Mkoa wa Mara umevuka lengo la
wanachama waliojitokeza kukidhamini chama cha (ADC) ambapo jumla ya
wanachama waanzilishi 250 kutoka wilaya za Mkoa wa Mara walijitokeza
kukidhamini na kuizidi mikoa ya Mwanza,Tanga na Pemba ambapo tayari
chama hicho kimeshakwenda kutafuta wadhamini.
Mara baada ya kutangazwa kuvuka
lengo la wanachama walijitokeza kukidhamini chama kipya cha siasa hapa
Nchini cha Alliance Democratic Change (ADC) shughuli iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Musoma club Kaimu Katibu mkuu wa chama cha
ADC Kadawi Lucas Limbu aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa
wingi na kuonyesha ni namna gani walivyo tayari kwa ajili kutaka
mabadiliko.
Ujio wa chama hicho unatajwa
kuja mara baada ya vyama vingi vya siasa vilivyoanzishwa hapa nchini
kuonekana kuwa na ubinafsi na kushindwa kuwashirikisha viongozi wengine
katika ngazi za chini hasa kwenye masuala ya ruzuku na
uwezeshaji pamoja na vyama hivyo kushindwa kufikia malengo ya kuanzishwa
kwake na kutokukidhi yale ambayo wananchi wanayatarajia kutoka katika
vyama hivyo.
Kwa mujibu wa viongozi wa ADC,
Chama hicho kinatarajia kuwa mfano wa kuigwa katika kuwashirikisha
wananchama wake na viongozi katika kada zote na iwapo chama cha hicho
kitakamilisha masharti waliyopewa na ofisi ya msajili wa vyama vya
siasa hapa nchini, kitakuwa chama cha 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment