Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana U20 ya Nigeria (Flying Eagles).
Timu ya
Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying Eagles)
inatarajia kuwasili nchini leo (Julai 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwa
ndege ya RwandAir ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18.
Flying
Eagles itapambana na Ngorongoro Heroes katika mechi ya kwanza ya raundi
ya pili itakayofanyika Jumapili (Julai 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hiyo
ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 20 zitakazochezwa mwakani nchini Algeria
itachezeshwa na waamuzi kutoka Kenya wakati Kamishna ni Charles Masembe
kutoka Uganda.
Flying
Eagles inayofundishwa na kocha John Obuh, jana (Julai 24 mwaka huu)
ilicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) kwenye Uwanja wa
Amahoro jijini Kigali. Nigeria ililala bao 1-0.
Msafara wa
timu hiyo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Nigeria (NFF), Chris Green. Baadhi ya wachezaji walioko
katika kikosi cha Flying Eagles ni Chidi Osuchukwu, Alhaji Gero, Shehu
Abdullahi, Aminu Umar, Aliyu Mohamed, Uche Agbo, Jonah Usman, Harrison
Egbune, Hassan Abubakar na Yahya Adamu.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu
na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A
itakuwa sh. 10,000.
NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME
Nusu
fainali zote mbili za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati
(Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam
na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu
fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu
fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili
jioni.
via. dewjiblog.com
No comments:
Post a Comment