Maafisa wa serikali nchini Ivory Coast wanasema takriban watu 60 wamefariki wakati wa mkanyagano wa sherehe za mwaka mpya mjini Abidjan.
Wengine 50 walijeruhiwa katika mkasa huo ambao ulitokea mapema Jumanne
katika wilaya ya Plateau kwenye uwanja wa mpira ambapo watu
walikusanyika kujionea fataki zikirushwa kuukaribisha mwaka mpya.
Televisheni
ya AIP nchini Ivory Coast inaripoti kwamba wengi wa waathirika walikuwa
vijana. Wazazi wakiwa na huzuni walikwenda kwenye uwanja wa mpira
wakiwatafuta watoto wao.
Walioshuhudia wamesema polisi walijaribu kuwadhibiti watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya lakini vurumai zilizuka na kusababisha watu kukanyagana. Haikufahamika mara moja ni nini kilikuwa chanzo cha mkanyagano huo
Rais Alassane Outtara wa Ivory Coast ameeleza kuwa vifo vya watu hao ni msiba wa kitaifa na amesema uchunguzi utafanyika.
No comments:
Post a Comment