Inawezekana taarifa za ajali ya
boti ya Seagul iliyotokea leo mchana Zanzibar ukawa umezisikia au
kuzisoma sehemu mbalimbali lakini kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani
imetoka muda mfupi uliopita.
Waziri Emmanuel Nchimbi
akiongea na TBC1 amesema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa
jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha
au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa
zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai
na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu,
juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”
Habari http://millardayo.com
No comments:
Post a Comment