Mhe.
Benjamin Mkapa akiwasili hotelini tarehe 21 Julai 2012, kuhudhuria
Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington
D.C. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare
Maajar.
Mhe.
Benjamin Mkapa akisalimiana na Dr. Ellen Mkondya-Senkoro, Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS mara baada ya kuwasili
hotelini tarehe 21 Julai 2012, kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa
la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C.
Mhe.
Benjamin Mkapa akipewa taarifa na Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi
wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili Washington D.C
kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI kuanzia Julai 22-28,
2012. Wengine kwenye picha ni Dr. Ellen Mkondya-Senkoro, Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS na picha nyingine ni Ms.
Eileen A. Swai, Msaidizi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Mhe.
Benjamin Mkapa akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Washington
Convention Centre Julai 23, 2012 kuhudhuria Kongamano la XIX la
Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C.
Ma-Champion
wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa na
Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano wakifuatilia mojawapo ya
mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini
Washington. Pembeni ni Mhe. Mwanaidi SinareMaajar, Balozi wa Tanzania
Marekani na Dr. Ellen Senkoro wa Taasisi ya Benjamin Mkapa.
Pichani
Juu na Chini ni Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu wa
Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim
Chisano na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda wakijiandaa kabla
ya mjadala kuanza kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C.
Rais
Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa akihitimisha mjadala kuhusu
Mpango wa Tohara ya Hiari kwa Wanaume ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI
kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa mjini Washington D.C.
Washington
DC;Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amewaasa viongozi wa Nchi za Kiafrika kuchukua hatua ya
kuhamasisha jamii za kiafrika kuhusu mpango wa tohara ya hiari kwa
wanaume (Voluntary Medical Male Circumcision for HIV Prevention) kama
mojawapo ya njia ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI barani Afrika.
Mheshimiwa
Mkapa aliyasema hayo alipokuwa anahitimisha mojawapo ya mijadala ya
pembeni (Satelite Session) iliyokuwa inaendelea wakati wa Kongamano la
XIX la Kimataifa la UKIMWI linaloendelea Mjini Washington DC, Marekani
ambapo watu takribani 22,000 wanahudhuria. Mjadala huo uliovutia mamia
ya wajumbe hususan kutoka Afrika kuhusu tohara ya hiari kwa wanaume,
uliendeshwa na Bi. Brenda Wilson kutoka Afrika Kusini ulielezea tafiti
za kisayansi kuhusu mpango huo kama njia ya kupunguza maambukizi ya
UKIMWI.
Rais
Mkapa alisema mpango huu ni muhimu kutekelezwa na viongozi wa nchi za
Kiafrika kwani imethibitishwa na tafiti zilizofanyika kwa Waafrika
kwamba unapunguza maambukizi kwa asilimia 60, ambapo alisema si jambo
dogo katika harakati za kutokomeza UKIMWI. Aliongeza kuwa ni mpango
uliopendekezwa na sisi Waafrika wenyewe na ni wa hiari na hivyo hakuna
atakayeshurutishwa.
“Umebuniwa
na nchi za magharibi, lakini umetafitiwa na kuthibishwa na sisi
Waafrika wenyewe, hivyo ni mpango wetu huu” alisisitiza Rais Mkapa huku
akishangiliwa kwa makofi na wajumbe wa mjadala huo.
Ili
kutekeleza mpango huu wa tohara ya hiari kwa mafanikio, Mhe. Mkapa
alielekeza mambo matatu. Kwanza nchi za kiafrika inabidi zitengeneze
sera na mikakati madhubuti ya jinsi ya kukabiliana na janga hili la
UKIMWI. Pili mipango na mikakati hiyo imilikiwe na wananchi wa nchi
husika ili wao wenyewe wathibitishe ushiriki wao na sio kuonekana kama
shuruti .Na mwisho mipango na sera za kukabiliana na UKIMWI itekelezwe
kwenye mazingira ya ukweli na uwazi ili jamii za kiafrika ziweze
kutambua athari za janga hili la UKIMWI. Pia serikali nazo zitenge
fedha za kusaidia katika mapambano haya na si kutegemea fedha za
wafadhili tu.
“Umefika
wakati sasa dunia nzima ielekeze nguvu zake kwenye kutokomeza ugonjwa
huu hatari ambao unaua maelfu ya watu kila siku” Alisema Mhe. Mkapa na
kuongeza kuwa mataifa mbalimbali duniani hutoa misaada haraka sana mara
majanga ya dharura yanapotokea, kama vile mafuriko, ajali n.k. Lakini
janga la UKIMWI ni kama dharura inayoendelea na sasa ni wakati muafaka
dunia nzima itazame janga la UKIMWI kama dharura na inayoendelea.
Naye
Mwenyekiti mwenza wa Mpango wa Tohara ya Hiari wa PEPFAR Dkt. Emmanuel
Njeuhmeli alithibitisha tafiti hizo kwa kutoa mfano wa Zimbabwe ambapo
maambukizi ya UKIMWI yanakadiriwa kupungua kwa asilimia 45 ndani ya
kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mpango huo.
Wengine
walioongea katika mjadala huo ni Angelo Kaggwa (Uganda), Mhe. Dkt.
Speciosa Wandira (Uganda), Bi. Henrica Okondo (Kenya), Chifu Jonathan
Mumena (Zambia), Mhe. Oburu Oginga (Kenya), Mhe. Dkt. Christine Ondoa
(Uganda), na Mhe. Blessing Chebundo (Zimbabwe). Mjadala huo pia
ulihudhuriwa na marais wastaafu wanaojishughulisha na mapambano dhidi ya
Ukimwi ( wajulikanao kama Champions for AIDS Free Generation)Mhe.
Joachim Chisano, Rais Mstaafu wa Msumbiji na Mhe. Kenneth Kaunda, Rais
Mstaafu wa Zambia
Mhe.
Mkapa amehudhuria Kongamano hili kubwa la UKIMWI kwa mwaliko wa taasisi
ya Champions for HIV-Free Generation inayoongozwa na Rais Mstaafu wa
Botswana Mhe. Festus Moghae, ambapo Mhe. Mkapa ni mmoja wa Ma-Champion
nane wa taasisi hiyo.
Kongamano
la XIX la Kimataifa la UKIMWI limeanza Washington DC tarehe 22 Julai
hadi 28 Julai 2012 ambapo watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wa
Marekani wamehudhuria akiwemo Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Marekani
Julai 25, 2012
No comments:
Post a Comment