Muigizaji maarufu Swahiliwood Flora Mvungi amesema kuwa bifu lake na
muigizaji mwenzake Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole haliwezi kuisha
hivi hivi kama shilole hatamuomba msamaha na kwenda kukiri kwenye
magazeti kwa alichokisema ambacho kilionekana kumkera sana
Flora.Swahiliworldplanet lilimtafuta Flora na kumuuliza kama yeye na
Shilole wakipatanishwa wanaweza kuondoa tofauti zao na kuwa mashostito
walioshibana kama mwanzo, Flora alijibu "Mi sina tatizo but ili mambo
yawe sawa ni lazima aniombe msamaha mimi na H.baba kwenye hayo hayo
magazeti ambayo alienda kuongea upuuzi la sivyo hayawezi kuisha na
sitaki kusuluhishwa kimya kimya, waandishi waitwe akiri alichofanya
mambo yawe wazi na baada ya hapo yatakuwa yameisha". Shilole na Flora
walikuwa mabest wakubwa huko nyuma lakini wakaja kuwa chui na paka,
shilole anadaiwa kumponda Mvungi pamoja na mwandani wake H.Baba kuwa
Flora hana maendeleo yoyote tangu aanze uhusiano wake na H.Baba amekuwa
anamsikiliza sana huyo H.Baba kama mungu mtu kiasi cha kushindwa
kujijengea maisha yake yeye mwenyewe kwasababu anamtegemea na
kumsikiliza kwa kila kitu.kwa upande mwingine mastaa hawa wa filamu
waliiingia kwenye mtifuano mkali baada ya Flora kudaiwa yeye ndiye
alimpokea Shilole na kuishi wote nyumbani kwake miaka kadhaa nyuma
wakati shilole anatoka kwao kuja mjini kutafuta maisha lakini Shilole
amemgeuzia kibao Flora kuwa asijitape yeye ndio alimpokea Flora mjini na
kuishi nae nyumbani kwake.Pia hivi karibuni Flora alikaririwa na gazeti
moja akisema "Shilole ananuka wanaume". Hatukufanikiwa kumpata shilole
ili kumuuliza kama yupo tayari kuyamaliza wakipatanishwa lakini bado
tunamsaka atoe yaliyo moyoni mwake....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment