangu na ushahidi ili ofisi yangu ichukue hatua kali za kinidhamu kwa sababu anayeshawishi, anayetoa na kupokea rushwa wote wanafanya makosa, waache kulalamika waje niwasilikize," alisema Kenyela.
NATURE AKERWA NA KIPINDI CHA TELEVISHENI WAMTOA NA KUKATIZA INTERVIEW KISA KAVAA NDALA NA KAWOSH

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature,
ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku katika kipindi cha
burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa
akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala
na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji alisema
watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko
hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea
na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala
na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika
kupitia ukurasa wake wa facebook....
hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha
mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo,kunywa nimekunywa bt kuna baya
nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa
kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na
ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji
interview
Saturday, April 20, 2013
TAARIFA KUHUSU WALIOMALIZA DARASA LA SABA KUANZA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU
.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B ambapo Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia Mwananchi kwamba baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine, Sifa zinazotakiwa ili kujiunga…. mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba, atakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma, awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni”
Mkurugenzi
amekaririwa akisema “Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa
habari kwa muda mrefu, mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila
tatizo, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu ambayo mtahiniwa ili apate
nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B, daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
Wednesday, April 17, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)















