Madiwani 22 wa CCM wa wilaya ya Misungwi (mkoa wa Mwanza) wamejiorodhesha na kutishia kutaka kuhamia CHADEMA kutokana mgogoro uliopo kati yao na viongozi wa CCM wilaya, Tanzania daima leo limeripoti. Uamuzi huo unatokana na Kamati ya siasa ya Mkoa na wilaya kumshinikiza Mkiti wa Halmashauri hiyo Mr Benard Policarp kujivua gamba kutokana na tuhuma za ufisadi wa fedha umma.
Hata hivyo, madiwani 22 kati ya 36 hawakubaliani na kamati hizo za siasa kwa madai kuwa uchunguzi wa kina ufanyike kwanza, ndipo uamuzi wa kumshinikiza M/kiti wao ajiuzulu ufuate, kwa kuwa hakuna uthibitisho uliopatikana dhidi yake hadi sasa. kwa mujibu wa taarifa hizo, ambazo zimethibitishwa na baadhi ya madiwani hao, tayari wamekwishajiorodhesha na kata wanazotoka na wamedhamiria kuipeleka majina yao makao makuu ya CCM.
Leo (jana) madiwani hao walitaka kuandamana kudai mali zao walizokuwa wakichangia Chama hicho lakini walikwama baada ya magari ya FFU kuzagaa kwa lengo la kupambana nao.
Mmoja wa madiwani hao (gazeti laficha jina) alisema muda wo wote watahamia Chadema kuanzia sasa.
Chanzo cha mtifuano.
Ripoti ya CAG ilionesha kuwa halmashauri hiyo ilikuwa na ripoti mbaya ikionesha ufisadi wa Bil 5. Waziri mkuu Pinda aliagiza mkurugenzi ashushwe ( + jirani wa sengerema) wote wameshushwa vyeo.
Baada ya hapo viongozi wa CCM (wilaya + mkoa) kupitia kamati za siasa wakahamisha bifu kwa m/kiti wa Halmashauri hiyo bila ushahidi wo wote, hata hivyo madiwani 22 kati ya 36 wakaamua kumkingia kifua ikibidi kwa gharama ya kuhama naye kwenda CHADEMA kutetea haki yao mpaka uchunguzi wa kina ufanyike kwanza.
My take;
Kama bifu linaanza mapema namna hii, kura ya maoni ya ndani ya CCM 2015 itakuwaje?
Pili, hivi Chadema isingekuwa na nguvu wangeweza kuwa na ujasiri huo walio nao sasa?
Wednesday, July 25, 2012
Madiwani 22 CCM Misungwi wajiandikisha kuhamia CHADEMA
MWARICK JAPHET MUJUNGU
Web Developer
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment